TANESCO wajiandae baada ya uchaguzi magufuli ang'aka

  • Thread starter Field Marshall ES
  • Start date

Field Marshall ES

Field Marshall ES

JF-Expert Member
Joined
Apr 27, 2006
Messages
12,659
Likes
100
Points
0
Field Marshall ES

Field Marshall ES

JF-Expert Member
Joined Apr 27, 2006
12,659 100 0
Magufuli Ang'aka.......Awaambia TANESCO Wajiandae Kuondoka ofisini Baada ya Uchaguzi .Awataka WanaArusha Waache FujoAkizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha, Dk Magufuli alisema kama watendaji wa shirika hilo wanamuhujumu kwa kumzimia umeme, wajiandae kutoka kwenye viti vyao akiingia ofisini kwani bado siku 18 tu za kuingia Ikulu.

Dk Magufuli, ambaye amekuwa akisisitiza kwenye mikutano yake kuwa hatavumilia watendaji wazembe, alisema mawaziri wa Wizara ya Nishati na Madini na watendaji wajiandae kuachia nafasi zao kwani hataweza kuwavumilia.

Alisema tatizo la umeme, ambalo linaonekana kuwa sugu, limekosa majibu ya uhakika.

"Ninajua mawaziri wapo kwenye kampeni, lakini nao wajiandae zimebaki siku 18 tu," alisema Dk Magufuli.

Awali Tanesco ilisema kuwa tatizo la sasa la umeme lingedumu kwa wiki moja kwa kuwa ilikuwa ikishughulikia kuunganisha mitambo ya kufulia umeme na mabomba ya gesi asilia, lakini mapema wiki hii imeeleza kuwa kazi hiyo inaweza kuchukua muda mrefu zaidi kutokana na gesi hiyo kuwa na uchafu uliotokana na uwekaji mabomba, msukumo kuwa mdogo na kusubiri matokeo ya vipimo vilivyopelekwa nje ya nchi.

Hali kadhalika, uwezekano wa kutumia umeme unaofuliwa kwa kutumia maji, haupo kwa sasa kutokana na mabwawa kukauka.

Awali, katibu mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana alisema ni jambo ambalo haliwezekani kwa tatizo la umeme kushindwa kupatiwa ufumbuzi kwa muda mrefu.

"Hatutaki majibu mapesi kwenye maswali magumu," alisema Kinana. "Kama wanabadilisha mitambo sasa kutumia gesi, kwanini hawakujiandaa?"

Kinana alisema viongozi ambao wamekuwa wakitoa majibu kuhusu sakata la umeme ni wale ambao wanaishi nyumba zenye mashine za jenereta, hivyo hawajui adha za wananchi.

"Kuna wananchi kazi zao ni vinyozi, sasa wanapokosa umeme ujue unawaathiri sana," alisema.

Katika mkutano huo, mamia ya wananchi walipaza sauti kulalamikia tatizo la umeme wakisema kuwa ni kero na hivyo kumfanya Kinana, ambaye amekuwa akilaumu watendaji wa Serikali, azungumzie tatizo

================================

Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dk John Magufuli akimnadi mgombea ubunge Jimbo la Monduli, Namelock Sokoine katika mkutano wa kampeni za CCM, mjini Monduli jana.

Monduli/Mwanga. Wagombea urais kwa tiketi za vyama vya Chadema na CCM jana waliungana kuzungumzia tatizo la umeme, walipoahidi kuwashughulikia wahusika endapo mmoja wao ataingia Ikulu wakati walipokuwa wakihutubia kwenye mikutano tofauti ya kampeni jana.

Kwa takriban wiki nne sasa, umeme umekuwa tatizo kubwa sehemu mbalimbali nchini na kuathiri shughuli mbalimbali za kiuchumi na za kijamii, huku Shirika la Umeme (Tanesco) likieleza kuwa tatizo hilo limesababishwa na ufuaji umeme kuanza kutumia gesi asilia na pia ukame uliosababisha mabwawa yaliyo na mitambo ya kufulia umeme kukauka.

Akiwa mjini Mwanga, mgombea urais wa Chadema, Edward Lowassa aliwaambia wananchi kuwa iwapo atachaguliwa kushika nafasi hiyo ya juu kisiasa, Tanesco watafute mahali pa kwenda, wakati mgombea wa CCM, Dk John Magufuli alisema mjini Arusha kuwa iwapo tatizo litaendelea, atamtimua Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene na wakuu wa shirika hilo.

Dk Magufuli na Tanesco

Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha, Dk Magufuli alisema kama watendaji wa shirika hilo wanamuhujumu kwa kumzimia umeme, wajiandae kutoka kwenye viti vyao akiingia ofisini kwani bado siku 18 tu za kuingia Ikulu.

Dk Magufuli, ambaye amekuwa akisisitiza kwenye mikutano yake kuwa hatavumilia watendaji wazembe, alisema mawaziri wa Wizara ya Nishati na Madini na watendaji wajiandae kuachia nafasi zao kwani hataweza kuwavumilia.

Alisema tatizo umeme, ambalo linaonekana kuwa sugu, limekosa majibu ya uhakika.

"Ninajua mawaziri wapo kwenye kampeni, lakini nao wajiandae zimebaki siku 18 tu," alisema Dk Magufuli.

Awali Tanesco ilisema kuwa tatizo la sasa la umeme lingedumu kwa wiki moja kwa kuwa ilikuwa ikishughulikia kuunganisha mitambo ya kufulia umeme na mabomba ya gesi asilia, lakini mapema wiki hii imeeleza kuwa kazi hiyo inaweza kuchukua muda mrefu zaidi kutokana na gesi hiyo kuwa na uchafu uliotokana na uwekaji mabomba, msukumo kuwa mdogo na kusubiri matokeo ya vipimo vilivyopelekwa nje ya nchi.

Hali kadhalika, uwezekano wa kutumia umeme unaofuliwa kwa kutumia maji, haupo kwa sasa kutokana na mabwawa kukauka.

Awali, katibu mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana alisema ni jambo ambalo haliwezekani kwa tatizo la umeme kushindwa kupatiwa ufumbuzi kwa muda mrefu.

"Hatutaki majibu mapesi kwenye maswali magumu," alisema Kinana. "Kama wanabadilisha mitambo sasa kutumia gesi, kwanini hawakujiandaa?"

Kinana alisema viongozi ambao wamekuwa wakitoa majibu kuhusu sakata la umeme ni wale ambao wanaishi nyumba zenye mashine za jenereta, hivyo hawajui adha za wananchi.

"Kuna wananchi kazi zao ni vinyozi, sasa wanapokosa umeme ujue unawaathiri sana," alisema.

Katika mkutano huo, mamia ya wananchi walipaza sauti kulalamikia tatizo la umeme wakisema kuwa ni kero na hivyo kumfanya Kinana, ambaye amekuwa akilaumu watendaji wa Serikali, azungumzie tatizo hilo.

Hata hivyo, Kinana aliwahakikishia wakazi wa Arusha kuwa Serikali ya Awamu ya Tano, ikiwa chini ya Dk Magufuli, itashughulikia matatizo hayo, ikiwamo kuondoa kodi zenye kero, matumizi makubwa ya Serikali kama ununuzi wa magari ya kifahari.

Lowassa na Tanesco

Akiwa Same, mkoani Kilimanjaro, Lowassa aliwashukia Tanesco akiwaonya watendaji wake kuwa akiingia madarakani wajiandae kutafuta kazi nyingine kwa kuwa umeme umekuwa ni kero kwa wananchi kutokana na kukatika mara kwa mara pasipo sababu za msingi.

