Tanganyika inateketea

Madin matupu kaongea asee ,

Maneno machache yenye ujumbe mkamilifu
 
Mkapa alimqambia Magufuli kuwa ile ni serikali ya CCM, si serikali ya Magufuli.

Samia anarudia yaleyale.
 
Your browser is not able to display this video.

Your browser is not able to display this video.

Your browser is not able to display this video.

Your browser is not able to display this video.
 
JE, MUUNGANO NA TANGANYIKA VIMEBAKIA KUWA MFUPA WAKATI ZANZIBAR INANAWIRI?

Kila mtu anaweza kutafsiri tofauti kazi yoyote ya sanaa ingawa maana iko kwa mtunzi. Tafsiri yangu kwa hiki kikaragosi (katuni) cha Masoud Kipanya ni hii: Skeleton (huyo samaki mkubwa aliyebakia mkia na kichwa) huonyesha Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (iliyowakilishwa kama kichwa) na Tanganyika (iliyowakilishwa kama mkia).

Samaki wadogo walionenepeana ni Zanzibar (samaki mkubwa kidogo) na Visiwa vya Unguja na Pemba (samaki hao wadogo) pamoja na visiwa tegemeo ambavyo huunda Zanzibar. Wanaonekana siha au afya yao inatokana na wao kupata lishe kwa kumla samaki mkubwa.

Tafsiri hii katika literature (fasihi) ndio ambayo tunaita reader response ikiwa na maana kuwa msomaji anaweza pia kutoa maana yake katika kazi ya faisihi hasa ambayo mtunzi wake yuko mbali au hawezi kuwa huru kufafanua maana.

Tafsiri yangu inakwenda na muktadha na siku ambayo kikaragosi hiki kimetolewa, tarehe 12 Januari 2026 ambayo ni siku ya maadhimisho ya miaka 62 ya Mapinduzi ya Zanzibar. Lakini kama wewe huamini katika uhuru wa kazi za fasihi waweza kwenda kumtia pingu Kipanya hata 'kumpilipili' Askofu Mwamakula ambaye ndiye mchambuzi wa kikaragosi cha Kipanya.
Je, nini kimekushangaza? Je, nini maoni yako?

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandakile Mwamakula
Itunge, Dar es Salaam; 12 Januari 2026; Saa 12:03 asubuhi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…