TANESCO yaanza kutumia makundi ya WhatsApp kuwasiliana na wateja

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
SHIRIKA la Umeme nchini (Tanesco) limeweka mfumo maalumu wa kutumia makundi ya WhatsApp kwa lengo la kutoa na pokea taarifa za nishati ya umeme kwa wateja wao wa kada mbalimbali nchini.

Akizungumza na MTANZANIA Jumapili jana Kaimu Meneja Uhusiano wa Tanesco, Leila Muhaji alisema kuanzishwa huko kwa makundi ya WhatsApp ni agizo kutoka bodi ya shirika hilo mkakati ukiwa ni kuhakikisha wateja wanapata taarifa ya kila kinachoendelea kuhusu nishati ya umeme.

“Tunatambua nguvu ya magrupu ya WhatsApp katika kufanikisha taarifa kwa jamii, hivyo Tanesco tumeona hili na hivyo kupitia Bodi yakatoka maagizo maalumu kwa wilaya zote na mikoa nchini kuhakikisha zinaanzisha magrupu hayo.

“Hivyo mameneja wa Tanesco kwa ngazi ya Wilaya na Mkoa tayari wameanzisha magrupu hayo kwa ajili ya kuwasiliana na wateja”.

Muhaji alisema makundi hayo yatajumuisha wateja na viongozi wa ngazi mbalimbali wa Tanesco lengo ni kuhakikisha changamoto yoyote inayohusu umeme inatolewa kwa wakati.

Alisema tangu kuanzishwa kwa makundi hayo tayari wameanza kuona matokeo chanya kwani hivi sasa wateja wao wanao uhakika wa kupata taarifa ya kila kinachoendelea na wakati huo huo wateja nao wanayo fursa ya kuwasilisha changamoto iwapo zitajitokeza.

Alisea katika kuhakikisha makundi hayo yanaleta tija kwa ngazi ya Wilaya na Mkoa walichokifanya ni kuweka makundi kulingana na aina ya wateja.

Kwa sababu hiyo alisema yapo makundi kwa ajili ya wateja wakubwa ambapo miongoni mwao wamo wawekezaji.

“Kuna makundi ya wateja wa kati na ya wateja wa kawaida kuanzia ngazi ya mtaa hadi mkoa.

“Tuliamua pia kwenye makundi hayo wawepo na viongozi wa ngazi mbalimbali wa Serikali za Mitaa, Wakuu wa Wilaya, wabunge na viongozi wengine wa serikali ambao ni sehemu ya wadau muhimu katika kuhakikisha tunatatua changamoto za umeme.

“Kwa maana hiyo hata Mkurugenzi Mtendaji wa shirika letu katika mtaa anaoishi ameunganishwa kama mteja wa Tanesco kwenye grupu la WhatsApp na wakati huo huo kama kiongozi,” alisema

Leila ambaye yupo kwenye ziara ya wahariri wa vyombo vya habari mkoani Arusha yenye lengo la kuangalia miradi mbalimbali ya umeme inayotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Tano amesisitiza umuhimu wa makundi hayo ambapo wawekezaji wa mkoa huo wamekiri kuwa sasa imekuwa rahisi kwao kupata taarifa.

Wakizungumza na Mtanzania baadhi ya wamiliki wa viwanda waliopo mkoani Arusha , wamesema kwa sasa wanajiona wenye thamani kutokana na namna ambavyo Tanesco imeamua kuwaweka karibu kupitia njia hiyo ya kuwasiliana.

Chanzo: Mtanzania

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Imechelewa sana hatua hii.
 
sawa n hatua nzuri sana lakini mkubuke hatuna access na server ya whatsapp..hv wataalamu wa IT hapa tz wanashidwa kutengeneza forum website ya server yetu na kutengeneza app yake ..tukaacha utegemezi jaman

Na mie hilo nimeliikiria na mengineyo..
 
Hahaha kuna ma group mengine ni ya kina delicious wale wanalipwa tu.
Na wana access vipi hayo makundi au ndio kwa msaada wa TCRA
 
Yapo.sisi wa tabata tuna group kubwa kabisa na kwakweli linasaidia kwa asilimia kubwa kupata taarifa na kusaidiwa kukiwa na matatizo yanayohusu tanesco tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ili kujisajili kwenye hayo magroup utaratibu ni wao wenyewe kusajili members kwa kutumia namba za simu za wateja wao zilizo kwenye database yao au wao wanatoa namba au link na kisha wateja kujiunga?
 
nguvu ya magrupu ya WhatsApp katika kufanikisha taarifa kwa jamii, hivyo Tanesco tumeona hili na hivyo kupitia Bodi yakatoka maagizo maalumu kwa wilaya zote na mikoa nchini kuhakikisha zinaanzisha magrupu hayo

I dare to say this is a foolish move towards cheating Magufuli, kama wameshindwa kufanyia kazi malalamiko yaliyofikishwa ofisini kwa simu (Morogoro mjini in particular) kwa physical visit ya mteja kwenye ofisi husika hata kwa kuwapa grid reference ya eneo yalipo matatizo nk, wakashindwa completely, hiyo ya whatsapp ndiyo wataiweza!!? I have several instances reported to the regional office kwa kila namna tangu 2016 mpaka leo hakuna kitu, naona waziwazi hapa wanamdanganya tu Rais kuwa wao ni wabunifu kumbe ni hopeless.
 
Back
Top Bottom