Tanesco Tabata, vipi kuhusu mita mpya za Luku?

Tanesco Tabata, vipi kuhusu mita mpya za Luku?

Shoctopus

JF-Expert Member
Joined
Dec 29, 2015
Posts
3,435
Reaction score
1,995
Mita yangu ya LUKU iliharibika miezi kadha kipindi cha mvua. Siku hiyo mvua ilinyesha kubwa sana ndipo matatizo yakaanza. Kwanza ilikuwa inapunja units nikinunua 20 mita inasoma 12 au 9 tu. Niliporipoti nikaambiwa nisubiri kidogo nitabadilishiwa nipate mita mpya. Baadae siku moja nikaambiwa mafundi wamesha pewa mita yako wapo nijiani wanakuja leo ila wameanzia maeneo ya mbali.

Wakimaliza huko watakuja kwako. Hawakuja mchana wote hadi usiku, nikaenda siku ya pili nikaulizwa: Unapata umeme? Nikasema ndiyo lakini sasa mita haionyeshi units ingawa umeme unapita! Wakasema: Kama hivyo tutakuja kwako baada ya kuhudumia wenye mita mbovu na hawapati umeme. Nikashangaa kutokuambiwa ile mita waliyosema mafundi walipewa kuniletea iliishia wapi!

Nikaambiwa tu niendelee kununua LUKU kama kawaida ili siku wakija ku-replace mita kama wakikuta sinunui LUKU watanikadiria deni ili nilipe kabla ya kuwekewa mita mpya!

Kuanzia hapo sielewi kama wamenisahau au ndio staili ya kutafuta sababu za "kunitoa upepo au vipi! Kwani baada ya muda nimeambiwa hawana mita mpya sasa kwa watu kama mimi. Kwasababu issue yangu sio dharura, Kwahiyo nisubiri hadi waletewe mita mpya toka Makao Makuuu? Nikauliza zitaletwa lini? Nikajibiwa: Hatujuwi, lakini kuna wenzio wanangoja toka mwaka jana!

Jamani! Kama TANESCO hawana mita za ku-replace zinazoharibika hawaoni huu ni mwanzo wa kuwapa mwanya wateja au wafanyakazi wao wa kutafuta kitu kidogo wakati watakaponiletea mita mpya? Naomba TANESCO watuepushe na uzembe huu jamani.
 
Back
Top Bottom