Tiba
JF-Expert Member
- Jul 15, 2008
- 4,607
- 3,191
Wadau,
TANESCO wanatumia hela nyingi kutangaza kwenye vyombo vya habari kwamba ukilipia huduma ya kuunganishiwa umeme, basi utaipata ndani ya wiki mbili. Huu ni uongo uliokomaa kwani hakuna kitu kama hicho. Inawezekana vituo vingine huduma inatolewa ndani ndani ya wiki mbili lakini mimi nimeipata hiyo huduma baada ya miezi miwili. Na hii imewezekana baada ya kutoa kitu kidogo vile vile otherwise ingechukua hata zaidi ya miezi miwili.
Kwa viongozi wa TANESCO wanaoingia humu JF inabidi wakimulike kituo cha Mbezi kwani pale kuna mtu mmoja anaitwa Shayo, yeye ni Mungu mtu kwani bila kutanguliza chochote kwake, utapiga teke la kufuatilia hiyo huduma mpaka kesho. Hata ukimuona meneja au Engineer mkuu pale bado watakuelekeza ukamuone Shayo. Na bila kumuona kiutu uzima hakika hiyo huduma utaisikia radioni.
Swali ni je kwanini TANESCO wanadanganya umma kwa matangazo wakati wakijua hiyo huduma haitolewi ndani ya wiki mbili?
Tujadili.