TANESCO Manyara wagumu kubadilika

BETONY

Senior Member
Apr 4, 2012
188
169
Nichukue nafasi hii kumpongeza Waziri wa Nishati kwa kazi kubwa anayoifanya. Pia ni ipongeze wizara nzima na watendaji wake wote kwa ujumla.

Niende moja kea moja kwenye mada. Wakati wa ujuo wa Mh rais wa JMT, Dkt Magufuli kipindi cha kampeni, alikutana na kero ya watu wengi kutofungiwa umeme mjini Babati. Na katika kipindi hicho alitoa mwezi mmoja wa watu kufungiwa umeme. Tunashukuru agizo hilo lilifanyika na wengi kufungiwa umeme.

Tatizo lililojitokeza baada ya watu kufungiwa umeme, ni pale unapoenda Tanesco ili kupata control number kwa ajili ya malipo umeme wako unapokuwa umeisha ili uendelee kutumia mita yako, baadhi ya watumishi wa TANESCO wamekuwa na majibu yasiyo ya kupendeza.

Kwanza wamekuwa wakisema ninyi ndio mlifungiwa umeme wa Magufuli, hivyo wanakusumbua kuwa Surveyor anahitajika kuja kwanza kwenye nyumba kuikagua. Sasa mtu unajiuliza, umeme tayari ulifungiwa na ukatumia kwa kipindi fulani zile unit zilizopo za mwanzo, iweje sasa unapokatika uzungushwe kama haujawahi kuunganishiwa umeme.

Pili basi hao Surveyors ambao ni muhimu, mbona hawafiki kwa wakati katika kuzikagua hizo nyumba na kuhakikisha kuwa watu hawalali na giza?.

Je ,hakuna dalili za rushwa hapo watu wanajitengenezea. Tunaomba meneja wa TANESCO Mkoa ushughulikie kero hii. Kwa pamoja tunaweza.

Imetolewa na muhanga wa kuunganishiwa umeme baada ya tamko la Mh Rais, Mkoani Manyara.
 
Kusema ukweli Tanesco ni shida tupu, Waziri wao ajipange upya, sijui wanasomea chuo gani, ipo haja kuwafanyia utafiti wa kutosha hao walimu wao. majibu ya wafanyakazi wa Babati hayapishani na majibu ya wafanyakazi wa Songea
 
Nichukue nafasi hii kumpongeza Waziri wa Nishati kwa kazi kubwa anayoifanya. Pia ni ipongeze wizara nzima na watendaji wake wote kwa ujumla.

Niende moja kea moja kwenye mada. Wakati wa ujuo wa Mh rais wa JMT, Dkt Magufuli kipindi cha kampeni, alikutana na kero ya watu wengi kutofungiwa umeme mjini Babati. Na katika kipindi hicho alitoa mwezi mmoja wa watu kufungiwa umeme. Tunashukuru agizo hilo lilifanyika na wengi kufungiwa umeme.

Tatizo lililojitokeza baada ya watu kufungiwa umeme, ni pale unapoenda Tanesco ili kupata control number kwa ajili ya malipo umeme wako unapokuwa umeisha ili uendelee kutumia mita yako, baadhi ya watumishi wa TANESCO wamekuwa na majibu yasiyo ya kupendeza.

Kwanza wamekuwa wakisema ninyi ndio mlifungiwa umeme wa Magufuli, hivyo wanakusumbua kuwa Surveyor anahitajika kuja kwanza kwenye nyumba kuikagua. Sasa mtu unajiuliza, umeme tayari ulifungiwa na ukatumia kwa kipindi fulani zile unit zilizopo za mwanzo, iweje sasa unapokatika uzungushwe kama haujawahi kuunganishiwa umeme.

Pili basi hao Surveyors ambao ni muhimu, mbona hawafiki kwa wakati katika kuzikagua hizo nyumba na kuhakikisha kuwa watu hawalali na giza?.

Je ,hakuna dalili za rushwa hapo watu wanajitengenezea. Tunaomba meneja wa TANESCO Mkoa ushughulikie kero hii. Kwa pamoja tunaweza.

Imetolewa na muhanga wa kuunganishiwa umeme baada ya tamko la Mh Rais, Mkoani Manyara.
Ahsante kwa taarifa tumeipokea tunaifanyia kazi mpendwa mteja wetu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom