Tamthiliya Zinachangia Ndoa Nyingi Kuvunjika

Tamthiliya Zinachangia Ndoa Nyingi Kuvunjika

Darren2019

JF-Expert Member
Joined
Nov 23, 2019
Posts
1,111
Reaction score
2,413
Wakuu haya ni maoni yangu binafsi baada ya kuangalia tabia za familia nyingi hasa za mjini.

Hivi karibuni kulitoka ripoti iliyoonyesha wingi wa ndoa zinavyovunjika Dar es Salaam.

Ukitazama maisha ya mjini familia nyingi zinamiliki Tv na nyakati za usiku channels nyingi hata zile za kawaida huonyesha tamthiliya.

Wanawake wengi ni wapenzi wa hivi vipindi vya maigizo hivyo hujikuta wakisalia sebuleni au kuweka concentration yao kwenye tv huku wakipishana na waume zao wakielekea kitandani kwenda kulala peke yao kwa kuwa wanaume walio wengi siyo wapenzi wa tamthiliya.

Kitendo hiki humfanya mwanaume ajione mpweke na asione umuhimu wa kuoa na mwishowe kuzaa migogoro ambayo hatima yake ni kuvunjika kwa ndoa kwa kuwa baadhi hujiongeza kutafuta faraja nje ya familia.

Wito wangu, wanawake tambueni wanaume tunapenda kusikilizwa, tunapotoka mihangaiko ya kutwa tunahitaji kufarijiwa, shauri yenu, Mimi nimemaliza.

Naomba kuwasilisha!
 
Binafsi narudishagwa kwetu kipindi cha UEFA sijui EFL...[emoji6][emoji854][emoji6][emoji846]
Tuvumiliane tu...
 
Kwamba wanashindwa kukaa na kuyamaliza kweli
 
ulevi nao unachangia pia,mwanamme unarudi sa sita mkeo unamfanya sa ngap?nawe mwanamke movie angalia mara mojamoja inawezekanaje mwanamme aende kulala afu we uendelee na kipindi
 
ulevi nao unachangia pia,mwanamme unarudi sa sita mkeo unamfanya sa ngap?nawe mwanamke movie angalia mara mojamoja inawezekanaje mwanamme aende kulala afu we uendelee na kipindi
Hapa Mkulu kama unanisema mimi daily ni kumi usiku sijui alfajiri ndio narudi ushakua uraibu ngoja nirudi kwenye maombii labda itasaidia .
 
Unaamka asubuhi kuchek views zako unakuta mke wa mtu ni miongoni mwa views zako, tena kaangalia usiku wa manane!! Hili ni janga la tano kwa Taifa. Naamuru nalo likaangaliwe
 
Upo sahihi kipindi cha UEFA gemu zao zinaisha saa nane tulikua tunawatesa sana wanawake unakuta gemu zipo Jumanne na Jumatano na zote kali dstv yenyewe ilikua ya kuunga unga mpaka ukaangalie bar ukirudi usiku muda huo ingawaje wengi walikua hawasemi ila ilikua mtihani kidogo kwao..ila wanawake wengi sasa hivi wanataka kuishi maisha ya Bongo movie na wanawafatilia sana wakati hawana mafunzo yeyote ya maana zaidi ya kuachana kila kukicha na wanaume..
 
Uki sahihi. Mzee wangu toka ajue hilo halipii kingamuzi. Muda wote bi mkubwa yupo anaangalia Sinema Zao hadi usiku wa manane. Mwendo wa tbc kwenda mbele.
 
Back
Top Bottom