TANESCO Kwa nini mnalinga lakini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TANESCO Kwa nini mnalinga lakini?

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Kimox Kimokole, Feb 12, 2012.

 1. Kimox Kimokole

  Kimox Kimokole Verified User

  #1
  Feb 12, 2012
  Joined: Jun 9, 2010
  Messages: 968
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Hivi kwa nini Tanesco mnalinga sana jamani?

  Leo ni siku ya Nne (4) hatuna umeme hapa Kunduchi Mecko, kila mkipigiwa simu mnasema mafundi wako hapo wanashughulikia
  hivi hawa mafundi siku nne zote wako hapo wanashughulikia tatizo moja? Wanalala na kukesha hapo?

  Kwa nini mnatufanya watoto wadogo lakini? Hivi fanyakazi wenu mmoja angekuwa anaishi hapa Kunduchi mngekaa siku nne bila umeme?

  Hili tatizo si mara moja au mbili kutokea hapa, ni zaidi ya mara tano mnasema kuna waya umekatika kila linapotokea tatizo,
  hivi huo waya unakatika sehemu hiyo hiyo kila siku? Na mara zote huo WAYA UKIKATIKA tutakaa siku tatu ama nne bila umeme, hivi ni kweli Mmekuwa na maringo kiasu hicho?

  Hivi mnajua kuwa wengine umeme ndio unaotufanya maisha yaende ingawa mmetukamua? Mnataka tuje kula na kulala hapo Mikocheni ofisini kwenu? Kwa nini mnatufanyia hivi?

  MNAKERA SANA KWA KWELI....
   
 2. Entuntumuki

  Entuntumuki Member

  #2
  Feb 12, 2012
  Joined: Dec 24, 2011
  Messages: 88
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  pole sana mkuu.

  Mtafute mfanyakazi mmoja pale Mikocheni Ofisini anaitwa Singano ata- solve tatizo!
   
 3. M

  Ma Tuma Senior Member

  #3
  Feb 12, 2012
  Joined: Jul 26, 2011
  Messages: 123
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Pia kijitonyama siku ya 3 hatuna umeme.vitu vinaoza.usiku joto la kufa mtu.
   
 4. mpinga shetani

  mpinga shetani JF-Expert Member

  #4
  Feb 12, 2012
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 3,268
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  Tunaringa kwa sababu tuko weeenyeweee bila mpinzani kama ilivyokuaga ttcl zamani
   
 5. u

  ureni JF-Expert Member

  #5
  Feb 12, 2012
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 1,272
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 160
  Watanzania poleni sana haya matatizo ya tanesco ni ya kawaida sana,mie wakati ule wa mgao nilipata shida sana katika umeme nikaamua nijitose nikapiga solar panel za kutosha sasa hivi tatizo la umeme kwangu halipo na tanesco nimeshasahau kama wapo tena,polen sana.
   
Loading...