Tamko la wajumbe baraza kuu chadema - mkoa wa pwani dhidi ya 'wasaka tonge'

Edward Kinabo

New Member
Nov 24, 2012
3
3
TAMKO LA WAJUMBE WA BARAZA KUU LA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA) KUTOKA MKOA WA PWANI


UTANGULIZI
Ndugu wanahabari, wanachama, wapenzi na wafia chama wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika Mkoa wa Pwani na nchini kwa ujumla.

Tumeamua kuzungumza nanyi waandishi wa habari kwa lengo la kuufikisha ujumbe wetu kwa watanzania wote walio ndani na nje ya nchi yetu, wenye mapenzi mema na nchi hii, ujumbe huu umebeba matumaini hasa kwa wale walio katika mapambano ya kweli ya kuhakikisha Mkoloni Mweusi yaani CCM anaondoka madarakani, si kutokana na kuwachukia kutokana na sura au maumbile yao, ila ni kwa sababu wameshindwa kabisa kutuletea maendeleo ambayo yangetuwezesha watanzania kuwa na maisha bora kama tulivyoahidiwa na Serikali ya CCM.

Ndugu wanahabari
Siku za hivi karibuni kumezuka mtindo ambao kwa namna moja ama nyingine unaratibiwa na viongozi wa CCM kwa mgongo wa waliokuwa viongozi wa CHADEMA ambao kwa sasa ni wanachama ama viongozi wa chama kipya cha Alliance for Change and Transparence – Tanzania (ACT - Tanzania). Tunaamini kuwa ni wanachama na viongozi wa ACT - Tanzania kwa sababu ushahidi wa kimazingira na kimwenendo pamoja na Taarifa kutoka Mkoa wa Tabora na Singida, Wilaya za Temeke, Pangani na Lushoto zinaonyesha kuwa hawa si wenzetu ila wanaendelea kuuhadaa Umma wa Watanzania kwa kujitambulisha kuwa ni viongozi wa CHADEMA, huku wakiwa mstari wa mbele kushiriki bila kificho kazi na majukumu ya chama hicho cha ACT –Tanzania, kama kushawishi watu kuwa wanachama na kugawa kadi za ACT wakiwa wamejificha katika koti la uongozi wa CHADEMA.

Ndugu wanahabari,
Mtakumbuka kuwa mnamo tarehe 23/06/2014, wasaka tonge hao waliitisha mkutano wa waandishi wa habari katika Hoteli ya Lamada Jijini Dar es Salaam, na kwa kiasi kikubwa mkutano huo uliitishwa kwa lengo la kuchafua hali ya hewa na kujaribu kuwaaminisha Watanzania kuwa ndani ya CHADEMA hali ni tete. Ukweli wa mambo ni kuwa CHADEMA hali ni shwari na kazi za kuimarisha mtandao wa chama zinaendelea vizuri na kwa mafanikio makubwa ambayo hayajawahi kufikiwa tangu kuanzishwa kwake. Wasaliti hao baada ya kujionea hali ya kutoungwa mkono na Watanzania, jana tarehe 25/06/2014, walikusanya watu ambao hakuna hata chembe ya ushahidi kuwa ni wanachama wa CHADEMA na kwenda nao katika Ofisi za Msajili wa Vyama vya Siasa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, huko waliwasilisha madai yao ambayo tunaamini kuwa yanatolewa wakati huu ili kuwaondoa watanzania katika mstari wa kujadili mambo makubwa yaliyo mbele yetu kama masuala ya Katiba Mpya, Ufisadi katika ITPL, Bajeti iliyomwiba mchungu kwa wananchi wa hali ya chini na ukata katika maeneo mbalimbali ya Umma:

Kutokana na utangulizi huo, Wajumbe wa Baraza Kuu la CHADEMA kutoka Mkoa wa Pwani wanapenda kuzungumzia hoja zao kwa lengo la kuweka sawa kumbukumbu na kuinua ufahamu wa watanzania juu ya hila hizo zinazoandaliwa kwa lengo la kuwasahaulisha masuala muhimu tuliyo nayo sasa.


