KERO Tanesco ni Wafalme wa huduma Mbovu Tanzania

KERO Tanesco ni Wafalme wa huduma Mbovu Tanzania

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

kiraza

JF-Expert Member
Joined
Jun 6, 2016
Posts
385
Reaction score
541
Customer Care ya Tanesco ni Geresha! Mwanzo ilikuwa mtu unapiga simu kwenda kwenye tawi la mtaa uliopo kisha mafundi wanakuja kurekebisha tatizo, Walipoona wanasumbuliwa sana ndipo wakaamua kuweka namba moja (Dodoma makao makuu) ambayo kimsingi namba hiyo ni geresha ya kuonekana nao wanasikiliza kero na kupokea matatizo kutoka kwa wateja.

Ni kampuni isiyopenda kuwajibika na inayochukia Ukweli! Kwa sababu ya kukosolewa kwa huduma zao Mbovu kwenye mtandao wa X (Zamani Twitter) Tanesco walipata hasira na kuamua kuingia mitini kwenye mtandao huo, ikiwa ni pamoja na kuwachukulia hatua kali waliokuwa wanalalamika! Hali ya umeme ni mbaya! Na namba yao ambayo ni geresha haipatikani! Umeme unakatika masaa 24! Hata pa kwenda kutoa taarifa hakuna, Dah!

Sisi wananchi tunatoka asubuhi kwenda kazini, Tanesco nao wanatoka Asubuhi kwenda kazini kukata umeme na kuanza kuutengeneza! Hawafikirii kuwa mchana ni muda ambao watu wanautumia kwa kutafuta kipato! Hivyo muda wa kukata umeme kwa marekebisho ni vyema ikawa ni usiku walao kuanzia saa 00:00 hadi 6:00.

Hakuna jambo Tanesco wanapenda kama kukata umeme saa moja asubuhi ma kurudisha saa kumi na mbili jioni! (Huu ni moja ya utaratibu kichaa kwelikweli)

Kwao ni kheri Mtanzania alale njaa ila usiku apigwe feni hadi asubuhi!

Kuna kukatika umeme kwa Dharula kutokana na hitilafu na hilo halizuiliki ila bado nina mashaka sana na Ustaarabu na Taaluma ya kupanga muda wa marekebisho na maboresho ya miundombinu! Ukweli ni kuwa hawajali kuwa umeme wanaousimamia kuna mamilioni ya watu wanautumia hivyo unatakiwa kukatwa kwa ustaarabu, Adabu.
 
Back
Top Bottom