KIBURUDISHO
JF-Expert Member
- Mar 28, 2011
- 1,002
- 274
Wakuu heshima iwe kwenu.
Waswahili husema ugumu wa maisha kipimo cha akili sidhani kama usemi huu ni sahihi sana.Mwenzenu baada ya purukushani na baba mwenye nyumba hatimae kwa sasa "nimehamia mtaa wa saba toka kule nilikokuwa nikiishi zamani........"!!
Niende moja kwa moja kwenye mada baada ya mwenzenu kufanikiwa kuhamia mtaa wa saba changamoto niliyokutana nayo ni hatari ya vyombo vyangu vitumiavyo umeme kugeuka mazalia ya viumbe hai kama vile wadudu na si binadamu.Nimekwenda kubisha hodi kwenye shirika letu hili la umma yaani Tanesco kwa ajili ya kuvinusuru vifaa vyangu vitumiavyo umeme visigeuke vichaka mtumishi wa tanesco kaja kanipimia zinahitajika nguzo nne ili niweze kupewa umeme mfukoni kiasi nilichonacho hakitoshi maana nguzo tatu tu zinagharimu sh 1,300,000/= ya nne sikujua itakuwa sh ngapi nikawacheki majirani zangu wawili kila mmoja ni chenga wanapiga wakiwa na taget kwamba nihangaike mimi ili wao waje wavute kiulaini nimefikiria sana nimeshindwa nifanye mbinu ipi ili niweze kuupata umeme.
Nilipofikia hapo nikapata wazo fulani japokuwa wazo hilo halitakuwa msaada kwa muda muafaka ila litakuwa limewapa mwanga fulani wahusika wa shirika letu.Kuna makampuni fulani ya solar kama vile Mobisol au Mpower nk yanayomkopesha mteja kwanini shirika letu lisiige huo mfumo kwasababu tulio wengi hatuna pesa ya kulipia kuunganishiwa umeme kwa mara moja.Ningewashauri Tanesco waweze kuwa na mkopo wa kuwakopesha wateja huduma ya kuunganishiwa umeme kwa mkopo wa muda fulani kadri watakavyokuwa wanaona inafaa endapo kama mteja atachelewa kulipia deni lake system yenyewe inamkatia mteja umeme hadi hapo atakapolipia deni ndio huduma inarudi.Natumai kwa utaratibu huu shirika litapata wateja wengi mbinu ambayo makampuni ya soral yamekuwa yakijizolea wateja wengi.