TANESCO mnatuibia!

TANESCO mnatuibia!

Ila kusema kweli hii nchi imeoza sana.Halafu bado kuna mambumbumbu humu JF wanatetea upuuzi wa serikali ya Chama cha Mamburula kisa tu wanapewa buku saba.
 
Umeme unakwenda sana mm natumia kwa siku unit 8 na nyumba yakawaida tu taa na tv hata feni situmii nipo karibu na beach sasa sijui nini tatizo

Wezi sana hawa! Halafu sasahivi wameanza na mfumo wa kufunga mita juu ya nguzo ya umeme hata kwa watumiaji wa umeme wa mkondo mmoja (single phase)
 
Sio kosa lao mkuu, wanapaswa kulipa sh. mil 200 daily watumie umeme au wasitumie, na mkataba wa IPTL umeongezwa muda.. sasa hizo hela watazipata wapi??? kwa hiyo ndo tunasaidiana kulipa deni.. tuvumilie tu labda maumivu haya kuna siku yatatupa akili ya kujua kura ni kitu gani..

Hivi capacity charges si ilikuwa ni ya miaka 20 au nakosea? Maana yangu ni kwamba sio ya kudumu hata ikinunuliwa na mtu mwingine, sana sana huyo mwingine anapata investment relief? Au ndio kizungumkuti chenyewe?
 
Umeme ni moja ya huduma muhimu katika maisha ya kila siku. Kwa Tanzania huduma hii inatolewa na kusimamiwa na TANESCO. Tunashukuru kwa huduma zinazotolewa na shirika hili. LAKINI kwa upande wa gharama ya matumizi ya nishati hii ndo kilio kwa Watanzania tulio wengi! Gharama ya Umeme ni KUBWA MNO, MNATUUMIZA!

Tunaomba muweke wazi tarrifs (makato) zenu! Mnadai mmetenganisha tarrifs za mtumiaji mdogo na mtumiaji mkubwa ambapo: Mtumiaji mdogo mmesema ni yule anayetumia umeme chini ya unit 75 kwa mwezi na anapaswa kulipia Tsh 100 kwa unit; Na mtumiaji mkubwa mmesema ni yule anayetumia umeme zaidi ya unit 75 kwa mwezi na anapaswa kulipia Tsh 350 kwa unit.

Nasema mnatuibia kwasababu; mbona mnatutoza gharama ya mtumiaji mkubwa ilihali baadhi yetu ni watumiaji wadogo? Kwa mfano MIMI mwenyewe toka nimeingiza umeme matumiz yangu kwa mwezi hayazidi unit 70 kwa mwezi na mnatoza gharama ya mtumiaji mkubwa! Na kibaya zaidi hamtozi Tsh350 kwa unit badala yake mnatoza 375 na point kadhaa! Acheni kutuibia bwana!
Nawasilisha wadau

Kama unatumia UMEME chini ya Unit 70 kwa mwezi na umetumia zaidi ya miezi 3 andika barua kwa Tanesco na upeleke kwenye office zao za mkoa uliopo watakubadilishia Tariff.
 
Ni kweli tanesco ni wezi hapo walitutega walipobadilisha tarrifs zao walibadilisha pasipo kufanya utafiti ili kujua mita gani itozwe viwango vya mtumiaji mdogo,wa kati,au mkubwa hivyo kama wewe unatumia chini ya unit 75 kwa mwezi inabidi uende ofisi za tanesco za mkoa au wilaya uendea na mita namba na uwaeleze kuwa unatumia units chini ya 75 kwa mwezi kisha watakupa fomu ujajeze na watahakikisha kwenye system zao kama kweli unatumia units hizo ni kisha wanakubadilishia,sema tatizo je ni wangapi wanajua hilo na kulifuatilia?je huo muda wakufuatilia nani anakulipa?

Yes, wangeweka option ya mteja kuchagua tarrif anayoitaka toka mwanzo. Na mita zao wangetofautisha yaan ziwepo za mtumiaji mdogo na mtumiaji mkubwa. Za mtumiaji mdogo zingesetiwa kuwa ziwe zna limitation ya kutojaza unit zaid ya 75.
 
Hivi capacity charges si ilikuwa ni ya miaka 20 au nakosea? Maana yangu ni kwamba sio ya kudumu hata ikinunuliwa na mtu mwingine, sana sana huyo mwingine anapata investment relief? Au ndio kizungumkuti chenyewe?

Nafikiri ipo hivo. Na hilo halina ubishi; Watanzania wote ambao ni wateja wa TANESCO km mimi na wewe tunalipia hiyo capacity charge kila mwezi kupitia SERVICE CHARGE tunayotozwa. Wewe fikiria kila mwezi unalipia Tsh 6734; ushajiuliza kwanin unalipia pesa hizo wakati unalipia energy charge ambayo ni Tsh 375 kwa unit? Hawa jamaa ni MAFISADI wa kupindukia!
 
Let's kokotoa matumizi kwa siku:
Kifaa Power(kw) Muda(hrs) unit
Fridge 0.3 10* 3
Taa 5 0.2 5 1
TV. 0.15. 5 0.75
Pasi. 2. 0.2. 0.4
Jumla ya units kwa siku. 5.1

*Fridge kwa wastani lina nguruma chini ya dakika 30 kwa saa 1(on off operation) Hivo kwa masaa 24 litakuwa on kama masaa 10.
 
Wapo kibiashara zaidi kuliko kua ki huduma zaidi...umeme si anasa ni sawa na huduma ya maji! wizi ndio msingi wa nchi yetu
 
Let's kokotoa matumizi kwa siku:
Kifaa Power(kw) Muda(hrs) unit
Fridge 0.3 10* 3
Taa 5 0.2 5 1
TV. 0.15. 5 0.75
Pasi. 2. 0.2. 0.4
Jumla ya units kwa siku. 5.1

*Fridge kwa wastani lina nguruma chini ya dakika 30 kwa saa 1(on off operation) Hivo kwa masaa 24 litakuwa on kama masaa 10.

Ukiwa na fridge kubwa ndani ya nyumba fahamu kuwa matumizi yako kwa mwezi yatazidi units 75. Ila mtu km mimi ambaye cna fridge ndan ya nyumba nilishafanya calculation nikaona matumizi yangu kwa siku hayazidi units 2.3
 
Ukiwa na fridge kubwa ndani ya nyumba fahamu kuwa matumizi yako kwa mwezi yatazidi units 75. Ila mtu km mimi ambaye cna fridge ndan ya nyumba nilishafanya calculation nikaona matumizi yangu kwa siku hayazidi units 2.3

Bila fridge hesabu ni unit 1.79 kwa siku . Bulb tano ni za watt 40 kila moja jumla watt 200. Bila shaka matumizi ya unit 8 kwa siku bila fridge yanatia mashaka. Solution? Household survey ya kulinganisha bill na matumizi halisi.
 
Mi nilipogundua wananiibia sana na mi nimeamua kuwaibia mwaka sijui 8+ awajapata hela yangu siwezi kuwanufaisha CCM (Si munajua kuwa taasisi zote za serikali na majeshi yote umeme tunawalipia sisi na bado wenyewe hawakatiwi na hawana mgao)
 
Naaam hatuna budi kuifutilia mbali CCM kwanza Kama tunataka ustawi wa wananchi.... CCM ni adui wa haki na ustawi was jamii tuwakatae
 
Back
Top Bottom