TANESCO: Taarifa ya katizo la umeme mkoa wa Kinondoni Kaskazini Juni 23, 2016

hakuna shida

Member
Dec 16, 2015
25
5
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawataarifu wateja wake wa Mkoa wa Kinondoni Kaskazini kuwa, kutakuwa na katizo la umeme siku ya ALHAMISI 23 JUNI, 2016 kuanzia Saa 03:00 Asubuhi hadi Saa 10:00 Jioni. SABABU: Kuzimwa kituo cha kupooza umeme cha MASAKI kwa ajili ya kuhamisha njia ya umeme msongo wa 11KV kupisha ujenzi wa njia mpya ya umeme msongo wa 33KV ili kuboresha hali ya upatikanaji wa umeme.
MAENEO YATAKAYOATHIRIKA

Eneo lote la Masaki na Msasani, pamoja na baadhi ya maeneo ya Oysterbay.
Toa taarifa TANESCO kupitia Dawati la dharura Mkoa wa Kinondoni Kaskazini: 0784 768584, 0716 768584 au Kituo cha miito ya simu namba 2194400 or 0768 985 100.

Uongozi unaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.

Imetolewa na: OFISI YA UHUSIANO, TANESCO – MAKAO MAKUU.
 
Back
Top Bottom