Tanesco,luku na madeni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tanesco,luku na madeni

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by magneto, Apr 19, 2011.

 1. m

  magneto Member

  #1
  Apr 19, 2011
  Joined: Jul 23, 2008
  Messages: 58
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Jamani naomba kujuzwa kama hii ni sawa au ni utapeli tunafanyiwa na tanesco
  leo nimeenda kununua vocha ya luku kwa ajili ya nyumba ya babu dada muuzaji alivyoingia kwenye hiyo account yetu akasema tumefungiwa na tanesco kununua vocha hadi twende tanesco tukapunguze deni in cash!
  Hapohapo nakumbuka ilikuwa ili tufungiwe luku ilikuwa ni lazima tuingie mkataba na tanesco,ambao ulikuwa unasema mteja atakuwa anakatwa kwa asilimia 50 kila anaponunua umeme,ikiwa na maana ukinunua umeme wa elfu 20 basi utapata unit za thamani ya elfu 10,elfu kumi nyingine inaingia moja kwa moja kwenye deni
  Nachotaka kujua hapa ni kwa nini watufungie kununua luku mpaka twende tanesco kulipa kwa cash kupunguza deni?na kama ni lazima kwenda tanesco kwanini hawakuweka hicho kipengele wakati tunasainishana mkataba?
  Naomba mwenye uelewa na haya majambo ya tanesco anijuvye,ni hayo tu kwa sasa
   
Loading...