Akizungumza na wananchi wa Mwanga kwenye mkutano wa kampeni jana, Lowassa alisema uongozi mbovu na Serikali isiyokuwa makini ndiyo vinasababisha kukosekana umeme wa uhakika wakati rasilimali zipo za kutosha.

"Uchumi unasimama kwa kukosekana umeme wa uhakika, uwezo upo lakini viongozi wetu wameshindwa kulitatua," alisema Lowassa, ambaye alikuwa Waziri Mkuu wa Serikali ya Awamu ya Nne kwa mwaka 2006 hadi 2008, kipindi ambacho nchi iliingia kwenye matatizo makubwa ya umeme kutokana na ukame.

"Ninawaambia Tanesco wajipange baadhi ya watendaji watafute kazi nyingine," alisema Lowassa.

Alisema bila kufanyika uamuzi wa haraka kutatua tatizo la umeme nchini mambo mengi yanakwama na uzalishaji viwandani unadorora na gharama za bidhaa kupanda hivyo kumuumiza mwananchi wa kawaida.

Lowassa alijiuzulu uwaziri mkuu mwaka 2008 baada ya Kamati ya Bunge kubaini kampuni ya Richmond Development ya Marekani iliyopewa zabuni ya kufua umeme wa dharura, haikuwa na uwezo unaokidhi mahitaji. Hata hivyo, Lowassa amekuwa akieleza kuwa uamuzi wake ulikuwa ni wa kuiokoa Serikali na kuhusishwa kwake kunatokana na maelekezo ya wakubwa wake, ambao hajawataja.

Mbali na kuzungumzia suala hilo, Lowassa pia alizungumzia suala la elimu, kilimo na afya akiwaeleza wananchi wa Same kuwa atashughulikia sekta hizo kwa umakini ili kuwasaidia wananchi kuondokana na matatizo ya kukosa hizo huduma muhimu kwa muda mrefu.

"Ninataka urais kwa kuwa nimechoshwa na mambo haya. Kila kitu hakipo sawa lazima watu wafanye uamuzi ili mambo yaende na si maneno maneno kila siku," alisema Lowassa.

Katika hatua nyingine, Lowassa ameitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuliangalia kwa makini suala la wanafunzi wa vyuo vikuu kushiriki kupiga kura kutokana na vyuo kufungwa wakati wa Uchaguzi Mkuu.

Alisema wanafunzi wengi walijiandikisha wakati wakiwa vyuoni hivyo ni muhimu NEC ikatafuta utaratibu mzuri ili wanafunzi hao wapige kura pale walipo kwa kuwa walijiandikishia vyuoni na hivi sasa vyuo vimefungwa.

Ahani msiba wa Kisumo

Baada ya mkutano wa Same, Lowassa alikwenda Usangi kuhani msiba wa mwanasiasa mkongwe nchini, Peter Kisumo kwa kuweka shada la maua katika kaburi lake.

Lowassa aliambatana na Waziri Mkuu wa Serikali ya Awamu ya Tatu, Frederick Sumaye na mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia.

Baada ya kuweka mashada ya maua, Lowassa alisema: "Nimetimiza azima yangu, yaliyopita yamepita Kisumo alikuwa ni rafiki yangu."

Lowassa alishindwa kufika Same kumzika kada huyo wa CCM baada ya msafara wake kuzuiwa kilomita chache kabla ya kufika eneo la maziko. Polisi waliruhusu gari la Lowassa na viongozi wachache lipite kuelekea kwenye mazishi, lakini alikataa.

Kwa upande wake kaka wa Kisumo, Daniel Mchangila alielezwa kusikitishwa na kitendo cha Lowassa kuzuiwa kuhudhuria mazishi na kumwomba asahau yaliyopita.

Dk Magufuli Jimbo la Monduli

Akiwa wilayani Monduli, Dk Magufuli aliwataka wananchi wa jimbo hilo na vitongoji vyake kumchagua kwani ana uhakika yeye ndiye rais wa awamu ya tano na hivyo wasipoteze kura kwa mtu ambaye hatashinda.

