The best person (mzawa) kuliongoza shirika kama Tanesco angekuwa Idrisa. Track record yake hata akiwa BOT ilikuwa nzuri. Mlishawahi kusikia matumizi mabaya ya account ya EPA au scandal yeyote wakati wa tenure yake pale BOT.
Doa pekee labda ni hizo payment zilizofanyika kwenye account yake kupitia kwa Andy Chenge. La kustaabisha ni kuwa hamna/hakuna mtu aliyemfuata kumuuliza his side of story (kama anayo hiyo obligation).
Hatoi posho au magari kwa wa wabunge/wanasiasa .
Critics wake should come out with suggestions na siyo kulaumu tu. Kama mnaona hafai basi angalau msuggest nani anaweza kuchukua nafasi hiyo.
Hebu njoo na ushahidi wa moja kwa moja. Dili la Rada lisingewezekana km asingemshirikisha????? Huu si ushahidi wa kiutendaji. Hawa na banker wa serikali. Serikali wanaweka pesa zao pale, mwenye fedha akizitaka je?? Rejea vizuri historia ya EPA maana mchezo huu umefanyika wakati wanahamisha zile akaunti toka NBCDCP iliyotafuna mabilioni ya fedha kuliko mwanaye EPA ilizaliwa wakati wa mzee rukhsa akiwa Raisi, Kikwete, Waziri wa Fedha na Rashidi, Gavana wa Benki Kuu. IPTL iliitangulia Richmond na wahusika wakuu wa IPTL ni hao hao - Mwinyi akiwa Raisi, Kikwete akiwa Waziri wa Nishati na Rashidi akiwa Benki.
Dili la Rada lisingewezekana kama lisingemshirikisha Gavana wa Benki wakati huo akiwa Dr. Idris Rashidi. Msaidizi mkubwa wa Chenge kama mwanasheria alikuwa mtaalamu wa fedha na msimamizi mkuu wa Benki Kuu ambaye alikuwa Rashidi.
Labda hatoi posho kwa kuwa ni mchoyo - anajilipa yeye tu na wasaidizi wake au washirika wake wana nguvu zaidi ya hao wanasiasa. Umewahi kujiuliza baada ya hicho kiasi kikubwa cha fedha kuingizwa kwenye akaunti yake bado anatafuta nini TANESCO.
Unaweza kuwa sahihi JokaKuu lakini kumbuka nchi yetu imejaa saana kupakana matope. Hebu angalia hoja za Mrema hapo pembeni, watu wanaandika tu ili kuchafuana. Hiyo issue ya import support na nyinginezo mbona asifikishwe mahakamani?Zitto,
..je, ni kweli kwamba Dr.Rashidi alituhumiwa ktk ripoti ya Tume ya Bunge iliyoongozwa na Edward Oyombe Ayila kwa ku-mismanage fedha za Import Support?
..wakati huo Dr.Rashidi alikuwa ni Mkurugenzi wa Idara BOT. baada ya hapo akapelekwa NBC kuwa DG, na baadaye akateuliwa kuwa Governor.
..vipi kuhusu zile tuhuma za kujipatia mkopo toka PPF yeye na Frederick Sumaye?
..na hizi tuhuma za majuzi zinazomkabili yeye na Andrew Chenge?
..inawezekana kwamba jamaa ni efficient hapo Tanesco, lakini ifike mahali tuwakatae hawa watumishi wenye rekodi za kifisadi-fisadi.
Richmond hakusaini Rashidi ila amedai kuwa hataki lawama pamoja na kwamba anataka mitambo ya kifisadi ambayo ni chakavu inunuliwe....Alitaka aondoke lakini bado wanamwitaji,kazi bado haijaisha,mitambo bado haijanunuliwa,kisingizio cha uchapa kazi,almost break even pamoja kwamba hakusaini Richmond aka Dowans anayoipenda ndio pazia la kuuwa soo.JF ina mambo mwingine anasema Richmond alisaini Dr Idris!
hizi tuhuma hazifikishwi mahakamani kwa sababu ni karibia wote walio kwenye position wanahusika au wanalindana.Unaweza kuwa sahihi JokaKuu lakini kumbuka nchi yetu imejaa saana kupakana matope. Hebu angalia hoja za Mrema hapo pembeni, watu wanaandika tu ili kuchafuana. Hiyo issue ya import support na nyinginezo mbona asifikishwe mahakamani?
Vipi hamkuingia gizani kwa kuwepa DOWANS? Vipi sasa gharama za IPTL ni nafuu kuliko DOWANS. Yale mafuta yanauzwa kiasi gani. Tuache siasa za majungu. Ubishi na kuchanganya siasa na professional zimeligharimu Taifa.Richmond hakusaini Rashidi ila amedai kuwa hataki lawama pamoja na kwamba anataka mitambo ya kifisadi ambayo ni chakavu inunuliwe....Alitaka aondoke lakini bado wanamwitaji,kazi bado haijaisha,mitambo bado haijanunuliwa,kisingizio cha uchapa kazi,almost break even pamoja kwamba hakusaini Richmond aka Dowans anayoipenda ndio pazia la kuuwa soo.
Nadhani hii ya Liyumba niliisema pia siku za mwanzo baada ya shahidi wa kwanza kuwa Liyumba atakuwa acquitted na serikali italipa fidia ya mabilioni.bnhai,
..Viongozi karibu wote Tanzania ni wachafu.
