TANESCO mnakata umeme Mbezi mara 4 kila siku

TANESCO mnakata umeme Mbezi mara 4 kila siku

maroon7

JF-Expert Member
Joined
Nov 3, 2010
Posts
11,341
Reaction score
15,829
Nyie TANESCO haya mambo ndiyo maana mnatumbuliwa haiwezekani kwa mwezi mzima kila siku mnakata umeme mara nne na hata zaidi na tena hamna taarifa yoyote iliyotolewa kuashiria tatizo maeneo ya Mbezi makabe.

Najua mnapita humu na hata Mawaziri husika wanapita humu. Kuweni waungwana kama kuna tatizo mrekebishe msiwe kama TANESCO ya Shinyanga wanakata nyaya wanaweka juu ya bati then kijana wa watu ananaswa anapoanika nguo na kupoteza maisha.

Uzembe wenu ni mwingi na bado mnafanya kazi kwa mazoea sana licha ya kuwa mnatumbuliwa.
 
Nyie Tanesco haya mambo ndio maana mnatumbuliwa haiwezekani kwa mwezi mzima kila siku mnakata umeme mara nne na hata zaidi na tena hamna taarifa yoyote iliyotolewa kuashiria tatizo maeneo ya Mbezi makabe.

Najua mnapita humu na hata mawaziri husika wanapita humu. Kuweni waungwana kama kuna tatizo mrekebishe msiwe kama Tanesco ya Shinyanga wanakata nyaya wanaweka juu ya bati then kijana wa watu ananaswa anapoanika nguo na kupoteza maisha.

Uzembe wenu ni mwingi na bado mnafanya kazi kwa mazoea sana licha ya kuwa mnatumbuliwa.
Mkuu kuhusu Tanesco kukata umeme bila taarifa na kila siku kwao ndiyo furaha. Kila siku waziri wao Kalemano anawatumbua pale Ubungo lakini hawakomi. Mimi nahisi kuna hujuma wanaifanya baadhi ya wafanyakazi wa Tanesco ili kumhujumu Kalemani. Haiwezekani kila siku wanakata. Siyo Mbezi tu, kuna eneo linaitwa Kimara Mavurunza, acha kabisa. Kila siku wao ni 'ka-ta'. Watu wakazi wa eneo hili wanailaani serikali kumbe ni baadhi ya watendaji tu!!!!! Naamini siku moja JPM atakapotembelea Kimara katika ziara yake ya mkoa Wa Dar es Salaam, atasema: umeme unakatika kila siku hapa Kimara, waziri upo. Mkurugenzi Wa Tanesco upo. Mainjinia mpo. Wasimamizi wa vituo mpo. Hapo lazima kuna. Mtu ataondoka na upepo wa kisulisuli.
 
Back
Top Bottom