TANESCO kukata umeme kwa taarifa za habari

TANESCO kukata umeme kwa taarifa za habari

MAGALEMWA

JF-Expert Member
Joined
Jul 8, 2015
Posts
6,413
Reaction score
4,889
Nimefuatilia wiki nne sasa hapa Arusha wakati wa taarifa za habari channel zote ikija habari ya siasa isiyo na mwelekeo wa CCM umeme UNAKATWA. Kama ni makusudi, ni kujivunjia heshima na kujikosesha mapato. Kama si makusudi, mimi na nadhani pamoja na baadhi ya wateja wenu tunastahili kupewa taarifa rasmi.

Ni ajabu kujinasibu na kuongezeka kwa umeme wakati hapa Arusha tunapata umeme si zaidi ya masaa 6 kwa siku.

Itabidi huko mbeleni kuwe na mkataba unaosimamia huduma hii kati ya mteja na TANESCO ili tudaiane usumbufu huu.
 
Tusiwape kura hata moja Serikali ya CCM kwa kutudharau sisi wananchi kwa kutukosesha haki yetu ya kupata umeme.
 
  • Thanks
Reactions: Kig
Hivi bado wanatamani kuwa madarakani! Kwa hili la umeme na mengine ni sababu tosha ya kuwakata ma ccm jaman
 
Yaani kama ni kweli ni wajinga na wanazidi kuwachukiza wananchi hata mimi hainiingii akilini kama ni line repair ni matengenezo gani yanafanywa usiku na alifajiri ukiamka huukuti umeme. Yaani kuna ombwe kubwa la uongozi hapa tanzania ni aibu kubwa sana. Yaani kila kukicha bora ya jana. Nilikuwa nasoma comparison ya kenya na tz kwakweli Tz ni shida sana.
 
Back
Top Bottom