Tanesco hawana mita[luku]

mfianchi

Platinum Member
Jul 1, 2009
11,842
8,231
Nimekerwa na Tanesco mkoa wa Kinondoni Kaskazini pale Mikocheni, niliomba kuunganishiwa umeme kwenye kahekalu kangu pale Wazo,nimelipia kila kitu nikaahidiwa kuwa nitapigiwa simu kunitaarifu kuwa wanakuja kuunganisha huo umeme, naam kwanza baada ya mkaguzi kukagua uwekaji wa nyaya na kuridhia kuwa ziko sawa nikaambiwa nikalipie,lakini siku niliyoambiwa nikalipie nilikuwa busy ,walipoona muda unaenda nami sijaenda kulipia nikapigiwa simu siku hiyo hiyo kuwa natakiwa nikalipie hiyo 455,000.00.

Sasa naona shida yao tanesco imeisha baada ya kupata hiyo hela kwani hakuna umeme wala hata kupiga simu kunitaarifu kuwa tuna uhaba wa hizo mita. Leo nikaamua nipige kwata hadi hapo tanesco kwenda kuulizia kulikoni mbona sasa wiki iya pili inakatika na hamji kuunganisha huo umeme, jibu nililo ambiwa limeniacha hoi nimeambiwa nisubiri hadi mwezi ujao kwani kwa sasa hawana mita [LUKU] sasa najiuliza wakati wananipigia simu kuwa nikalipa hawakujua kama hawana hizo mita,kwani hiyo hele si ningezalishia kwa kuwekeza kwenye shughuli nyingine,kama hawakuwa na LUKU kwanini waliniharakisha kwa kunipigia simu kuwa nikalipe?

Hakika Tanesco wanakera sana. Kwa mambo kama haya yakizidi kuendelea sijui huo ufanisi utatoka wapi,kwa uzembe huu mimi naathirika zaidi ingawa wao Tanesco hawaoni hasara kukosa mapato kwani wanajua nipende au nisipende nitawasubiri tu.

Sijui niende EWURA kuwashitaki hawa watu?
 
Habaria wakuu,natafuta meter ya luku ya kununua kwa mtu(meter za dealsz).kama kuna mtu anazo au anajua mahali naweza pata ani pm au call 0654000253:
 
utanunua za wizi halafu iwe taabu kwako kuna shida gani ukienda tanesco wakakupa mpya
 
Kwanini usiunganishe nyaya tu, halafu uendelee kutumia? Kwani Luku inawekwa kwa ajili gani? VYA BURE VIBAYA SANA NDUGU.
 
Mkuu mbona Tanesco siku hz hawana shida?unalipia service line ambazo ni 460,000 unasubiri zako watakuja wenyewe hakuna kufukuzia kama zamani!naona wamejirekebisha kwa hilo!

Ukinunua ya deal wakigundua watai delete kwenye system halafu utashindwa kununua umeme utajipeleka mwenyewe!kisha unakua umeliwa hela yako!hata ukiipata kwa laki moja itakula kwako kaka!
 
Wabongo kwa dili za kujilisha hasara ndo wenyewe!! Badala ya kuumiza kichwa kupiga dili kubwa kubwa kama kukopa bank 500Mil bila kuwa na chochote,wewe unataka kamita. Ushauri wangu, achana na hako kadili, ukiona hela haitoshi wewe jipange tu zitafika, kama vipi weka PV system or Wind Turbine kwa ajili ya matumizi mhimu tu.
 
kwa sasa hivi Tanesco haina mita za luku huu ni kama mwezi wa tano...........hakuna miter kbs so jamaa ana haki ya kutafuta ya dili maana hali si hali!!!!
 
Kuna jamaa mmoja huwa anauzaga vitu vya wizi na mafuta ya transifoma ngoja nimuulize kama anaweza kupata mita,
oh sorry! Namba yake imefutika!
 
