Tanesco Sengerema imulikwe

Tanesco Sengerema imulikwe

Status
Not open for further replies.

Bhikalamba

JF-Expert Member
Joined
Dec 6, 2015
Posts
2,344
Reaction score
3,375
Kwako waziri wa nishati mh. Kalemani, pamoja na mkurugenzi wa Tanesco.

Mh. Waziri kwanza nianze kwa kukupongeza kwa hatua kubwa ya usambazaji umeme ilipigwa na wizara yako.

Sasa naomba nijikite kwenye mada, pamoja na pongezi hizo naomba uelewe kuwa kuna watendaji wa chini wanakungusha nami nataka nikutonye tu ili ufanyie kazi malalamiko haya, ili yasijekukuta yaliyo wakuta Kichere na Kakunda.

Mh. Waziri imekuwa nimekuwa nikisikia malalamiko sehemu mbalimbali kuwa ukienda Tanesco ili upate kuunganishiwa umeme ni hadi utoe kitu kidogo ndo utashughulikiwa maombi yako, sikuamini sana juu ya hilo , hususani katika awamu hii ya sasa.

Mh. Waziri, sasa ndo nathibitisha juu ya hilo. Tangu mwezi wa February nilijaza fomu ya kuomba kuunganishiwa umeme pale Tanesco Sengerema, huwezi amini nilisubiri kwa muda wa miezi miwili pasipo jamaa kuja kufanya survey kwenye nyumba yetu pamoja na kufuatwa Mara kwa Mara (ukizingatia nyumba yangu iko umbali wa kama kilomita mbili na nusu tu kutoka ofisi za Tanesco) lakini majibu yao siku zote ilikuwa tutakuja, tunaratiba ya kuzungukia mtaa huo tutawajulisha.

Baadae dada mmoja akanitonya kuwa nimuone jamaa fulani privately, ambaye alinichaji elfu20 na baada tu ya kumpatia kesho yake wakaja kufanya survey huyo jamaa na mwenzie. Siku mbili baadae nikapata ujumbe wa kwenda kulipia Tanesco Sh.337,500/= kwani kunahitajika nguzo moja kufikia kwenye nyumba yangu. Bila ajizi nilifika Tanesco maramoja nikapewa fomu na baadae kwenda kulipia benki. Lakini tangu nilipie sasa imepita tena miezi miwili sasa.
Kiufupi naona ni mkakati waliojiwekea hapo ofisini wa kuwacheleweshea huduma wateja hadi utoe kitu kidogo nami siko tena tayari kulambwa hela nyingine.

Nimeamua kuandika thread hii kukutanabahisha mh, ufanye ufuatiliaji si hapa kwetu Sengerema tu bali pia sehemu zingine ambako watendaji Tanesco wamekuwa ni kero. Huenda kuna mamia ya watu waliopata dhahama kama Mimi. Ila tu hawajajitokeza.

Nasema hivyo kwa sababu utakumbuka mwaka juzi mh. Rais aliwahi kuzungumza suala la mwekezaji wa kiwanda cha tiles kukwama kuanza uzalishaji sababu ya Tanesco kuchelewa kumuunganishia umeme hadi Rais alipoingilia kati. Sasa nakuomba nawe uingilie kati.

======

UPDATES:

=======

Mrejesho kuhusu lalamiko la mteja wetu hapo juu

Timu yetu imefanya uchunguzi kwa kina ili kujiridhisha na lalamiko lako ambapo ili kukamilisha ushahidi huu mteja alipaswa kutoa ushirikiano lakini mpaka tunaporudi hapa mteja hakutoa ushirikiano wowote hata wa namba ya simu au jina aliloombea umeme. Aidha tumewapigia simu wateja wa mwezi wa pili mpaka tano mwaka huu ili kujiridhisha kama kuna mteja aliyapeta tatizo lililolamikiwa bila mafanikio.

Tunawaomba sana wateja wetu mtupatie ushirikiano kwa taarifa kamili za tuhuma mnazotoa kwa kuwa zipo taratibu kwa mujibu wa sheria na kanuni za kufata kama mfanyakazi amezikiuka.

Shirika linaendelea kukuomba mteja wetu kama kuna mfanyakazi au mtu yeyote amejihusisha na vitendo ulivyolalamikia toa taarifa hapa hata kwa siri au tumia vyombo vya dola badala ya kutoa tuhuma nzito bila ushirikiano

Tunapenda kuwasikia wateja wakitoa taarifa kamili za matatizo, malalamiko au maombi ili tuyafanyie kazi .

Shirika linaendelea na uchunguzi wake ili kubaini ukweli wa tuhuma hizi

TANESCO HUDUMA KWA WATEJA

MAKAO MAKUU
 
Mara nyingi ukiona unacheleweshewa huduma hasa huduma za uma ujue unatengenezewa mazingira ya kutoa rushwa. Hakuna maeneo ambayo watanzania tunapoteza muda mwingi kama kwenye ofisi za uma. Naona leo tanesco wanaandamwa kweli kweli ila lisemwalo lipo kama halipo tulisubirie.
 