  1. KUSHINDWA KWA UONGOZI WA KITAIFA.

Ndugu wanahabari,
Wasaka tonge, wameelezea Umma wa Watanzania kuwa Viongozi wetu wakuu yaani Mwenyekiti wa Taifa Mhe, Freeman Mbowe na Katibu Mkuu Dkt Wilbroad Peter Slaa wameshindwa uongozi hivyo waachie ngazi.

Sisi tunajiuliza umakini wa hao watu uko wapi? Tunapata maswali mengi ambayo hayana majibu, kwa kuwa kipindi hiki CHADEMA kipo katika mchakato wa Uchaguzi wake na mwezi huu mpaka Julai tunakamilisha chaguzi za ngazi ya Kata kwa Wilaya na Majimbo yote ya mkoa wa Pwani ambayo hayajakamilisha chaguzi hizo, mwezi Agosti tunarajia kufanya uchaguzi ngazi ya Mkoa tukisubiria mwezi Septemba kukamilisha mchakato wa uchaguzi wa Chama kwa kuchagua viongozi wa ngazi ya Kitaifa. Sasa kama kweli wanaona viongozi wetu wakuu wameshindwa kuongoza kwa nini wasisubiri wawaondoe katika uchaguzi mkuu wa chama? Badala yake wanakimbilia kutoa matamko yasiyo na tija ambayo hayaendani na Miongozo, kanuni, na Katiba ya CHADEMA.

Sisi wajumbe wa Baraza Kuu la CHADEMA kutoka Mkoa wa Pwani tunaamini kuwa Viongozi wetu ni shupavu na wana weledi mkubwa katika masuala ya uongozi. Ndani ya uongozi wao CHADEMA imeweza kusambaa nchi nzima na kuwa na wanachama katika Mikoa, Wilaya, Tarafa, Kata, Vijiji, Mitaa na Vitongoji, tumeongeza idadi ya wabunge kutoka 4 na madiwani 42 mwaka 1995 hadi wabunge 5 na madiwani 74 mwaka 2000, na kutoka wabunge 5 na madiwani 74 hadi wabunge 11 na madiwani 102 mwaka 2005, na kutoka wabunge 11 na madiwani 102 hadi kufikia wabunge 49 na madiwani 520 huku tukiongoza halmashauri kadhaa mwaka 2010.

Kwa ubunifu wa viongozi wanaoitwa wameshindwa kazi, tumeanzisha program ya CHADEMA ni Msingi ambayo inakipelekea chama kuwa na mtandao mkubwa na kuweza kukabiliana na hila za CCM mpaka kwenye mizizi. Vile vile tumeweza kushiriki chaguzi ndogo kuanzia za Viongozi wa Vijiji na Mitaa, Madiwani na Wabunge kwa kipindi cha kuanzia mwaka 2011 katika chaguzi ndogo tumeweza kupata Jimbo moja la Arumeru Magharibi ambalo lilikuwa linashikiliwa na CCM. Hayo ni baadhi tu ya mafanikio yaliyofikiwa katika uongozi huu



  1. UBADHILIFU WA FEDHA NA MALI ZA CHAMA
Ndugu wanahabari,
Kinachoelezwa katika kipengele hiki kwenye tamko la wanaojiita wajumbe wa Baraza Kuu na Mkutano Mkuu, ni mwendelezo wa hadithi au riwaya za kinafiki na hazikuanza leo maana ziko mpaka kwenye mkakati wa mabadiliko 2013, mtakumbuka kuwa mwaka jana kuna mtu alijitokeza na kuuaminisha Umma wa watanzania kuwa CHADEMA haikaguliwi, hivyo wapinzani wetu wakaanza kutembea na kauli hizo kwa kumuamini kwa kuwa alikua kiongozi, lakini tokea CAG aanze mchakato wa kukagua hesabu za vyama vya Siasa na kukamilisha bila kukipa chama hati chafu na bila kubaini ufisadi wowote kelele hizo zimekwisha.

Sisi tunaamini kuwa Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali ndiye mwenye taarifa za mwenendo wa matumizi ya fedha katika CHADEMA na mwenye kuujua ukweli kupitia wataalamu wake kuliko wanaojivika taaluma ya fedha ambayo hawanayo.


