Automata
JF-Expert Member
- Mar 3, 2015
- 3,349
- 4,620
TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI
Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro (NCAA) inapenda kuwataarifu waombaji kazi wote walioomba kazi zilizotangazwa mwezi Desemba, 2107 kuwa, usaili unatarajiwa kuendeshwa kuanzia tarehe 3 – 8 Februari, 2018 na hatimaye kuwapangia vituo vya kazi waombaji kazi watakaofaulu usaili huo.
Wasailiwa wanaoitwa kwenye usaili wanapaswa kuzingatia maelekezo yafuatayo:-
i. Usaili wa Mchujo utafanyika tarehe 3 Februari, 2018 kama ilivyoainishwa kwenye tangazo hili, muda na sehemu usaili ambapo usaili utafanyika umeainishwa kwa kila Kada;
ii. Kila Msailiwa anapaswa kuwa na kitambulisho kwa ajili ya utambuzi;
iii. Vitambulisho vinavyokubalika ni pamoja na:- Kitambulisho cha Mkazi, Kitambulisho cha Mpigakura, Kitambulisho cha kazi, Kitambulisho cha Uraia au Hati ya kusafiria;
iv. Wasailiwa wanatakiwa kufika na VYETI VYAO HALISI, kuanzia cheti cha kuzaliwa, kidato cha IV, VI, Stashahada, Stashahada ya Juu, Shahada na kuendelea kutegemeana na sifa za Mwombaji;
v. Wasailiwa watakaowasilisha“Testimonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati za matokeo za kidato cha IV na VI (form iv and form vi results slips) HAVITAKUBALIWA NA HAWATARUHUSIWA KUENDELEA NA USAILI;
vi. Kila msailiwa atajigharamia kwa chakula, usafiri na malazi;
vii. Kila Msailiwa azingatie tarehe na mahali alipopangiwa kufanyia usaili;
viii. Kwa waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe Vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na mamlaka husika (TCU, NACTE na NECTA); na
ix. Waombaji kazi ambao majina yao hayakuonekana katika tangazo hili watambue kuwa hawakukidhi vigezo. Hivyo, wasisite kuomba tena pindi nafasi za kazi zitakapotangazwa na kuzingatia mahitaji yaTangazo husika.
x. Kwa kada ambazo wanatakiwa kusajiliwa na Bodi zao za Kitaaluma wanapaswa kuja na vyeti vyao Halisi vya Usajili pamoja na Leseni za kufanyia kazi.
Kuona orodha ya majina ya walioitwa kwa ajili ya usaili pakua nyaraka ya hapo chini