Pia Tanesco Kigamboni kila siku utawasikia wanasema Nguzo hakuna hakika ni Usumbufu kwa wateja.
 
Hakika hawa jamaa wanapaswa kufuatiliwa kwa ukaribu vinginevyo itakuwa ni mwendo wa kusubiri mikutano ya Rais na kutokea kama yale ya jana kwa TRA.
 
Tatizo la Tanesco si la Sengerema tu ni la nchi nzima hata sisi tunaoishi huku Chattle anapotokea huyo waziri pamoja na mkuu wa nchi tatizo Ni hilo hilo na pengine huku kunaweza kuwa na matatizo makubwa kuliko huko maana siku hizi wanakata umeme wapendavyo Kila saa Kila wakati kwa kweli Tanesco ni kelo
 
Kwako waziri wa nishati mh. Kalemani, pamoja na mkurugenzi wa Tanesco.

Mh. Waziri kwanza nianze kwa kukupongeza kwa hatua kubwa ya usambazaji umeme ilipigwa na wizara yako.

Sasa naomba nijikite kwenye mada, pamoja na pongezi hizo naomba uelewe kuwa kuna watendaji wa chini wanakungusha nami nataka nikutonye tu ili ufanyie kazi malalamiko haya, ili yasijekukuta yaliyo wakuta Kichere na Kakunda.

Mh. Waziri imekuwa nimekuwa nikisikia malalamiko sehemu mbalimbali kuwa ukienda Tanesco ili upate kuunganishiwa umeme ni hadi utoe kitu kidogo ndo utashughulikiwa maombi yako, sikuamini sana juu ya hilo , hususani katika awamu hii ya sasa.

Mh. Waziri, sasa ndo nathibitisha juu ya hilo. Tangu mwezi wa February nilijaza fomu ya kuomba kuunganishiwa umeme pale Tanesco Sengerema, huwezi amini nilisubiri kwa muda wa miezi miwili pasipo jamaa kuja kufanya survey kwenye nyumba yetu pamoja na kufuatwa Mara kwa Mara (ukizingatia nyumba yangu iko umbali wa kama kilomita mbili na nusu tu kutoka ofisi za Tanesco) lakini majibu yao siku zote ilikuwa tutakuja, tunaratiba ya kuzungukia mtaa huo tutawajulisha.

Baadae dada mmoja akanitonya kuwa nimuone jamaa fulani privately, ambaye alinichaji elfu20 na baada tu ya kumpatia kesho yake wakaja kufanya survey huyo jamaa na mwenzie. Siku mbili baadae nikapata ujumbe wa kwenda kulipia Tanesco Sh.337,500/= kwani kunahitajika nguzo moja kufikia kwenye nyumba yangu. Bila ajizi nilifika Tanesco maramoja nikapewa fomu na baadae kwenda kulipia benki. Lakini tangu nilipie sasa imepita tena miezi miwili sasa.
Kiufupi naona ni mkakati waliojiwekea hapo ofisini wa kuwacheleweshea huduma wateja hadi utoe kitu kidogo nami siko tena tayari kulambwa hela nyingine.

Nimeamua kuandika thread hii kukutanabahisha mh, ufanye ufuatiliaji si hapa kwetu Sengerema tu bali pia sehemu zingine ambako watendaji Tanesco wamekuwa ni kero. Huenda kuna mamia ya watu waliopata dhahama kama Mimi. Ila tu hawajajitokeza.

Nasema hivyo kwa sababu utakumbuka mwaka juzi mh. Rais aliwahi kuzungumza suala la mwekezaji wa kiwanda cha tiles kukwama kuanza uzalishaji sababu ya Tanesco kuchelewa kumuunganishia umeme hadi Rais alipoingilia kati. Sasa nakuomba nawe uingilie kati.
Ndugu mpendwa mteja wetu tumesikitika sana kwa hayo uliyoeleza.Shirika lako la Umeme Nchini (TANESCO) linaomba ushirikiano wa wewe kutupatia taarifa zitakazosaidia wewe kupata huduma na muhusika kuchukuliwa hatua.Je umelipia kwa jina gani? Namba ya simu? Na je aliyekuomba rushwa ni nani?

Unaweza kutupatia taarifa zako hadharani au inbox ili kuwasiliana na wewe.Tupo tayari kukutembelea na kukusikiliza kwa nia ya kutoa huduma bora zaidi
 
Kwako waziri wa nishati mh. Kalemani, pamoja na mkurugenzi wa Tanesco.

Mh. Waziri kwanza nianze kwa kukupongeza kwa hatua kubwa ya usambazaji umeme ilipigwa na wizara yako.

