TANESCO mnatuibia!

TANESCO mnatuibia!

Mnyalu Junior

JF-Expert Member
Joined
Oct 25, 2012
Posts
573
Reaction score
200
Umeme ni moja ya huduma muhimu katika maisha ya kila siku. Kwa Tanzania huduma hii inatolewa na kusimamiwa na TANESCO. Tunashukuru kwa huduma zinazotolewa na shirika hili. LAKINI kwa upande wa gharama ya matumizi ya nishati hii ndo kilio kwa Watanzania tulio wengi! Gharama ya Umeme ni KUBWA MNO, MNATUUMIZA!

Tunaomba muweke wazi tarrifs (makato) zenu! Mnadai mmetenganisha tarrifs za mtumiaji mdogo na mtumiaji mkubwa ambapo: Mtumiaji mdogo mmesema ni yule anayetumia umeme chini ya unit 75 kwa mwezi na anapaswa kulipia Tsh 100 kwa unit; Na mtumiaji mkubwa mmesema ni yule anayetumia umeme zaidi ya unit 75 kwa mwezi na anapaswa kulipia Tsh 350 kwa unit.

Nasema mnatuibia kwasababu; mbona mnatutoza gharama ya mtumiaji mkubwa ilihali baadhi yetu ni watumiaji wadogo? Kwa mfano MIMI mwenyewe toka nimeingiza umeme matumiz yangu kwa mwezi hayazidi unit 70 kwa mwezi na mnatoza gharama ya mtumiaji mkubwa! Na kibaya zaidi hamtozi Tsh350 kwa unit badala yake mnatoza 375 na point kadhaa! Acheni kutuibia bwana!
Nawasilisha wadau
 
patamu hapa ngoja nikunje 4 na kurefresh browser kila saa nione updates..
 
Huwezi tenganisha utendaji wa mashirika ya umma na chama tawala. Utendaji mbovu wa Tanesco ni udhaifu wa chama Tawala. Usilalamikie Tanesco halafu kesho unapigia kura CCM, ni sawa na kujipiga mgumi ya jicho kwa mkono wako mwneyewe.

Chukua hatua, sema hapana kwa uonevu wa Tanesco kwa kusema hapana kwa CCM!
 
Umeme unakwenda sana mm natumia kwa siku unit 8 na nyumba yakawaida tu taa na tv hata feni situmii nipo karibu na beach sasa sijui nini tatizo
 
Corrupt government including his agencies so dont expect mercy from them.
 
huduma ya tanesco kwa ujumla ni kero, kwani unakuta transformer inaungua halafu wanakujibu ni hali halisi ya nchi yako. Au vp kanunue generator, mfano ni Mkoa wa kilimanjaro Wilaya ya hai transformer imeungua karibia wiki sasa watu wanakaa gizani. Hivi nchi hii lini itatokea kampuni shindani na tanesco?
 
Umeme ni moja ya huduma muhimu katika maisha ya kila siku. Kwa Tanzania huduma hii inatolewa na kusimamiwa na TANESCO. Tunashukuru kwa huduma zinazotolewa na shirika hili. LAKINI kwa upande wa gharama ya matumizi ya nishati hii ndo kilio kwa Watanzania tulio wengi! Gharama ya Umeme ni KUBWA MNO, MNATUUMIZA!

Tunaomba muweke wazi tarrifs (makato) zenu! Mnadai mmetenganisha tarrifs za mtumiaji mdogo na mtumiaji mkubwa ambapo: Mtumiaji mdogo mmesema ni yule anayetumia umeme chini ya unit 75 kwa mwezi na anapaswa kulipia Tsh 100 kwa unit; Na mtumiaji mkubwa mmesema ni yule anayetumia umeme zaidi ya unit 75 kwa mwezi na anapaswa kulipia Tsh 350 kwa unit.

