Tanga: Walimu wanaobeza elimu bure kukiona

Sinoni

JF-Expert Member
May 16, 2011
5,531
9,144
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mwantumu Mahiza ametangaza ‘vita’ dhidi ya walimu watakaobainika kutofundisha kwa wakati darasani kwa kisingizio cha mpango wa Serikali wa elimu bure.

Mahiza alitoa kauli hiyo wakati akifungua kikao kilichoitisha kwa ajili ya kuweka mikakati ya kikazi na wakuu wa shule, wakurugenzi wa halmashauri na maofisa elimu wa sekondari mkoani Tanga.

Alisema baadhi ya walimu katika shule za msingi na sekondari wamekuwa wakitegea kufundisha na wanapofuatwa na wanafunzi huwajibu hiyo ndiyo elimu bure. “Wanawaambia wanafunzi subirini tu mtaisoma namba mwaka huu,” alisema Mahiza.

Alisema lugha hizo za kuwasimanga wanafunzi ni sawa na kuidhalilisha Serikali jambo alieleza kuwa hatakubali litokee tena. “Nitawaweka kizuizini walimu watakaotegea au kubainika kutoa lugha za kuitusi Serikali kuhusu mpango wa elimu bure, nitatumia Sheria Namba 8 ya Usalama ya Mwaka 2010 kwani huko ni kuhujumu elimu,” alisema Mahiza.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, George Simbachawene alisema Serikali imetenga Sh131.4 bilioni ikiwa ni fedha za ruzuku ya uendeshaji wa shule, chakula, mitihani na fidia ya ada.

Alisema Serikali imejipanga kugharamia uendeshaji wa shule ili kuziba pengo la ada na michango mbalimbali iliyokuwa inatolewa na wazazi na walezi.

Chanzo: Mwananchi
 
Tanga. Mkuu wa Mkoa wa
Tanga, Mwantumu
Mahiza ametangaza
‘vita’ dhidi ya walimu
watakaobainika kutofundisha kwa wakati darasani kwa
kisingizio cha mpango wa Serikali wa
elimu bure.

Mahiza alitoa kauli hiyo
wakati akifungua
kikao kilichoitisha
kwa ajili ya kuweka
mikakati ya kikazi na
wakuu wa shule,
wakurugenzi wa
halmashauri na maofisa
elimu wa sekondari mkoani Tanga.

Alisema baadhi ya
walimu katika shule za
msingi na sekondari
wamekuwa wakitegea kufundisha na wanapofuatwa na wanafunzi huwajibu hiyo ndiyo elimu bure.
“Wanawaambia
wanafunzi subirini tu
mtaisoma namba
mwaka huu,” alisema Mahiza.

Alisema lugha hizo za
kuwasimanga wanafunzi ni sawa na
kuidhalilisha Serikali jambo alieleza kuwa
hatakubali litokee tena.
“Nitawaweka kizuizini
walimu watakaotegea
au kubainika kutoa lugha za kuitusi
Serikali kuhusu
mpango wa elimu bure,
nitatumia Sheria Namba
8 ya Usalama ya Mwaka 2010 kwani
huko ni kuhujumu
elimu,” alisema Mahiza.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, George Simbachawene
alisema Serikali imetenga Sh131.4
bilioni ikiwa ni fedha za
ruzuku ya uendeshaji
wa shule, chakula, mitihani na fidia ya ada.

Alisema Serikali
imejipanga kugharamia
uendeshaji wa shule ili
kuziba pengo la ada na
michango mbalimbali
iliyokuwa inatolewa na
wazazi na walezi.

Chanzo: mwananchi online

Hawa wakuu wa mikoa nao wamekuwa majipu, wanafanya kazi kwa vitisho, kwanini wasiende kwa hao waliowaona wanakiuka na kuwachukulia hatu badala ya kupoteza muda majukwani?
 
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mwantumu Mahiza ametangaza ‘vita’ dhidi ya walimu watakaobainika kutofundisha kwa wakati darasani kwa kisingizio cha mpango wa Serikali wa elimu bure.

Mahiza alitoa kauli hiyo wakati akifungua kikao kilichoitisha kwa ajili ya kuweka mikakati ya kikazi na wakuu wa shule, wakurugenzi wa halmashauri na maofisa elimu wa sekondari mkoani Tanga.

Alisema baadhi ya walimu katika shule za msingi na sekondari wamekuwa wakitegea kufundisha na wanapofuatwa na wanafunzi huwajibu hiyo ndiyo elimu bure. “Wanawaambia wanafunzi subirini tu mtaisoma namba mwaka huu,” alisema Mahiza.

Alisema lugha hizo za kuwasimanga wanafunzi ni sawa na kuidhalilisha Serikali jambo alieleza kuwa hatakubali litokee tena. “Nitawaweka kizuizini walimu watakaotegea au kubainika kutoa lugha za kuitusi Serikali kuhusu mpango wa elimu bure, nitatumia Sheria Namba 8 ya Usalama ya Mwaka 2010 kwani huko ni kuhujumu elimu,” alisema Mahiza.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, George Simbachawene alisema Serikali imetenga Sh131.4 bilioni ikiwa ni fedha za ruzuku ya uendeshaji wa shule, chakula, mitihani na fidia ya ada.

Alisema Serikali imejipanga kugharamia uendeshaji wa shule ili kuziba pengo la ada na michango mbalimbali iliyokuwa inatolewa na wazazi na walezi..source Mwananchi
 
Back
Top Bottom