Septemba11
JF-Expert Member
- Jan 18, 2013
- 620
- 535
Kuna kibao tu kimeandikwa "Karibu Tanga" huku maeneo ya Pongwe..lakn hakuna kibao cha "Kwa Heri Tanga"....mana ukingia hutoki
Ndio raha zenyewe za Tanga hizo mkuu, Tanga yetu ni njema, atakaye aje! Hatuna kwaheri huku, ukija waambiwa karibu, ukiondoka twakuambia karibu!
Nilikula chapati kwa mama ntilie Tanga, chapati imekwandwa na nazi, ukifunga inafunguka kama kurasa za kitabu. Ile chapati sijawahi kuiona mahali popote. Chezea Tanga wewe.
Phew! nilikuwa nazipitia post zote huku roho ikinidunda kwa kasi ya ajabu nikidhani mie na familia yangu tumelamba misumu miaka yote hiyo! nimetetemekaje?
Yani wewe umewaza vibaya kama mimi lolz.. Yani nilisikia tumbo lanikata. Nkajua tayari uziii unaleta habari za maududu ya hayo maziwa.. Mweeee
Mungu tusaidie!
Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
Huu mtindi wa Tanga ni mzito mmno ukilinganisha na mitindi mingine kama wa Mara,Asaad,Kilimanjaro na tena hii uwa unasikia kabisa kaharufu kama maziwa yaliyo chacha ,ata mitindi nilikunywa vijiji hauko kama wa Tanga....labda nikahisi huu wa Tanga ni mchanganyiko wa mambo...!!!!!!!!!
Nasikia kwenda bafuni, unabebwa mgongoni.Unapewa pia na visahani vidogo viwili; kimoja cha kuwekea sabuni na kingine......!Mwaipopo alienda tanga kununua nazi kwa ajili ya biashara kutoka tanga mbeya, basi alipofika si akala na mtaji wote baada ya kula haya mahanjumati kutoka kwa mmama wa kitanga.....alirudi mbeya na matenga yake matupu mtaji ukiwa umebaki tanga. Chezea tanga wewe ni padogo lakini pakubwa sana tu
kiukweli nimekunywa sana mtindi wa tanga fresh kwa miaka mingi sana and it was the best mtindi ever until I found the real and natural mtindi, si mwingine bali ni wa kilimanjaro mtindi.
Yaani haya maziwa kiukweli yako very natural, less of chemical additives na naupenda saaaana.
Kwa hapa dar bado haupo lakini siku wakiingia soko la dar, 'mitindi' yote ijiandae kutolewa sokoni.
Wanakusanya maziwa kutoka kwa wafugaji mbalimbali, then wanatengeneza huo mtindi.Hadi sasa sijaona jibu la kisayansi...wote mwapiga porojo tu.
Hebu tuelezeni kama kuna ranchi ambayo hufugwa ng'ombe wa maziwa.
Binafsi ninahisi hawa jamaa wanatoa maziwa eneo moja laitwa Mlingano lipo Pongwe, kama sikosei kule kuna ranchi. (Hili sina uhakika bado maana nimeondoka Tanga kitambo kidogo).
Wana jamvini hivi kweli mtindi wa Tanga Fresh ni maziwa ya ngombe au mimi ni mpenzi sana wa mtindi lakini napata shida kidogo kuamini kama huo mtindi ni kweli maziwa ya ngombe .mwenye jibu jamani