TANESCO yatangaza Kiama

Bora muje huku mtaani kwangu tupambane muraa maana mmeniunguzia vifaa vyangu sana katika zima-wacha yenu kira mara ....nami natangaza vita muraa

Na hiyo id yako inaendana kabisa na ulichokiandika 😅😂😃😆
 
huku wazohill juzi usiku lori la tanesco limekuja mtaani wakafungua kitu fulani kina umbo kama mtungi wa gesi tulipowahoji wakadai wanakuja kufunga lingine baadae, ila hadi leo hawajarudi, taarifa zinadai kile kilikua kifaa maalumu kwaajiri ya kuiba umeme ila kutokana na hali ya sasa imebidi kukitoa ili kuepusha dhahama!
 
Mkuu mbona umeandika kama toinyo au kibogoyo , wenda ndio kusema una upungufu
wa meno kinywani mwako, ..?
Siku nyingine jifunze kuandika kama "Senior Expert Member wa JF".
Kwani kwa namna ulivyoandika hapo inaonesha hata mwandiko
wako wa mkono ni mbaya sana "una hati ya bata".

 
Mkuu PDidy, katika utawala huu nimejifunza jambo,
ukicheza dili na serikali ujue imekula kwako. jifikirie mtu aliyepitsha kontena kwa rushwa ya 5m ili asilipe 40m leo hii anatakiwa alipe yote 40m huoni kama amepoteza?
hao jamaa washauri wakalipe zote tanescola tu maana yakija kufumuka watalipa zote na faini juu wakati hapo wamelipishwa nusu
 
Mr. Mramba, Kama ni wafanyakazi wako wanahujumu shirika weye sema usiogope. Hii kata, washa mnavyopenda, inakukumba weye kweli?? Toeni basi kataarifa kidogo. Ni aibu na fedheha kwa Tanesco ltd. Shirika kongwe kuliko shirika jingine lolote lililo hai hapa Tz.
Maji ya bureeeee, nguzo ni miti tunapanda wenyewe halafu mnawaza kuthibiti wadokozi wa wats badala ya hayo makilowati yanayo potelea hewani kwa kushindwa kuyatumia.
Ni aibu, tz kukatikiwa umeme kila saa. Hakuna siku itapita salama. Tumeshindwa hata kubajeti vyakula kwa sababu vingi tunamwaga kwa kuharibika.
Badala ya woote kuhama ofisi kukimbilia mitaani kusaka mita mbovu, gawaneni kazi wengine mjifungie mahali mkifanya kautafiti muondoe hii kadhia ya washa, zima, washa, kata. Mmetumalizia vyombo majumbani.
Nasikia ati unaitwa Injinia Mramba, uliupataje huo uinjinia kama hata kaubunifu huna?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…