TANESCO wakishindwa kukusanya madeni,bei ya umeme haitapanda?

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,014
144,372
Kilio cha sasa cha TANESCO kwa wadaiwa sugu wa shirika hilo bila shaka kinatokana na kutopanda kwa bei ya umeme kama TANESO iliyoomba kiasi kwamba hata Zanzibar imetishiwa kukatiwa umeme.

TANESO wametoa wiki mbili kwa wadaiwa sugu kulipa madeni(ni kweli kila mtu anastahili kulipa) ila kukusanya madeni nako si kazi rahisi maana itategemea na hali ya kiuchumi ya wadaiwa wa shirika hilo.

Sasa najiuliza endapo ukusanyaji wa madeni utakuwa mgumu,bei ya umeme haitapanda?

Bei isipopanda,mgao wa umeme utaepukika?

Alafu kwanini wakati wa Mramba serikali haikutoa tishio kama hili la kuikatia umeme Zanzibar?

Serikali ya Muungano huku bara yenyewe haidaiwi na TANESCO?

Naziona dalili za Mramba kuonekana alitendewa vivyo sivyo.

"Narudi koromije,mjini wanataka vyeti"
 
Shirika hili liko hoi bin taabani linajiendesha kwa hasara, kumfukuza Mramba pale zilikuwa ni siasa za kijinga sana
 
Back
Top Bottom