Akihutubia mikutano ya hadhara katika mji wa Mto wa Mbu na Monduli mjini, jana asubuhi Dk Magufuli alisema ana uhakika yeye ndiye Rais wa awamu ya tano na hata kama kura zingepigwa leo (jana) nchi nzima angeshinda kwa zaidi ya asilimia 85.

"Ndugu zangu Monduli msipoteze kura zenu kwa mtu ambaye hatashinda urais. Mimi ndiye Rais wa awamu ya tano," alitamba Magufuli huku akishangiliwa na wafuasi na wananchama wa chama hicho.

Alisema anaifahamu vizuri Monduli tangu enzi za Waziri Mkuu wa zamani, Hayati Edward Sokoine kwa kuwa alikuwa Kambi ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) ya Makuyuni. Alisema wakati huo, Monduli ilikuwa inakwenda vizuri, lakini sasa inakabiliwa na kero nyingi ikiwepo ya maji, njaa na elimu.

"Ninawahakikishia kuibadilisha Monduli. Jimbo hili lina umuhimu sana kwetu nitashirikiana na mbunge Namelock Sokoine kuhakikisha mji wa Monduli unakuwa na lami," alisema.

Alisema pia atahakikisha mji wa Mto wa Mbu unakuwa na huduma muhimu kama benki na ofisi za Tanesco ili kuwaondolea adha ya wakazi wa mji huo kwenda Wilaya ya Karatu kufuata huduma hizo.

Amnadi Namelock

Katika mikutano hiyo, Dk Magufuli alimuombea kura Namelock ambaye anagombea ubunge wa Monduli, akisema ni mwenye damu ya shujaa wa Taifa ambaye atatimiza ndoto za baba yake katika jimbo hilo.

Dk Magufuli alisema wapo ambao watafika jimboni hapo kumpiga vita Namelock kwa kuwa ni mwanamke, lakini wapuuzwe kwa kuwa kila mtu amezaliwa na mwanamke na pia Namelock ni mgombea mwenye uzoefu wa bungeni.

Magufuli jana alitembelea kaburi la Sokoine na kuweka shada la maua kisha kuzungumza na familia yake.

Namelock atamba yupo Imara

Akizungumza kwenye mikutano hiyo, Namelock alisema yupo imara hana mpango wa kujiondoa kugombea ubunge CCM.

Chanzo: Mwananchi
 
Super human

Super human

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2015
Messages
1,141
Likes
646
Points
280
Super human

Super human

JF-Expert Member
Joined Feb 26, 2015
1,141 646 280
Mgombea urais kulalamika kana kwamba umeme ulianza kukatika kipindi hiki ti while tanesco ina matatizo?? Kumbe hajui tanzania ina shhida ya umeme inayoitaj mipango kuimalz? Say no to magufuli
 
Z

Zamazangu

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2015
Messages
632
Likes
235
Points
60
Z

Zamazangu

JF-Expert Member
Joined May 16, 2015
632 235 60
Mgombea urais kulalamika kana kwamba umeme ulianza kukatika kipindi hiki ti while tanesco ina matatizo?? Kumbe hajui tanzania ina shhida ya umeme inayoitaj mipango kuimalz? Say no to magufuli
Huyu mgombea wa ccm anajifanya hajui shida ya umeme? au hili hajacrem? n shiiida
 
Bajeti ya kunguru

Bajeti ya kunguru

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2014
Messages
678
Likes
308
Points
80
Bajeti ya kunguru

Bajeti ya kunguru

JF-Expert Member
Joined Sep 21, 2014
678 308 80
Mgombea urais kulalamika kana kwamba umeme ulianza kukatika kipindi hiki ti while tanesco ina matatizo?? Kumbe hajui tanzania ina shhida ya umeme inayoitaj mipango kuimalz? Say no to magufuli
na anaye mfanyia hujuma ameshajulikana ni Machali
 
Pascal Ndege

Pascal Ndege

Verified Member
Joined
Nov 24, 2012
Messages
2,397
Likes
542
Points
280
Pascal Ndege

Pascal Ndege

Verified Member
Joined Nov 24, 2012
2,397 542 280
Ufisadi wote Tanesco ulifanywa na wanasiasa sasa Ndugu yangu simbachawene hela mle wenyewe sisi tunapata shida. Alafu aturusiwi kusema. Tutawapa kura watakao tuahaidi umeme hili swala lipo wazi wala halina nguvu kulisema.
 
Rweye

Rweye

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2011
Messages
16,245
Likes
4,024
Points
280
Rweye

Rweye

JF-Expert Member
Joined Mar 16, 2011
16,245 4,024 280
MD mramba achunguzwe
 
Matola

Matola

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2010
Messages
39,257
Likes
20,375
Points
280
Matola

Matola

JF-Expert Member
Joined Oct 18, 2010
39,257 20,375 280
Magufuli Ang'aka.......Awaambia TANESCO Wajiandae Kuondoka ofisini Baada ya Uchaguzi .Awataka WanaArusha Waache Fujo

View attachment 296045

Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha, Dk Magufuli alisema kama watendaji wa shirika hilo wanamuhujumu kwa kumzimia umeme, wajiandae kutoka kwenye viti vyao akiingia ofisini kwani bado siku 18 tu za kuingia Ikulu.

Dk Magufuli, ambaye amekuwa akisisitiza kwenye mikutano yake kuwa hatavumilia watendaji wazembe, alisema mawaziri wa Wizara ya Nishati na Madini na watendaji wajiandae kuachia nafasi zao kwani hataweza kuwavumilia.

Alisema tatizo la umeme, ambalo linaonekana kuwa sugu, limekosa majibu ya uhakika.

"Ninajua mawaziri wapo kwenye kampeni, lakini nao wajiandae zimebaki siku 18 tu," alisema Dk Magufuli.

Awali Tanesco ilisema kuwa tatizo la sasa la umeme lingedumu kwa wiki moja kwa kuwa ilikuwa ikishughulikia kuunganisha mitambo ya kufulia umeme na mabomba ya gesi asilia, lakini mapema wiki hii imeeleza kuwa kazi hiyo inaweza kuchukua muda mrefu zaidi kutokana na gesi hiyo kuwa na uchafu uliotokana na uwekaji mabomba, msukumo kuwa mdogo na kusubiri matokeo ya vipimo vilivyopelekwa nje ya nchi.

Hali kadhalika, uwezekano wa kutumia umeme unaofuliwa kwa kutumia maji, haupo kwa sasa kutokana na mabwawa kukauka.

Awali, katibu mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana alisema ni jambo ambalo haliwezekani kwa tatizo la umeme kushindwa kupatiwa ufumbuzi kwa muda mrefu.

"Hatutaki majibu mapesi kwenye maswali magumu," alisema Kinana. "Kama wanabadilisha mitambo sasa kutumia gesi, kwanini hawakujiandaa?"

Kinana alisema viongozi ambao wamekuwa wakitoa majibu kuhusu sakata la umeme ni wale ambao wanaishi nyumba zenye mashine za jenereta, hivyo hawajui adha za wananchi.

"Kuna wananchi kazi zao ni vinyozi, sasa wanapokosa umeme ujue unawaathiri sana," alisema.

Katika mkutano huo, mamia ya wananchi walipaza sauti kulalamikia tatizo la umeme wakisema kuwa ni kero na hivyo kumfanya Kinana, ambaye amekuwa akilaumu watendaji wa Serikali, azungumzie tatizo
Hii ID imerudi tena? au umewakabidhi vijana wa IT masaki?
 
kamtesh

kamtesh

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2014
Messages
1,286
Likes
182
Points
160
kamtesh

kamtesh

JF-Expert Member
Joined Jul 26, 2014
1,286 182 160
Kwani yeye yupo chama gani. Tanesco ipo ndani ya serekali ya nani? Aache maigizo yake!
 
