TANESCO Maswa waikatia umeme idara ya maji

Equitable

JF-Expert Member
Dec 24, 2021
2,010
5,449
Usumbufu wa kukosa maji wilayani Maswa sasa ni wiki tangu maji yaache kutoka. Kwa mujibu wa mamlaka ya maji mjini Maswa wamedai kuwa kuna deni la umeme la muda mrefu.

Wamedai kuwa mchakato wa kulipa deni hilo unafanywa huko wizarani. Sasa swali

1. Kama Serikali ni moja kwanini wizara zisiwasiliane ili wananchi wasiteseke na adha ya kukosa maji?

2. Je wizara ya fedha inachelewesha makusudi malipo ili wananchi waichukie serikali ya mama yetu?

Naomba rais aangazie wizara zote (Maji na Nishati) kama wapo kumsaidia au kumharibia.
 
Back
Top Bottom