Sasa naomba nijikite kwenye mada, pamoja na pongezi hizo naomba uelewe kuwa kuna watendaji wa chini wanakungusha nami nataka nikutonye tu ili ufanyie kazi malalamiko haya, ili yasijekukuta yaliyo wakuta Kichere na Kakunda.

Mh. Waziri imekuwa nimekuwa nikisikia malalamiko sehemu mbalimbali kuwa ukienda Tanesco ili upate kuunganishiwa umeme ni hadi utoe kitu kidogo ndo utashughulikiwa maombi yako, sikuamini sana juu ya hilo , hususani katika awamu hii ya sasa.

Mh. Waziri, sasa ndo nathibitisha juu ya hilo. Tangu mwezi wa February nilijaza fomu ya kuomba kuunganishiwa umeme pale Tanesco Sengerema, huwezi amini nilisubiri kwa muda wa miezi miwili pasipo jamaa kuja kufanya survey kwenye nyumba yetu pamoja na kufuatwa Mara kwa Mara (ukizingatia nyumba yangu iko umbali wa kama kilomita mbili na nusu tu kutoka ofisi za Tanesco) lakini majibu yao siku zote ilikuwa tutakuja, tunaratiba ya kuzungukia mtaa huo tutawajulisha.

Baadae dada mmoja akanitonya kuwa nimuone jamaa fulani privately, ambaye alinichaji elfu20 na baada tu ya kumpatia kesho yake wakaja kufanya survey huyo jamaa na mwenzie. Siku mbili baadae nikapata ujumbe wa kwenda kulipia Tanesco Sh.337,500/= kwani kunahitajika nguzo moja kufikia kwenye nyumba yangu. Bila ajizi nilifika Tanesco maramoja nikapewa fomu na baadae kwenda kulipia benki. Lakini tangu nilipie sasa imepita tena miezi miwili sasa.
Kiufupi naona ni mkakati waliojiwekea hapo ofisini wa kuwacheleweshea huduma wateja hadi utoe kitu kidogo nami siko tena tayari kulambwa hela nyingine.

Nimeamua kuandika thread hii kukutanabahisha mh, ufanye ufuatiliaji si hapa kwetu Sengerema tu bali pia sehemu zingine ambako watendaji Tanesco wamekuwa ni kero. Huenda kuna mamia ya watu waliopata dhahama kama Mimi. Ila tu hawajajitokeza.

Nasema hivyo kwa sababu utakumbuka mwaka juzi mh. Rais aliwahi kuzungumza suala la mwekezaji wa kiwanda cha tiles kukwama kuanza uzalishaji sababu ya Tanesco kuchelewa kumuunganishia umeme hadi Rais alipoingilia kati. Sasa nakuomba nawe uingilie kati.
Mrejesho kuhusu lalamiko la mteja wetu hapo juu

Timu yetu imefanya uchunguzi kwa kina ili kujiridhisha na lalamiko lako ambapo ili kukamilisha ushahidi huu mteja alipaswa kutoa ushirikiano lakini mpaka tunaporudi hapa mteja hakutoa ushirikiano wowote hata wa namba ya simu au jina aliloombea umeme. Aidha tumewapigia simu wateja wa mwezi wa pili mpaka tano mwaka huu ili kujiridhisha kama kuna mteja aliyapeta tatizo lililolamikiwa bila mafanikio.

Tunawaomba sana wateja wetu mtupatie ushirikiano kwa taarifa kamili za tuhuma mnazotoa kwa kuwa zipo taratibu kwa mujibu wa sheria na kanuni za kufata kama mfanyakazi amezikiuka.

Shirika linaendelea kukuomba mteja wetu kama kuna mfanyakazi au mtu yeyote amejihusisha na vitendo ulivyolalamikia toa taarifa hapa hata kwa siri au tumia vyombo vya dola badala ya kutoa tuhuma nzito bila ushirikiano

Tunapenda kuwasikia wateja wakitoa taarifa kamili za matatizo, malalamiko au maombi ili tuyafanyie kazi .

Shirika linaendelea na uchunguzi wake ili kubaini ukweli wa tuhuma hizi

TANESCO HUDUMA KWA WATEJA

MAKAO MAKUU
 
MREJESHO:

Nashukuru kwa Tanesco makao makuu kushughulikia malalamiko yangu, niseme tu kwa kifupi mambo yanakwenda vizuri sasa.
 
Mi nafikiri hili tatizo lipo karibia wilaya zote za mkoa wa mwanza. Nimewahi kupitia thread moja humu ya TANESCO wanaeleza kwamba fomu ya maombi ya kuunganishiwa umeme inatolewa bure lakini kiuhalisia unapoenda kuichukua unatozwa pesa wakati mm naunganishiwa mwaka 2012 nilitozwa 10,000/= kwa miaka ya hivi karibuni dau limepanda mpaka kufikia 21,000/= na wakati mwingine nahisi kuna watu wanapigwa zaidi maana kiwango halisi hakieleweki
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom