Tanesco Msiwakate Wapangaji Kodi Ya Jengo...

Tanesco Msiwakate Wapangaji Kodi Ya Jengo...

100 others

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2017
Posts
10,188
Reaction score
36,395
Tanesco kitendo mnachofanya cha kukata kodi za majengo kupitia LUKU si kitendo cha uungwana, kuna watu wamepangwa na wanamlipa mwenye nyumba kodi ya pango, kwa nini hawa hawa wapangwaji tena walipe kodi ya jengo.

Unakuta nyumba ina madeni ya kodi kwa miaka, leo hii eti mpangwaji aje awe analipa, kwa maana hio analipa mara mbili, kodi ya jengo na kodi ya pango...
Tanesco piteni kwenye nyumba za wateja wenu Tanzania nzima, mfahamu wamiliki wa nyumba pia mtatue hili tatizo kwa kushirikisha wapangaji na wapangwaji, mtatue hili tatizo, mnawaumiza watu...

Na hii mmefanya makusudi, mlijua wazi kwa hili suala mtawaumiza wapangwaji lakini kwa sababu wa Tanzania mmetuzoea sisi ni nyumbu ni sawa... tukamuoeni tu...
 
Tatizo liko wapi mdau,we siku ya kulipa kodi kama ni miezi sita unakata elfu sita.Mbona inaeleweka hio.
 
Nilimsikia Rais akisema anataka kodi ya haki siyo dhuruma
Lakini hii kodi ya jengo inayokusanywa kupitia Luku kuna Dhuruma kubwa sana inayofanyika watu wanaokatwa hii kodi hawahusiku Serikali imetoa maelekezo ya kuwabana wamiliki. Mmiliki akienda kuomba kodi ya jengo akatwe yeye kuna issue nyingine itajitokeza withholding Tax, asilimia 10% Pango inabidi ipelekwe TRA. Je hizo Luku unazoomba ukatwe wewe unasema ni wapangaji wako withholding Tax zinapelekwa TRA.
Utajikuta umekwepa kulipa elf 1 umeenda kulipa Laki. Wapangaji haya maumivu ya Kulipa kwenye LUKU kodi yatabaki kuwa yako, ukigoma kodi inaongezwa Au unapigwa notice ya kuama.
 
WEWE mleta mada vipi wewe? Kwani Risiti ya Tanesco ya umeme au mita inasoma jina la nani?

Tanesco wanamjua mwenye nyumba ambaye mita inasomeka jina lake

Hiyo bill inasomeka jina lako mpangaji? Hadi uombe Tanesco wasikate?

Hayo mambo malizana na mwenye nyumba wako sio Tanesco wala TRA
 
Sasa wale ambao Wana meter binafsi Kwa Kila chumba itakuwaje?
Mbona kitaumana na mwenye nyumba
 
Nchi hii bwana binafsi hii kod naona nihalali kabisa kama kweli 12000 kwamwaka tatizo mm nasema tozo nimzigo mkubwa
 
Back
Top Bottom