Muda wa SAA 8:15 mchana nikiwa maeneo ya Liberthi kuhemea bidhaa wakati naelekea Nyengezi round about ya Liberthi lilitokea gari la CHADEMA likiwa na bendera na speaker zikitangaza mkutano k esho tarehe 20/5/2015 kwamba mkutano utahutubiwa na Ezekiel Wenje na mbuge mtarajiwa wa Morogoro Afande Selle!! Ilifikia hatua nikawaza hivi leo ni siku ya wajinga duniani am a ndizo siasa za majitaka!!? Wakuu hili si jambo la kutania ni kweli kabisa na Mimi nafahamu Wenje ni CHADEMA wakati Afande Selle ni ACT WAZALENDO. Nilijaribu kulipiga picha lakini likawa limetokomea huku Mimi nikihofia kuibiwa mizigo na msukuma mkokoteni aliyekuwa ananipelekea mizigo stand ya Igombe Lwagasole ili ninyoke Nyengezi.