Tanesco Iringa: Ajali Kazini ama Uzembe Kazini?

Tanesco Iringa: Ajali Kazini ama Uzembe Kazini?

MaxShimba

Platinum Member
Joined
Apr 11, 2008
Posts
36,008
Reaction score
4,093
Fundi wa Shirika la Umeme Tanesco mkoani Iringa, Selemani Mbuma akiwa amenaswa na umeme baada ya wenzake kuwasha umeme kimakosa wakati akiendelea na matengenezo katika eneo la Mlandege mkoani humo.

Matatizo haya hujitokeza mara kwa mara Je swali la kujiuliza huwa hawawasiliani pindi wanapotaka kurudisha umeme huo? au hakuna fundi in charge ambaye ndio kiongozi wa msafara wa ufundi ambaye ndie atakaye husika na miongozo yote ya kuhakikisha kuwa hakuna mtu anaye endelea na matengenezo ndio umeme uwashwe? jibu naweza jipa mwenyewe kuwa lazima awepo ila ni Ufanyaji kazi wa mazoea na kuwaamini sana hawa wanaoitwa saidia kuwapa majukumu yaliyokuwa makubwa kuliko uwezo wao na ndio makosa kama haya yanatokea, maisha ya mtu yanapotea kwa uzembe wa kizembe kama huu

 
Huu ni uzembe aisee, wahusika hapo inabidi wawajibike. By the way alipona au alikufa?
 
hapo kuna uzembe wa hali ya juu! wawajibishwe waliohusika kuwasha huo umeme
 
Back
Top Bottom