ShyaRuwa
JF-Expert Member
- May 30, 2015
- 8,252
- 14,793
Wakuu wa Jukwaa heshima kwenu!
Moja kati ya nguzo muhimu za maendeleo ni ushindani.Hata mataifa yaliyoendelea ni yale yaliyohubiri sera za ushinadi.Ushindani unaongeza mbio za maendeleo ya anayekimbiza na anayekimbizwa.
Ukiangalia shirika la uzalishaji na ugavi wa umeme nchini halina mshindani, linaendeshwa ki-monopoly mno. Haishangazi kuona linagubikwa na kashfa lukuki za kifisadi huku likitoa huduma kwa kusuasua kwa wateja wake wachache lililonao.TANESCO ni tofauti sana na makampuni mengi yenye washindani kama ya mitandao ya simu za mikononi, ya usafirishaji, n.k.
Sasa nauliza je kuna uwezekano wa kuwepo makampuni ya kushindana na TANESCO kwenye biashara ya kuzalisha na kusambaza umeme nchini?
Je kama ushindani utatokea, pata kuwepo na uafadhali kwa mtumiaji wa umeme kama vile umeme wa uhakika kwa bei nafuu?.....Au hakuna unafuu utakaopatikana zaidi ya huu wa TANESCO?