Tanesco Na Luku

Ndallo

JF-Expert Member
Oct 1, 2010
7,619
4,292
Wakuu kuna tatizo limejitokeza Tanesco sasa hivi kwasisi wateja tunaotumia huduma ya kulipia kupitia hizi Metter za LuKU, ni kwamba sasa hivi huku mkoani Arusha tatizo limeshaanza kua sugu, unanunua umeme Tanesco halafu unapokuja kujaza zile number kwenye Metter ya LUKU hazikubali, nimejaribu kuingiza zile tarakimu zaidi ya mara tano lakini wapi nimerudi Tanesco na kuambiwa na mfanyakazi wa shirika hili kua hata yeye ni muda wa siku tano hana umeme na tatizo ni hilohilo na akaniambia hajui tatizo hili litaisha lini na kwasasa wanafanya tadhimini ya wateja wangapi wameshaanza kuonja joto hili ili walifanyie kazi! Je kwa wenzangu mlioko mikoani je tatizo hili nanyi limeshaanza kuwapata??? Nawasilisha.
 
Back
Top Bottom