Habari, Ndugu Mteja.
Kwanza, tunaomba radhi kwa kuchelewa kujibu ujumbe wako kupitia Jamii Forums. Tulipata changamoto ya muda kwenye akaunti yetu, lakini kwa sasa huduma imerejea katika hali ya kawaida.
Pole sana kwa changamoto uliyoipata. Tafadhali fahamu kuwa tunapolazimika kusitisha huduma ya umeme kwa ajili ya matengenezo yaliyopangwa au kutokana na hitilafu za dharura, huwa tunatoa taarifa kupitia njia mbalimbali rasmi, ikiwemo ujumbe mfupi wa simu (SMS) na makundi yetu ya WhatsApp. Taarifa hizi huwasaidia wateja wetu kufahamu kinachoendelea katika maeneo yao na muda unaotarajiwa wa kurejea kwa huduma, kwa kuwa baadhi ya matengenezo huchukua muda mfupi na mengine muda mrefu zaidi.
Iwapo hukupokea taarifa hizo, au uliona hazikukidhi matarajio yako, tunaomba radhi kwa usumbufu uliotokea.
Je, tayari umejiunga na mojawapo ya makundi yetu ya WhatsApp? Kupitia makundi hayo tunatoa taarifa muhimu kuhusu huduma zetu, pamoja na kupokea maoni na changamoto za wateja. Ikiwa bado hujajiunga, tafadhali tujulishe ili tukuunganishe.
Asante kwa uvumilivu na ushirikiano wako. ^GK