RUKUKU BOY

RUKUKU BOY

JF-Expert Member
Joined
Sep 8, 2015
Messages
1,292
Likes
1,285
Points
280
RUKUKU BOY

RUKUKU BOY

JF-Expert Member
Joined Sep 8, 2015
1,292 1,285 280
Magufuli Ang'aka.......Awaambia TANESCO Wajiandae Kuondoka ofisini Baada ya Uchaguzi .Awataka WanaArusha Waache Fujo

View attachment 296045

Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha, Dk Magufuli alisema kama watendaji wa shirika hilo wanamuhujumu kwa kumzimia umeme, wajiandae kutoka kwenye viti vyao akiingia ofisini kwani bado siku 18 tu za kuingia Ikulu.

Dk Magufuli, ambaye amekuwa akisisitiza kwenye mikutano yake kuwa hatavumilia watendaji wazembe, alisema mawaziri wa Wizara ya Nishati na Madini na watendaji wajiandae kuachia nafasi zao kwani hataweza kuwavumilia.

Alisema tatizo la umeme, ambalo linaonekana kuwa sugu, limekosa majibu ya uhakika.

"Ninajua mawaziri wapo kwenye kampeni, lakini nao wajiandae zimebaki siku 18 tu," alisema Dk Magufuli.

Awali Tanesco ilisema kuwa tatizo la sasa la umeme lingedumu kwa wiki moja kwa kuwa ilikuwa ikishughulikia kuunganisha mitambo ya kufulia umeme na mabomba ya gesi asilia, lakini mapema wiki hii imeeleza kuwa kazi hiyo inaweza kuchukua muda mrefu zaidi kutokana na gesi hiyo kuwa na uchafu uliotokana na uwekaji mabomba, msukumo kuwa mdogo na kusubiri matokeo ya vipimo vilivyopelekwa nje ya nchi.

Hali kadhalika, uwezekano wa kutumia umeme unaofuliwa kwa kutumia maji, haupo kwa sasa kutokana na mabwawa kukauka.

Awali, katibu mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana alisema ni jambo ambalo haliwezekani kwa tatizo la umeme kushindwa kupatiwa ufumbuzi kwa muda mrefu.

"Hatutaki majibu mapesi kwenye maswali magumu," alisema Kinana. "Kama wanabadilisha mitambo sasa kutumia gesi, kwanini hawakujiandaa?"

Kinana alisema viongozi ambao wamekuwa wakitoa majibu kuhusu sakata la umeme ni wale ambao wanaishi nyumba zenye mashine za jenereta, hivyo hawajui adha za wananchi.

"Kuna wananchi kazi zao ni vinyozi, sasa wanapokosa umeme ujue unawaathiri sana," alisema.

Katika mkutano huo, mamia ya wananchi walipaza sauti kulalamikia tatizo la umeme wakisema kuwa ni kero na hivyo kumfanya Kinana, ambaye amekuwa akilaumu watendaji wa Serikali, azungumzie tatizo

================================

Chanzo: Mwananchi
Jiwe huwezi pata tena watu kama hawa
 
Fullfilledtruth

Fullfilledtruth

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2018
Messages
1,906
Likes
1,282
Points
280
Fullfilledtruth

Fullfilledtruth

JF-Expert Member
Joined Oct 28, 2018
1,906 1,282 280
Hawapati lakini kupita kama vile upepo utokapo pasipo na uwazi ukaelekea na kujiachia penye uwanda.

Au siyo Chifu? haha hahaaaaaa.......!!!!
Jiwe huwezi pata tena watu kama hawa
 
Forum statistics

Threads 1,274,613
Members 490,740
Posts 30,517,956