Deadbody
JF-Expert Member
- May 30, 2015
- 4,274
- 6,592
KUELEKEA BARAZA KUU LA CHADEMA TAIFA KESHO MARCH 12 2016
Na Shirima Juvenal
Wakati ambapo BARAZA KUU LA CHADEMA Taifa linakaa likiwa na agenda mbili ambapo mojawapo ni kumpata katibu mkuu mpya ambaye ataziba pengo lililoachwa wazi na Dr Slaa mwaka Jana Mara baada ya kuachana na CHADEMA na siasa kwa ujumla. Katika kuelekea katika uchaguzi wa majina mawili yatakayowasilishwa na mwenyekiti taifa Freeman Aikael Mbowe ili jina moja liidhinishwe kwa kupigiwa kura na wajumbe wa Baraza Kuu.
Naamini katika majina mawili yatakayowasilishwa kesho yatakuwa miongoni mwa: fedrick Turwawey Sumaye, Benson Singo Kigaila, Mabere Nyaucho Marando, Salum Mwalimu, Ezekiel Wenje, Dr Marcus Albanie, Wilfred Muganyizi Lwakatare, Tundu Antipas Mughuay Lissu, Peter Msigwa na John John Mnyika. Ingawa majina hayo yote ni ya viongozi wazuri lakini Naamini mwenyekiti taifa Freeman Aikael Mbowe amezingatia vigezo vifuatavyo ambavyo pia wajumbe wa BARAZA KUU mnapaswa kuzingatia ili kumpata katibu mkuu atakayetuvusha 2020 kama ifuatavyo:
1. Umaarufu wa katibu. lazima tutakaye mchagua awe anajulikana Tanzania nzima mpaka kule Sigimbi asiwe mtu ambaye akiitisha mkutato wa kisiasa wanakuja watu mia moja kama ndugu yangu mwigamba wa ACT. Lazima watanzania wavutiwe kwenda kumuona kama alivyokuwa Dr Slaa Lazima awe zaidi ya kinana na wenzie.
2. Uwezo wa kidiplomasia lazima katibu mkuu ajaye awe anajulikana nje ya nchi tutegemee kumuona kwenye vikao na vyama wshirika wetu kama Conservative, CDF, FDC, Republican, Democratic, ODM, TNA, akituwakilisha. Tusije tukachagua mtu ambaye hata ukitafuta Wikipedia historia yake haipo.
3. Asiwe na matamanio ya kugombea au kuwa na nyadhifa ndogondogo kama udiwani na ubunge ili aweze kutulia kutulia ofisini kuratibu shughuli za chama kunadi wagombea na kuendesha mikutano na kampeni nchi nzima. Ili katibu ajaye aweze kufanya shughuli za kisiasa nchi nzima bila ya vikwazo vya kuhangaika kuhudumia pia jimbo lake (must be freely available for any office works). Sisi tu Mashahidi kwamba makao makuu yetu yalidorora sana kwa sababu katibu hakuwepo manaibu katibu wote Walikuwa wagombea hivyo kama tusingekuwa na mh Sumaye Kingunge, Masha, Prof Safari, Prof Baregu, Said Issa Mohammed, TwahaTaslima, Habib Mnyaa na bibi Fatma kampeni zingekuwa ngumu sana ilihali ukizingatia Mh Mbowe Mh Mbatia Mh Makaidi nao Walikuwa wagombea.
4. Aifahamu CCM na mawakala wake vizuri simanishi tu kuwajua kwa jina Bali kuweza kuijua mipango yao pia kuweza kujua mbinu za kuweza kuikabili ipasavyo ni vigumu sana kuangamiza ugonjwa kama hajui chanzo chake sahihi. Lazima aweze kujua vizuri sana CCM inavyofanya kazi zake.
5. Lazima aijue ipasavyo mifumo ya kiusalama wa taifa kama vile polisi, JWTZ, magereza, uhamiaji, navy, mgambo, JKT na Usalama wa taifa kwani huwezi kushinda dola bila kuiteka hiyo mifumo pia ili uweze kuiondosha CCM. Sijaona dola yoyote inadondoshwa na upinzani usiokuwa na mgombea na uongozi imara wa upinzani mfano Kenya.2002 Kibaki aliwahi kuwa makamu wa Rais (1978-1988) Nigeria 2015 Buhari aliwahi kuwa Rais na mkuu wa majeshi Malawi 2014 Peter Mutharika alikuwa kaka wa Bingu wa Mitharika Senegal 2014 Miki Saley IvoryCoast Alasan Watar Zambia 1991 Fred Chiluba nk wote hao walifanikiwa kwa kuwa na viongozi wa chama na wagombea walioasiwa na vyama tawala.
6. Awe na umri wa kutosha busara za hali ya juu ili asiwe anaandamwa na majukumu ya kifamilia kama malezi ya watoto uwezo wa kuamua mambo kwa busara na weledi usiokuwa kuwa na ukinzani wote.
7. Lazima aheshimike na viongozi wengine wa ili aweze kutimiza majukumu yake asiwe mgomvi Wala mvurugaji.
8. Awe anauwezo wa kiutawala na kiuongozi ili aweze kumudu vikao vya makubaliano maridhiano mfano UKAWA, vikao vya Secretariat, kamati Kuu, Baraza Kuu, kusimamia haki, chaguzi za ndani na kutatua migogoro ya ndani na nje ya chama.
9. Mwaminifu na mchukia rushwa ili aweze kusimamia fedha na mali za chama na taifa kwa ujumla lazima awe na moyo wa kupambana na rushwa na udhalimu wa chama cha mapinduzi (CCM).
10. Lazima awe na uwezo kiuchumi ili asitegemee tu posho za chama ili asijekununuliwa na CCM kama tulivyoshihudia kwa kina Dr Kaborou na Dr Slaa ambao wote wamekuwa makatibu wakuu waliofuatana mtawalia lakini wakatusaliti.
11. Tusiendeshwe na propaganda za CCM za ukanda ukabila udini udhehebu wala umikoa bali tuzingatie uwezo wa mtu na usahihi wa uteuzi wa mhusika anayefaa kufuata hayo ni kuhalalisha dhambi mbaya sana ya ubaguzi ambayo ilikemewa sana na baba wa taifa Mwal Nyerere.
Kwa kuhitimisha niwatakieni Baraza Kuu jema na lenye mafanikio mema chini ya uongozi shupavu wa mh mwenyekiti taifa Freeman Aikael Mbowe, na wajumbe wa kamati Kuu wote bila kuwasahau Mh Edward Lowassa Mh Fedrick Sumaye (mawaziri wakuu wastaafu na wajumbe wa kamati Kuu), Mzee kingunge Ngombale Mwiru, Babu Juma Duni Haji (Mgombea mwenza), Maalim Seif Sharif Hammad (katibu mkuu CUF makamu wa kwanza wa Rais Zanzibar na Mgombea urais wa UKAWA Zanzibar), James Mbatia(mwenyekiti NCCR) na marehemu Dr Emmanuel Makaidi(mwenyekiti NLD) na wengine wote kwa kazi nzuri iliyotufikisha oktoba 25.
Imeandikwa na;
Shirima Juvenal
0752360618 & 0654608929
Dar es Salaam Tanzania.