Mkuu aikurwa!sijui upo mji gani!mm jana jamaa wamenifungia mita ya Luku!sijafuatilia wala nn,nilikua bussy na mambo yangu,nimerud jion nakuta umeme unawaka!mita zipo mkuu!taabu wabongo tumezoea kutoa rushwa.
 
Nadhani mtoa mada ni mtu wa TANESCO yupo katika kupima hili na lile!Sijawah kusikia mtu anataka mita ya kununua mkononi kwa mtu.halafu itafungwa wapi?kila mita ipo katika system.......
 
Shida ya hiyo dili unajua kwanini inauzwa??

Pengine jamaa mwenye hiyo mita utakayouziwa alikamatwa anachakachua ndio ikatolewa uje uingie mkenge,
Kama Tanesco zipo nakushauri tukazichukue hizo
 
Wabongo kwa dili za kujilisha hasara ndo wenyewe!! Badala ya kuumiza kichwa kupiga dili kubwa kubwa kama kukopa bank 500Mil bila kuwa na chochote,wewe unataka kamita. Ushauri wangu, achana na hako kadili, ukiona hela haitoshi wewe jipange tu zitafika, kama vipi weka PV system or Wind Turbine kwa ajili ya matumizi mhimu tu.
Hihiii, hapo umenigusa; kuna Bank moja niliwaomba wanikopeshe 850M dhamana hchocho nachotaka kununua wakazingua, ebu nipe mchongo jinsi ya kukopa bila dhamana? hihiiiiiii:eyebrows:
 
Aidha yeye mwenyewe mwizi au anataka kujua wezi
shukrani kwa comments zenu may b let me respond abit,
1.meter za deals zinahusisha meter za luku ambazo either mtu anahama,au meter yake ni mbovu amenunua nyingine so ile emekuwa repaired na technitians,then inauzwa. Au meter za zamani za luku mtu anawish kuinstall mpya(hivyo ndo nilivyoelekezwa na watu).so i came with the writting kufahamu zaidi.
2.kwa insue ya kuwa naweza uaiwa kimeo i didnt know so thanks ntakuwa makini.
3.mi siyo mwizi wakuu,ila let me use deals,na prefer vitu vyasecond hand,a bit cheap.
4.natafuta meter hii cause wenye nyumba wanamgao wao,umeme saa moja asubuhi hadi saa 11 jioni haupo so,nataka ni solve problem at lower cost,
5.kwa maisha ya bongo second hand stuffs ni kitu cha kawaida sana,so dont be scared nkitafita second hand,laki nne parefu sana.

HITIMISHO:bado nasisitiza natafuta meter za deals,any one knows pse call me o ni pm.i hope am not wrong.
 
Kwa muda wa kama four months, upatikanaji wa LUKU ya card imekuwa ngumu. Vituo vingi kwa sasa hawatoi huduma ya kuuza LUKU za card na wanasema kuwa TANESCO hawana card.
Tunaomba TANESCO watoe jibu na ufumbuzi wa tatizo hili.
 
jamani nimelazimika kuomba msaada hapa baada ya kuwa njia zingine zote zimeshindikana, shida yangu ni moja tu, nataka umeme jamani nimewalipa tanesco yapata miezi miwili sasa lakini naambiwa kuwa eti hawana LUKU metres, sasa nashindwa kuelewa nifanye nini nimeishi bila umeme kwa zaidi ya miezi mitano sasa nma kama nilivyosema nimeshalipa kila kitu, please heeeeeeeeelp!!!!!
 
Hv hili linawezekana?

Hata Mi nitahitaji!


Huwezi jua bana, sasa kama imewezekana tanesco kukosa luku na ndio bidhaa inayowaingizia kipato, hii itashindikana vipi, kuna jamaa aliniambia yapo maduka yanayouza mita hizo lakini eti tanesco hawazitapokei sasa sielewei wanamuuzia nani au wanaweka madukani kwa nini, lakini ukweli ni kwamba nimechoka kabisa.

kwani humu hakuna wa tanesco? hebu jitokezeni mtupe solution.
 
Back
Top Bottom