TANESCO Kilimanjaro kuweni wakweli

Aljazeera

Senior Member
Jun 27, 2006
128
43
Mimi mwananchi wa kawaida nimesikitshwa na kitendo cha hawa wakuu kulazimisha kununua umeme wa tariff one angali kwa zaidi ya miaka miwili nimekua natumia tariff 4. Kwa zaidi ya miaka 2 umeme wa elfu tano hutumika zaidi ya mwezi. Cha kishanhaza nimeambiwa kuna uhakiki kwa hiyo lazima kwa miezi mitatu niishi kwa tariff 1 mpaka watanhaze utaratibu mwingine.

Huu naona ni mpango wa kuongeza mapato ili hali wananchi kijijini wanateseka. Kama ni kujua matumizi halali ya mwananchi si waangali manunuzi ya kila mwezi.

Tanesco wamekuwa TRA nyingine au?

Halafu dada wa mapokezi ana kauli mbaya sana. Anaongea na mteja kama vile sistahili kusikilizwa au kuelekezwa. Kila unachouliza ueye majibu yake ni Subiri matangazo.
 
Hapo lazima kuna jambo. Inawezekana matumizi yako yamezidi 75 Units kwa mwezi ila hujapata majibu sahihi. Hata hivyo sioni uhusiano na mateso wananchi vijijini wanayoyapata sema inaonekana kalalamika ndio jadi yako. Huyo dada kama majibu hayafai nikukosa maadili ya kazi inatakiwa aridhishe mteja. Unaweza kwenda kumuona meneja wa mkoa akakusaidia kuliko kuja huku kulalamika.
 
Mimi nilienda Tanesco nikapewa maelezo ya kina na kuonyeshwa jedwali kwenye computer. Matumizi yangu ni zaidi ya units 75 kwa mwezi, nilikua mpole nikakubaluli ili mambo yaishe. Nilijiingiza mwenyewe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom