Tanesco na umeme wa Mbagala

Tanesco na umeme wa Mbagala

Mkulima wa Kuku

JF-Expert Member
Joined
Jan 13, 2011
Posts
1,270
Reaction score
536
Tangu jana mchana wote haukuwa na umeme hadi muda huu niandikapo uzi huu. Sina taarifa ya kilichotokea ila ni kawaida sana Tanesco kufanya hichi walichokifanya. Aidha kuna maeneo kuna low voltage kiasi kwamba tumepata hasara nyingi ya mali sababu ya inconsistency ya umeme wao. Tumelalamika juu ya suala la low voltage hawajibu....Tunamuomba Mh. Magufuli aingilie kati kwani tumelipia ili tupate umeme mkamilifu si unaozidi au kupungua. Umeme kwa wengi wetu ni maisha, ni uchumi, ni kila kitu. Tunataka haki yetu ya kupata 220-240 V na si vinginevyo. Pengine kama haiwezekani tuamini kuwa kuna madaraja ya wanaostahili kupewa umeme toshelevu na wasistahili
 
Nchi nzima hakuna umeme. Magufuli anasema Tanesco wanahujumu mabwawa ili watu wauze magenerata, na mafuta. May be.
 
Hata arusha toka asubuhi hakuna Umeme umerudi kabla ya dakika 15 na ukakatika na kurudi Mara 3 na sasa umekatika kabisa
 
Tangu jana mchana wote haukuwa na umeme hadi muda huu niandikapo uzi huu. Sina taarifa ya kilichotokea ila ni kawaida sana Tanesco kufanya hichi walichokifanya. Aidha kuna maeneo kuna low voltage kiasi kwamba tumepata hasara nyingi ya mali sababu ya inconsistency ya umeme wao. Tumelalamika juu ya suala la low voltage hawajibu....Tunamuomba Mh. Magufuli aingilie kati kwani tumelipia ili tupate umeme mkamilifu si unaozidi au kupungua. Umeme kwa wengi wetu ni maisha, ni uchumi, ni kila kitu. Tunataka haki yetu ya kupata 220-240 V na si vinginevyo. Pengine kama haiwezekani tuamini kuwa kuna madaraja ya wanaostahili kupewa umeme toshelevu na wasistahili

"Umeme wa mbagala" ndo upoje? U sound unaishi mitaa ya Tandale Kwa Bi-nyau ambapo ata baiskeli haipenyi.
 
Ukweli ni kuwa tumekuwa na tatizo hili miaka mingi na Tanesco hao hao wanashughulikia matatizo ya maeneo mengine wanashughulikia bila wasiwasi hii ndiyo inayoleta hisia kuwa kuna madaraja ya watu hapa nchi ni. Wanaostahili huduma na wasiostahili
 
Mtoa post uwe unafatilia taarifa kuhusu Tanesco maana hilo walilitolea taarifa kwaiyo usitake kuupotosha uma ili Tanesco ionekane haifai. Nawakati mwingine wananchi ndo wa kwanza kuihijumu miundo mbinu ya Tanesco ikiwemo wizi wa Umeme kwaiyo basi likitokea tatizo wao ndo wa kwanza kulalamika
 
Umeongea ukweli huku Kijichi Mgeni nani nyumba nyingi ikifika saa 2 usiku basi umeme unashuka toka240v- 220v mpaka 90-100v, na hakuna dalili yoyote ku solve hili jambo kuna kipindi nilisikia sababu ni transformer kuzidiwa mzigo sasa cjui issue itatatuliwa lini
 
Kwani Tanesco wanafaa?kifupi hawafai!,ktk mashirika ya umma ninayoyachukia la kwanza ni Tanesco haiwezekani nilipie nguzo,waya,service line kisha bado nalipia service charge,eura,rea,kodi ya umeme ninaotumia nyumbani kila mwezi wakati nalipa kodi zote za serikali ,umeme bei kubwa halafu umeme wenyewe siupati kiuhakika shirika limejaa rushwa,waswahili na wababaishaji,mfano wiki iliyopita nilienda Tanesco kuripoti pale mbagala charambe kuhusu tatizo la mita yangu haipitishi umeme wakachukua namba yangu ya mita na Simu pale chumba no moja na mbili yaani wanatega kutafuta deal za pesa tu huwezi amini mpaka Leo hawajapiga wala hawajaja matokeo yake nipo gizani natamani hizi mita zingekuw zinauzwa kariakoo ningeshanunua kariakoo,kwanini hili shirika lisiruhusu biashara huria ya kusambaza umeme?
 
Ikifikia biashara huria ya umeme watanyooka hawa iwapi leo Kampuni ya postal na simu?
 
Back
Top Bottom