TANESCO yadaiwa na makampuni ya Umeme Mwanza

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797

picture-4.jpg

Na Saed Kubenea - Imechapwa January 2012

SERIKALI ya Rais Jakaya Kikwete yaweza kufikishwa mahakamani kwa mara nyingine. Mara hii kwa kushindwa kutoa malipo yanayohusiana na uzalishaji nishati ya umeme.

Makampuni mawili ya nje tayari yamekalia kooni Shirika la Umeme la taifa (TANESCO) yakidai kulipwa ingawa hayajaanza kuzalisha umeme wa megawati 60 kwenye eneo la Nyakato, jijini Mwanza.

Makampuni yanayodai TANESCO ni M/S Semco Maritime AS na Rolls-Royce Marine AS ya nchini Uingereza. Ubia wa makampuni hayo unadai kiasi cha Euro 15, karibu Sh. 40 bilioni.


Katika barua yao kwa Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO ya 9 Desemba 2011, makampuni hayo yanasema, "Sisi ni makampuni yenye uvumilivu na yanayoaminika na tunatambua kuwa kweli inaweza kuchukua muda bila malipo kufanywa.


"Lakini kwa mtiririko huu wa uvunjaji ahadi za kauli na maandishi, naona hakuna suluhisho lolote lile isipokuwa kurejea Dar es Salaam siku ya Jumatatu, 12 Desemba 2011, kuanzisha hatua muhimu za kulinda maslahi ya kampuni yangu," anaandika Kim Christensen, mkurugenzi wa maendeleo ya biashara.


Christensen alitishia, "Nitakuwa ofisini kwako siku ya Jumanne, 13 Desemba 2011, saa 13:45 mchana."


Makampuni hayo yaliingia mkataba na TANESCO wa kuzalisha megawati 60 za umeme unaotokana na mafuta mazito. Mkataba huo, Na. PA/001/09/HQ/W/033 ulisainiwa tarehe 4 Oktoba 2010.


Barua ya makampuni hayo inakumbusha baadhi ya vifungu vya mkataba vinavyosomeka. Kwa mfano inasema Kipengele cha 3.1 cha mkataba kinaitaka TANESCO kulipa malipo ya awali (advance payment).


Aidha, barua inakumbusha kuwa mkataba unasema ni mwajiri (TANESCO) ambaye atatoa Barua ya Dhamana (Letter of Credit – LC) kwa makampuni hayo ili yaweze kuitumia kupata mikopo.


Kifungu kingine ambacho kinakumbushwa ni kuhusu utaratibu wa malipo, kwamba makampuni yana haki ya kupokea malipo kwa kila sehemu inayokamilika kadri kazi inavyoendelea.


Kupatikana kwa taarifa hizi kumekuja ndani ya kipindi cha miezi michache baada ya mahakama ya kimatifa ya usulihishi wa migogoro ya kibiashara (ICC) kuipa tozo kampuni ya Dowans ya kulipwa kiasi cha 94 bilioni.


Katika uchunguzi wake, gazeti hili limefanikiwa kuinasa barua iliyotumwa tarehe 9 Desemba 2011 kutoka kwa mkurugenzi mkuu wa kampuni hiyo, Kim Christen kwenda kwa mkurugenzi mtendaji wa TANESCO, William Mhando.


Semco na Rolls-Royce wanasemwambia mkurugenzi mtendaji wa tanesco kurejea "vipengele katika barua yetu iliyopita ya tarehe 17 na 18 Aprili 2011."


"Tayari mkandarasi ameruhusiwa kuingia kwenye saiti, amemaliza kufanya upimaji na ramani na ameanza ujenzi," anaeleza Christensen katika barua ambamo anaandika kuwa ishughulikiwe na Bw. William Mhando, Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO.


Nakala za barua hiyo zimepelekwa kwa Cervacius Likwelile, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Uchumi, Eliakim Maswi, aliyeapishwa juzi kuwa katibu mkuu wizara ya nishati na madini; na Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Juma Reli.


Anasema kampuni hiyo ya kigeni tayari ilianza kutekeleza mkataba wake ikiwamo kufanya kazi za kiinjinia katika eneo hilo na uagizaji wa vifaa kutoka nje ili kukamilisha mradi uliopangwa.


Malipo ambayo makampuni yanadai yalipaswa kufanywa kati ya 4 Octoba 2010 na 12 Mei 2011.


Tayari makampuni yamemwingiza Rais Kikwete katika sakata hili na kumhusisha na "njoo kesho, njoo kesho" ambayo wameita "uvunjaji ahadi wa wiki baada ya wiki, mwezi baada ya mwezi" na ambao wanasema umewachosha.


"Pamoja na ushiriki wa mheshimiwa rais katika kikao cha Jumnatatu, 10 Oktoba 2011, ikulu Dar es Salaam… bado hatujapata malipo yaliyokubaliwa," imeeleza barua ya madai.


Haya yanatokea wakati serikali ikikabiliwa na ukata mkubwa kiasi cha kukata matumizi yake katika maeneo kadhaa kwa asilimia 50.


Aidha, serikali haijapona majeraha ya kuamriwa kulipa kampuni ya Dowans/Richmond kiasi cha Sh. 115 bilioni kutokana na kilichoitwa kuvunja mkataba wake na makampuni hayo wa kuzalisha umeme wa megawati 100 jijini Dar es Salaam.


Vilevile madai haya yanakuja katika kipindi ambako sakata la umeme wa dharura na hali ya kifedha ya TANESCO ni miongoni mwa mambo ambayo yanaisumbua serikali.


"Haya si mambo madogo, hasa katika kipindi hiki ambamo serikali inashindwa hata kushughulikia suala hili la upatikanaji umeme wa uhakika," ameeleza waziri mmoja mwandamizi ndani ya serikali aliyezungumza kwa sharti la kutotajwa gazetini.


Meneja Uhusiano wa TANESCO, Badra Masoud ameliambia MwanaHALISI kuwa wanatambua kuwepo kwa malalamiko ya mkandarasi huyo ambaye alisema anaendelea kufanya kazi jijini Mwanza.


Badra alisema mkandarasi huyo tayari ameshalipwa Euro 8 milioni kwa awamu ya kwanza na mipango ya kumlipa Euro 7 milioni zilizobaki inakamilishwa.


Hata hivyo, alikiri kuwa utaratibu wa kumlipa mkandarasi huyo tangu mwanzo ulipata matatizo kwa sababu mbili kubwa: Kwanza wenyewe walichelewa kuleta barua ya dhamana. Pili, waliweka masharti magumu kuhusu mambo ya mdhamini wao, jambo alilosema lilikuwa kinyume cha ahadi.


"Tunalijua suala hili na hatuna tatizo isipokuwa lazima nao watambue walianza vibaya kwa kuchelewesha barua ya kuelezea mahitaji ya fedha baada ya kuwa tumesaini nao mkataba," alisema.


Badra alikiri kuwa mkandarasi huyo amezunguka kwa wakubwa kadhaa serikalini kulalamika hadi kuamua kukutana na Rais Kikwete. "Lakini mwote humo alielezwa ukweli wala siyo kuhangaishwa kama anavyolalamika," amesema.





 

Similar Discussions

Back
Top Bottom