TANESCO ni kiboko!

Bondpost

JF-Expert Member
Oct 16, 2011
6,594
9,338
Ndugu zangu TANESCO walisema LUKU itapandisha mapato ili waweze kutoa huduma bora, watanzania tukakubali wafanye hivyo lakini matokeo yake ni yaleyale.

Wakaja na maombi ya kupandisha bei kwa viwango mbalimbali, matatizo ndio yameongezeka.

Sasa umeme ndio umekuwa wimbo miongoni mwa watanzania, kukatika kusiko na ukomo, umeme bei juu, ukinunua umeme wa elfu kumi unapata units 36 tu hapo wakikata ile service charge yao ambayo service hatuioni ndio umeumia.

Hivi tunakoelekea wapi? Sasa hivi maeneo kadhaa ya huku mbezi juu hakuna umeme, na toka asubuhi walikata, samaki, nyama sasa zilizokuwa kwenye fridge imebidi kununua ice blocks kuweka kwa fridge. Nawaza wale wenye biashara za kutegemea umeme!

Hivi kweli hakuna strategy madhubuti za kuweza kudhibiti hali hii? Mbona nahisi kuna uzembe tu na ukiritimba?

Mungu atusaidie, ila TANESCO wanatuumiza wananchi, bei ya umeme wamepandisha na matatizo ni yaleyale, i guess wao hawaishiwi visingizio.

TANESCO hebu kuweni makini kibiashara.
 
Waziri alisema hakuna mgao, huo sio mgao, hukua arusha na moshi kila siku wanakata saa 12 jiioni sijui unarudi saa ngapi, na siku nyingine wanakata siku nzima,
kweli tanesco ni kiboko yao
 
Nadhani huyo waziri sasa akubali tu kuwa ofisi ile ni nzito kwake! Kwani akikubali atapata hasara gani? Kuliko kukaa na kuangalia mambo yanavyoenda kama hivi, vululu vululu!
 
wee acha tu sh 20,000 nilikuwa napata units 84 nimenunua wiki hii nimepata units 60!!!!

Tena unit moja sh 273
 
Hapo ndio nashindwa kuelewa hawa tanesco ni kitu gani kinaendelea pale?
Sasa naona wanapandisha bei kama ya bia, kila mwaka na tusishangae mwezi novemba wakatoa tangazo la kusudio la kupandisha bei tena.
Huwa sielewi, kama unanunua umeme kwa bei fulani ambayo wao wanapata faida, sasa hii kitu inayoitwa service charge what the hell do they mean?
 
wee acha tu sh 20,000 nilikuwa napata units 84 nimenunua wiki hii nimepata units 60!!!!

Tena unit moja sh 273

Kuna haja ya kuangalia upya safu ya wataalam kwenye hii kampuni iliyo kama kichwa cha mwenda wazimu!
 
Back
Top Bottom