TANESCO, mtuambie ukweli. Haiwezekani umeme kupanda kila siku! Kuna mkataba mbovu sehemu, si bure

Pascal Ndege

Verified Member
Nov 24, 2012
2,393
2,000
Nimejiuliza sana lakini sipati jibu! Tanzania tunavyo vyanzo rahisi kabisa vya umeme lakini kila siku Tanesco inadai kuongeza bei ya umeme! Meter tunanunua wenyewe, nguzo tunanunua wenyewe wanapata ruzuku serikalini. Mtueleze gharama za exploration ni kiasi gani na gharama za usafirishaji ni kiasi gani. Hii nchi yetu ilivyo masikini tutabeba madudu ya mikataba mapak lini?
Gharama hizi hapa za kuzalisha umeme kwa Gasi .
Bei ya Gas ya kimataifa leo hii ni MMbt=3.6$ bila gharama za uzalishaji na usafirishaji.
Kwa hela za madafu au hela za Tanzania ni MMbtu=Tsh 8,000/=

Hiii MMbtu=1,000,000btu
Kwahiyo
1,000,000btu=8,000/= kumbuka hapa exploration charges and transportation Charge is excluded.
Ukigawa unapata
1btu=0.008tsh
Ujazo wa gasi wa kuzalisha umeme kwa unit moja inategemea na mtambo ila mtamo imara kabisa unazalisha wastani
10,408 Btu= inatoa (kilowatt )1kWh
Ukichukua rate yake ni 1btu=0.008tsh
Ambayo ni sawa na
Ths 83.264 = kilowatt moja ya umeme.(unit moja)

Unit moja ya umeme sisi kwa bei ya mtaani ni Tanzania shilingi 330. Hivi kibongobongo biashara amabyo unapata faida zaidi ya mara tatu ni ipi? Na bado serikali inamweka mahera yetu kibao kila siku huko tanesco. Hivi mnashindwa kujiendesha kweli? Hapana Mtakuwa mmerogwa na Mganga aliyewaroga kafa.


HAPA CHINI NI REFERENCE

1kg of NG=43cubic

Mcf — equals the volume of 1,000 cubic feet (cf) of natural gas. MMBtu — equals 1,000,000 British thermal units (Btu).Pound 1=0.453592kg


One Btu is the heat required to raise the temperature of one pound of water by one degree Fahrenheit.

The kilograms amount 68.15 kg - kilo converts into 1 cu ft - ft3, one cubic foot. It is the EQUAL concrete volume value of 1 cubic foot but in the kilograms mass unit alternative.
 

Majighu2015

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
2,855
2,000
Duu hizo hesabu ataelewa engineer wa umeme..Hapo nimetoka kapa mkuu,hembu dadavua kwa lugha nyepesi na sisi HKL tuelewe vizuri.Wengine tukiona KW,Inch vichwa vinawaka moto.
 

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
39,482
2,000
This planet is not our place.We belong to somewhere far beyond this planet and the entire universe-tuko kwenye hii dunia kimakosa tu maana hatufanani na wenzetu.
 

kahupwe

JF-Expert Member
Sep 9, 2016
290
250
Balaa hili alianza JK,akiwa waziri wa nishati na madini,tangu hapo mzimu wa Tanesco unatutafuna watanzania.Tanesco imekuwa seemu ya ulaji kuanzia ujenzi wa bomba Gesi hadi kuzalisha umeme.Kwanza mzimu wa IPTL uondoke tutaona Tanesco watapata ahueni.Lakini kwa vile imekuwa ni shamba la bibi mtaji wa watu basi.Tusuke au tunyowe.
 

maonomakuu

JF-Expert Member
Jul 24, 2015
2,522
2,000
Pascal ikifika 2020 utasikia hao hao wanatosha.We need real change maana hata Magufuli alikuwa anashangaa wakati wa kampeni ila leo karudi nyuma.
 

Ngushi

JF-Expert Member
Jul 8, 2016
9,085
2,000
Basi gesi yetu tuliyoahidiwa itazalisha umeme haina faida!
Wanasema bei haitapanda kwa watumiaji wa kawaida majumbani ila ukifuata mfululizo unampandishia mwenyekiwanda unategemea bidhaa bei itakua ile ile!
Wakuumia ni yule yule masikini!!!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom