Tanganyika irudi, Zanzibar inaanza kukata mbuga

Tanganyika irudi, Zanzibar inaanza kukata mbuga

Mwiba

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2007
Posts
7,607
Reaction score
1,760
Baada ya kusikiliza mkutano wa Paje -Unguja niliiona wazi njia ya Zanzibar kujikwamua na ukoloni Tanganyika ni nyeupe ,na gea walioondokea na mkutano huu wa Paje kwa kweli wamekusudia kwa hali yeyote ile Mamlaka kamili ya Zanzibar yanarudi chini ya Uongozi wa CUF.

Hisia kali zinazotolewa na Katibu Mkuu wa CUF ni hisia ambazo kila Mzanzibari mzalendo ataungana nae na haswa aliposema CCM wajiandae kisaikolojia kwani ushindi mkubwa ambao utavuka kiwango utaiangamiza CCM.

Jingine ni pale alipotangaza waziwazi kuwa Serikali itakayoongozwa na CUF haitafuata wala kusikiliza firimbi zitakazopulizwa Tanganyika aka Serikali ya Muungano ,wao kama WaZanzibari watakuwa na maamuzi yao kiserikali na hawatamsikiliza yeyote yule kutoka nchi nyingine (Tanganyika).

Hotuba yake imejenga matumaini 100% kwa WaZanzibari na imetangaza kuwa miezi tisa ijayo ni kuiangamiza CCM Zanzibar' kama una nafasi sikiliza hiki kipande sehemu ya mwisho baada ya Mansori. Ameukandia utawala wa mafisadi na kudai hakuna kitakachozuia CUF isiongoze Zanzibar ,hakuna na atakae jaribu atajuta.

Last edited by a moderator:
Tanganyika ndiye bwana mkoloni wenu mtake msitake mtakoloniwa tu.
 
Tanganyika ndiye bwana mkoloni wenu mtake msitake mtakoloniwa tu.

Tatizo bado upo usingizini ,ukimaliza hangup utaelewa ni wapi upepo unaelekea. WaZanzibari wamejitambua na sasa huwezi na hakuna nguvu za kibinadamu zinazoweza kuwasimamisha ,umesikia kilichotokea leo tega sikio ITV kwenye taarifa ya habari saa mbili. Leo Zanzibar imetetemeka na kutetemesha umma. Endelea na fikra mgando.
 
Tanganyika yetu, wapi?

Tanganyika ipo ila mafisadi hawataki hata kuisikia ,kwani ndio itakuwa safari yao ya kuelekea Jela ,ama wakimbie kusikojulikana ,ila ikijulikana wamekwenda wapi tutawatweet warudi au tutatumia SMS warudishwe kwa haraka kwani watakuwa na kesi si ya bali za kujibu.

Ila kama wewe ni mwenye kuipenda TANGANYIKA kama mimi basi anza kufurahia bila ya shaka yeyote ile Wazenji wataturudishia kwa mikono miwili na kama hatuitaki watatutupia.
 
Daah inakera sana! Escrow inatusumbua, panya road wanatutesa, Tanganyika wameikataa kabisa, katiba wamechakachua! hatusifiki kwa biashara ya Tanzanite bali cocain, kiporo alichowekewa Muhongo hakitaki kuchacha, nasikia Kenya wamekataza magari ya Tz kuingia uwanja wa ndege wa Jomo Kenyata! Mikopo ya chuo bado kitendawili, elimu ndo Mukulo type.... aah nikitamani maisha ya ulaya naambiwa sina uzalendo sasa huo uzalendo mimi nitautoa wapi ndugu zangu? sikufunzwa uzalendo mimi wala sijawahi kufunzwa! mmenidumaza kifikra ili nisifikiri sawa sawa, huo uzalendo ntautoa wapi ndugu zangu? poa tu CCM si ndo mmeamua kunifanyia hivi bhana, fresh tu! ila mjue ndo mnatuandaa hivi "october is not far from now"(sijui nimepatia?)
 
Ndio maana Wazenji wanajiengua kiana ,nina hakika kuna magogo ya CCM wataikimbia CCM katika dakika za mwisho na kurukia jahazi ya UKAWA na haswa huko Zanzibar ,fununu zimeanza kuwa wanaoonekana wahafidhina wa CCM watakiwacha mkono chama hicho pia wapo viongozi wa ngazi za juu ,hao wamebana kimya kuchungulia kinachoendelea ila wenyewe CUF wanawajua na wengine wameambiwa wasifanye haraka watulie tuli kama Nunda chini ya kitanda.
 
Biblia inasema kuwa ni Mungu aliyeufanya moyo wa Farao uwe mgumu ili ishara na miujiza yake zidhihirike! Moyo mgumu wa CCM unatoka kwa Mungu ili hatimaye ifikie mwisho wa enzi yake na Tanganyika yetu irudi!
 
Wazanzibar wanataka mamlaka yao yaliyoporwa na mkoloni mweusi kupitia muungano.
 
Kutawaliwa na Mtanganyika ambaye hakubaliki EA nzima kwa ubinafsi ni fedheha kubwa kwa wazanzibari.
 
Ccm wameshatuua sana, kipindi cha uchaguzi viongozi wote hua wanakuja zanzibar kwa kujihakikishia kwamba bara wamepita. Sasa huku bara imekua kizaa zaa ni zamu ya cuf kwa upande wa zanzibar. Kitu muhimu kwao ni kujipanga tu
 
Asante mkuu. mada ndio hiyo na hainapingamizi huku kwetu.Mamlaka kamili ndio mtindo uliopo.
 
Kama mnasema kwamba watu wanaenda mbele hawarudi nyuma ,basi mwaka huu Zanzibar wanaweka rekodi ya kurudi nyuma ,Tanganyika watairudisha na kama hamuitaki watawatupia ,muongozwe na mafisadi.
 
Hawa wakileta fujo tutawateka tu na kuwa na rais moja hizi shida nyingine ni za kujitakia tu.
 
Back
Top Bottom