Nasema mnatuibia kwasababu; mbona mnatutoza gharama ya mtumiaji mkubwa ilihali baadhi yetu ni watumiaji wadogo? Kwa mfano MIMI mwenyewe toka nimeingiza umeme matumiz yangu kwa mwezi hayazidi unit 70 kwa mwezi na mnatoza gharama ya mtumiaji mkubwa! Na kibaya zaidi hamtozi Tsh350 kwa unit badala yake mnatoza 375 na point kadhaa! Acheni kutuibia bwana!
Nawasilisha wadau

Ni kweli tanesco ni wezi hapo walitutega walipobadilisha tarrifs zao walibadilisha pasipo kufanya utafiti ili kujua mita gani itozwe viwango vya mtumiaji mdogo,wa kati,au mkubwa hivyo kama wewe unatumia chini ya unit 75 kwa mwezi inabidi uende ofisi za tanesco za mkoa au wilaya uendea na mita namba na uwaeleze kuwa unatumia units chini ya 75 kwa mwezi kisha watakupa fomu ujajeze na watahakikisha kwenye system zao kama kweli unatumia units hizo ni kisha wanakubadilishia,sema tatizo je ni wangapi wanajua hilo na kulifuatilia?je huo muda wakufuatilia nani anakulipa?
 
Sio kosa lao mkuu, wanapaswa kulipa sh. mil 200 daily watumie umeme au wasitumie, na mkataba wa IPTL umeongezwa muda.. sasa hizo hela watazipata wapi??? kwa hiyo ndo tunasaidiana kulipa deni.. tuvumilie tu labda maumivu haya kuna siku yatatupa akili ya kujua kura ni kitu gani..
 
Tanesco ni mradi wa nani? kwa miaka yote niliosikiliza budget ya nchi hii sijawahi sikia tanesco imeingiza sh ngapi hazina, kuna taarifa kuwa ni mradi wa chama tawala, ni kweli?
 
Jamani waacheni

Unafikiri kina rugemalila na wenzie wa escrow watakula wapi???
 
Tatizo hapa ni service charge nadhani niTshs 7000/= au zaidi. Jameni hata kabla ya unit 1.
Tatzo la hawa TANESCO ni kwamba wafanyakazi wao wanapewa Unit 50 kila mwezi bure, ila wasingekuwa wanapewa hizi lazima wangepiga kelele.
 
Umeme ni moja ya huduma muhimu katika maisha ya kila siku. Kwa Tanzania huduma hii inatolewa na kusimamiwa na TANESCO. Tunashukuru kwa huduma zinazotolewa na shirika hili. LAKINI kwa upande wa gharama ya matumizi ya nishati hii ndo kilio kwa Watanzania tulio wengi! Gharama ya Umeme ni KUBWA MNO, MNATUUMIZA!

Tunaomba muweke wazi tarrifs (makato) zenu! Mnadai mmetenganisha tarrifs za mtumiaji mdogo na mtumiaji mkubwa ambapo: Mtumiaji mdogo mmesema ni yule anayetumia umeme chini ya unit 75 kwa mwezi na anapaswa kulipia Tsh 100 kwa unit; Na mtumiaji mkubwa mmesema ni yule anayetumia umeme zaidi ya unit 75 kwa mwezi na anapaswa kulipia Tsh 350 kwa unit.

Nasema mnatuibia kwasababu; mbona mnatutoza gharama ya mtumiaji mkubwa ilihali baadhi yetu ni watumiaji wadogo? Kwa mfano MIMI mwenyewe toka nimeingiza umeme matumiz yangu kwa mwezi hayazidi unit 70 kwa mwezi na mnatoza gharama ya mtumiaji mkubwa! Na kibaya zaidi hamtozi Tsh350 kwa unit badala yake mnatoza 375 na point kadhaa! Acheni kutuibia bwana!
Nawasilisha wadau

Halafu bado 6750 kwa mwezi kama service charge.Mkuu moja ya maazimio yangu ya mwaka huu ni kuondokana nahuu uwizi wa Tanesco kwani hadi sasa sioni faida yake nataka nijiwekeza kwenye umeme jua,wacha nitumie hela nyingi lakini niondokana na huu ujinga,tunawatajirisha tu akina Rugemalira/Edo/Rostam/Singasinga/Marwa.
 
Tatizo sio TANESCO tatizo ni hawa wezi wanaolala Magogoni mchana kweupe, wameleta makapuni ya kutapeli kuiba pesa za walipa kodi kwa njia ya Tanesco, Voda etc. mnafikiri EL na JK wanapata wapi pesa wanazohonga mahawara na kuvinjari hovyo kama wamepagawa au wanavyonunua nyumba nje ya nchi.
 
mtu anachekacheka kama mwehu unategemea atamdhibiti nani,tanesco wanapandisha tu januari ya mwaka huu wameogopa sababu escrow bado ya moto!
 
Back
Top Bottom