dafity
JF-Expert Member
- Aug 16, 2008
- 1,881
- 2,091
Nimekutana nayo hii habari Facebook na kwa kweli hili tangazo linadhalilisha wanawake. Silipendi kweli. Mwenye "Audio" yake iweke hapa please.
Linatangazwa sana kwa sasa na limeandaliwa na wanaojiita "EQUALITY FOR GROWTH" likidhaminiwa na "UN Trust Fund".
Lengo lao ni kukataa kuwatukana na kuwadhalilisha wanawake lakini kwa bahati mbaya wao ndio wanawatukana waziwazi kwenye tangazo hilo.
Kwenye tangazo anasikika mwanaume akienda kunywa supu kwenye kibanda cha mwanamke lakini yule mwanaume alivyodaiwa pesa akaanza kuporomosha matusi ya kikwelikweli ambayo hapa siwezi kuyaandika. Matusi ambayo watoto huyasikia na kujifunza kitu kibaya kutoka redioni.
Nashauri TCRA walifungie hili tangazo haraka kama walivyofungia baadhi ya nyimbo zisizo na maadili.
HAWAKUPASWA KUTUKANA KIKWELIKWELI ILI KUNOGESHA TANGAZO. TUSI NI TUSI TU. WAWE NA ADABU!