TANESCO: Umeme ndiyo nishati yenye unafuu wa bei kuliko zote hapa nchini

mukandarasi

JF-Expert Member
Sep 3, 2012
932
275
Leo asubuhi kulikuwa na kipindi katika kituo kimoja cha Tv hapa nchini ,TANESCO wakieleza kuwa Umeme ndiyo nishati yenye unafuu wa bei kuliko zote hapa nchini! Tena wakijaribu kutoa na mifano isiyo na uhalisia,kuwa mwananchi wa kawaida ana uwezo wa kununua kopo moja la mkaa kwa Sh.2000/- mpaka 2500/-kwa siku ambayo kwa mwezi ni Sh.60,000/-.Hili ni kweli.

Lakini huyo jamaa wa shirika la umeme nchini anashindwa japo kuwaangalia na kuelewa maisha ya ndugu zake pale kijijini kwao achilia mbali uswazi,je ni wangapi wana uwezo wa kupata Sh.60,000/- za ziada kuilipa TANESCO?

Naziita za ziada kwasababu mwananchi huyo awe amejikimu yeye na familia yake kisha abaki na hizo Sh.60,000/-akanunue umeme(Hapo zingatia si wote wenye Mita za LUKU).

Mazungumzo hayo yalitokana na mjadala ''kwanini watu wanaiba umeme ?''
Nilichogundua toka kwa ma ofisa hao wa TANESCO ni kwamba Shirika hilo halijafanya utafiti wa kulijibu swali hilo!!

Hakuna binadamu wa leo asiyetaka kutumia umeme katika maisha yake ya kila siku,kinachogomba ni kipato cha watanzania tulio wengi kuwa ni chakuungaunga.
 
Kwa nini wasitumie mkaa wakati on average Arusha (au kaskazini) wanazima umeme mara 3-4 kwa siku?? Tena kwenye nyakati za kuandaa chakula. Nakumbuka wafanyakazi wa Tanesco zamani walikuwa na special tariff (niseme zero tariff). Kama Tzs.60,000 kwao ni ghali, wajaribu tariff za sisi mitaani.
 
Tatizo kubwa la Tanzania sasa hivi ni kwamba kila mtu ni mwanasiasa, urahisi wa huo umeme analinganisha ni kitu gani?? Mkaa hauwashi taa, zaidi ya kupika. Hivyo zaidi ya mkaa ana mzigo wa kulipia taa pia mkaa hauendeshi fridge wala radio, tv... Kuna watu wakisha jua wako live wanaonekana kwenye luninga akili huwatoka na kuvaa ujinga. Huwezi niambia mimi na akili zangu umeme wa Tanzania ni rahisi nikubaliane na ww kamwe,,,,,, umeme umekuwa biashara badala ya huduma bado serikali haioni hilo ni story za ajabu tuu.
 
Back
Top Bottom