..ukiona kiongozi amepelekwa mahakamani ujue wenzake wameamua kumtoa kafara tu.
..kesi kama za Liyumba na Mramba kwangu mimi naona ni suala la "funika kombe" tu.
..kwenye kesi kama ya Liyumba sasa imekuwa ni vichekesho tu manaake mashahidi wa mashtaka wanatoa kauli za kumsafisha mshtakiwa.
..Mramba anashtakiwa kwa kusababisha hasara ya Bilioni 11. wakati huohuo serikali imeamriwa na mahakama kulipa Bilioni 15 baada ya Waziri Magufuli kutoa amri ya kuvunja kituo cha mafuta kule Mwanza. kwa hali ya kawaida si Magufuli naye angepaswa kupelekwa mahakamani?
Ni nani aliyesema kama si wewe mwenyewe?JF ina mambo mwingine anasema Richmond alisaini Dr Idris!
bnhai,
..kesi ya Liyumba siilewi vizuri.
..kama gharama za mradi zimekuwa inflated basi siyo Liyumba peke yake anayepaswa kuchunguzwa. hapa inabidi Contractor na Project Consultant nao wachunguzwe.
..au labda Liyumba alikuwa anatoa malipo pesa ambayo Contractor hajadai, na Project Consultant hajaidhinisha.
Dawa ni kutupa jongoro na mti wake....Kusema kweli mimi ni mtizamaji tu,sina isight,na kwa wenye insight kama wakipita hapa lazima watakuwa wanatucheka sana....Maana wanajua ni karata gani ya kucheza kwa wakati gani kwasababu hata sisi tunasubiri wao watasema nini and so tunachambua upi mchele ipi chuya.Hata hivyo nia hasa ya mafisadi ni kutulazimisha sisi tu "play by their rules" kwamba sasa heri nusu shari kuliko shari kamili....Gharama za IPTL ni kubwa sana hivyo tununue mitambo ya Dowans..Na ndio maana kuna wasiojali shari kamili,kwani hukusikia kuna wenye kudai kuwa heri wakae gizani kuliko kununua mitambo ya Dowans?Vipi hamkuingia gizani kwa kuwepa DOWANS? Vipi sasa gharama za IPTL ni nafuu kuliko DOWANS. Yale mafuta yanauzwa kiasi gani. Tuache siasa za majungu. Ubishi na kuchanganya siasa na professional zimeligharimu Taifa.
Moja tu - Amechukua u CEO pakiwa na hasara ya 162bn kwa mujibu wa audited accounts za 2006. 2007 hasara ilishuka mpaka 67bn. 2008 imeshuka mpaka 30bn na mpaka june 2009 tayari TANESCO ilikuwa imebreak even. Kama sio mgawo wa Septemba, Oktoba na Novemba wangepata faida mwaka huu.
Mbili - kwa mara ya kwanza Taasisi za fedha zimekopesha TANESCO 400bn na wana service mkopo huo bila tatizo lolote na hivyo kuweka mazingira ya kukopa zaidi.
Tatu - Shirika lina mpango wa muda mfupi, wa kati na mrefu wa kuzalisha na kusambaza umeme. Miradi yote ya kuanzia mwaka jana imekwamishwa na Serikali kama Mhisa mkuu.
Nne - Sasa Shirika lina rejesta ya mali zake zote (zenye thamani ya 1bn usd) na wakati Rashidi anaingia CAG alitoa disclaimer audit opinion kwa kuwa pamoja na mambo mengine Shirika halikuwa na orodha na thamani halisi ya mali zake. NHC wana tatizo hilo na Kamati ya Bunge ya Mashirika ya Umma iliwatimua na mpaka leo hawajaweza kufanya kama TANESCO.
Tano - Yupo very clear anataka Shirika lifike wapi kwa muda gani. Kwa mfano kama Mhisa pekee (serikali) angetekeleza commitment zake na faida iliyotarajiwa mwaka huu ikawa realised, lengo lilikuwa ni kustain faida kwa miaka mitatu ili TANESCO iuze hisa zake DSE na hivyo public listed company - kuongeza uwazi kwa mujibu wa masharti ya PLCs.
Niendelee?
Zitto
mbona uko shallow hivyo? Hiyo hasara iliyopunguzwa uliomba kupata detailed schedule kujua ni ongezeko la Revenue au kupungua kwa gharama za uendeshaji kabla ya conclude?Kwa mfano kama malipo ya Richmond yalisimamishwa na unacompare vipindi hivyo viwili lazima utaona tofauti.je bei ya umeme iliongezwa? kwenye uhasibu tunaita analytical Review sio unakurupuka tu nakusema ooh hasara imeshuka kwa hiyo rashid ni mkurugenzi mzuri jiulize what were the factors leading to that?je accounting procedures zimebadilishwa.. kwa mfano unaweza kukuta kuna vitu vilikuwa vinakuwa expensed sasa viko capitalized wher u just charged depreciation in the PL kwa bottom line number inaonekana nzuri,kuna mambo mengi ....inabidi ujue accounts...... Yani mtu anahusika kuchannel pesa za rada unamwita best CEO .. anyway haishangazi sasa ... waarabu wa pemba hujuanan kwa vilemba...