Tangazo la ajira

Dec 12, 2021
7
9
TANGAZO TANGAZO

Kampuni ya AQUARIAN PROJECT SOLUTIONS iliyoko jijini Mwanza kupitia LILIAN KITCHEN CATERERS na DW CLEANING SERVICE inapenda kutangaza nafasi za ajira kama ifuatavyo

Nafasi 20 za kazi ya usafi (wafanya usafi) katika chuo kikuu Mjini Musoma

Majukumu ya kazi
1. Usafi wa mazingira ya nje (Kuhakikisha mazingira yanakuwa safi muda wote)
2. Usafi wa maofisi pamoja na thamani za ofisi kama vile meza, viti nk
3. Usafi wa Vyooni
4. Usafi wa majengo
5. Usafi wa bustani, utunzaji na upandaji maua.

Nafasi 20 za kazi ya uhudumu mgahawa wa chuo kikuu Mjini Musoma

Majukumu ya kazi
1. kuhudumia chakula kwa wateja
2. Usafi wa mgahawa pamoja na mazingira yanayozunguka
3. Usafishaji vyombo vya chakula

Nafasi 10 za nafasi ya upishi katika mgahawa wa chuo kikuu Mjini Musoma

Majukumu ya kazi
1. Upikaji wa vyakula aina mbali mbali kwa ajiri ya kifungua kinywa, mchana na usiku
2. Usafi wa mgahawa na mazingira yanayozunguka

vigezo vya muombaji
1. Awe Mtanzania
2. Umri kati ya miaka 20 mpaka 30
3. Jinsia ya kiume au ya kike
4. Muombaji awe na elimu ya sekondari au elimu ya kazi husika na anayejua kusoma na kuandika
5. Muombaji awe tayari kuishi Musoma
6. Muombaji awe tayari kupimwa afya katika magonjwa kama kifua kikuu, Homa ya Ini na Ukimwi.
7. wenye uzoefu wa kazi watapewa kipaumbele
8. wakazi wa Musoma na kanda ya ziwa watapewa vipaumbele

Maombi ya kazi yatumwe kupitia

email: recruitment@aquarian.co.tz

watsup no: 0747851120

maombi yaambatane na kichwa cha habari cha nafasi husika inayoombwa.

Hakuna gharama za uombaji kazi..epuka matapeli.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom