Tangazo la TAMISEMI Kuhusiana na uhamisho

Tangazo la TAMISEMI Kuhusiana na uhamisho

mkumbwa junior

JF-Expert Member
Joined
Oct 22, 2014
Posts
853
Reaction score
1,702
jamani kuna Tangazo la TAMISEMI nimeliona halmashauri ya Masasi linahusiana na maswala ya mwajiriwa anayehitaji kuhama kwa gharama zake mwenyewe
linadai eti yabidi utume barua moja kwa moja kwa Katibu wa TAMISEMI na wakatoa namba za simu za Bwana mmoja Anayeitwa Mr.Juma Bakari kwa ambao hawajaelewa utaratibu nilipompigia huyo Mr.akanipa Taratibu zote na akaniambia inatakiwa niandae LAKI SITA kama gharama za ofisa atakaye shughulika na swala hilo ambapo fedha hiyo ni gharama ya usafiri na malazi ya Ofisa atakaye ni shughulikiaa
sasa sijajua kama ni kweli au ni Matapeli hebu anayefahamu utaratibu tujulishane
 
Watumishi wengine utadhani hawajawahi kuingia darasani,hivi hata kwa akili ya darasa la nne unashindwa kugundua huo ni utapeli?
 
Kwahiyo ukituma barua akiisaini ndo amesafiri? Wakishughuliiaga uhamissho hapo TAMISEMI kuna usafiri? Tuma hizo hela uibiwe
 
mi mwenyewe nilihisi ni wezi ila cha kuchangaza wamebandika matangazo kama 5 ofisi za Elimu wilaya na mengine mengii tu kwenye NOTICE BOARD zote za wilaya sasa nikakiuliza ina maana watumishi wa idara ya Elimu huwa hawasomi hayo matangazo??ili wayatoe au watoe taarifa kwa uma kwamba ni utapeli maana wameyabandika mengii
 
Hiv unataka tapeli hadi ajitangaze? hilo n tangazo tosha kuwa yeye ni tapeli :
 
Back
Top Bottom