  1. UVUNJIFU WA KATIBA NA KANUNI ZA CHAMA
Ndugu wanahabari,

Katika kipengele hiki wajumbe hao wakiongozwa na aliyekuwa kiongozi wa Temeke na kufukuzwa, katika tamko lao, wameainisha vipengele vitatu vya katiba ya chama vilivyovunjwa kwa mtazamo na matakwa yao, tunaomba tuvitolee ufafanuzi kama ifuatavyo:


  • Kitendo cha kutoka na kususia kwenye Bunge maalum la Katiba

Ndugu wanahabari,

Tunawashangaa sana hawa wanaojiita Wajumbe wa Baraza kuu na Mkutano Mkuu ambao hata mapendelezo ya Chama kwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba hawayafahamu. Katika waraka Na.1 wa mwaka 2013 wa CHADEMA ulihusu Maoni na Mapendekezo ya CHADEMA kuhusu maudhui na mchakato wa Katiba Mpya. Sehemu ya kwanza ya waraka huu ilihusiana na utangulizi ambao ulielezea kuwa kikao cha Kamati Kuu cha tarehe 15 – 16/12/2012, pamoja na ajenda zingine ilipokea taarifa kuhusu mchakato wa mabadiliko ya Katiba na Kamati kuu iliazimia January 2013 kupitia Kamati yake maalumu iwasilishe mapendekezo ya CHADEMA kwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba juu ya maono ya CHADEMA. Sehemu ya pili ya Waraka huo ilikuwa ni maoni ya CHADEMA juu ya Maudhui ya Katiba Mpya ya Tanzania na kuonyesha kuwa muundo unaopendekezwa ni wa Shirikisho lenye Serikali tatu litakaloundwa kwa hiari na nchi za Tanganyika na Zanzibar. Tunaamini na kususia Bunge Maalumu la Katiba ni kutekeleza kwa vitendo maoni na mapendekezo ya CHADEMA juu ya Muundo wa Muungano ambao kwa bahati nzuri wananchi walio wengi wameungana na CHADEMA katika pendekezo hilo na kusababisha Tume ya Mabadiliko ya Katiba kuweka muundo huo katika Rasimu ya kwanza na ya Pili ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano.






  • Kitendo cha kuunda baraza kivuli la mseto

Ndugu wanahabari,

Ukiona mtu ambaye anajiita kiongozi anaanza kuhoji kuundwa kwa Baraza Kivuli la Mseto katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inakupasa ujiulize mara dufu kuwa huyu mtu ana akili timamu kweli? Wahenga walieleza kuwa Umoja ni nguvu na utengano ni dhaifu. Baraza Kivuli ni Kielelezo tosha juu ya uwepo wa Ukawa, anayepingana na hilo lazima atakuwa anatekeleza na kusimamia maoni ya CCM.


  • Kutokuitishwa kwa mkutano mkuu wa Baraza kuu

Ndugu wanahabari,

Uwakala wa hao Jamaa kwa CCM unajidhirihisha hapa, wakati wanaelewa kuwa tupo katika mchakato wa Uchaguzi wa Chama na katika mwaka wa Uchaguzi Baraza kuu litaitishwa baada ya kukamilika kwa uchaguzi wa Ngazi za Mikoa. Ibara ya 7.7.11, inaelezea wajumbe wa Baraza Kuu kuwa ni Wajumbe wote wa Kamati Kuu. Wenyeviti wa Baraza la Uongozi, Mikoa, Wajumbe wateule wasiozidi sita watakaoteuliwa na Mwenyekiti wa Taifa kwa kushauriana na Katibu mkuu na kuidhinishwa na baraza kuu, Wajumbe wateule hawa watateuliwa kwa uwiano wa wajumbe wanne wanaume wawili na wanawake wawili, Wajumbe watano watakaochaguliwa na Mkutano Mkuu wa kila Baraza la Chama, kwa uwiano wa wajumbe wanne toka Bara na mmoja toka Zanzibar kwa kila Baraza, Wenyeviti wa wilaya za chama na Mwakilishi wa jimbo na chama. Na kwa kuwa Mkutano wa Baraza Kuu hufanyika mara moja kwa mwaka ni dhahiri kuwa wajumbe hao watapatikana katika mchakato huu, kwa maana nyingine ni kuwa Wajumbe wa Baraza kuu waliopo sasa watashiriki katika Mkutano wa Baraza kuu lijalo kama watachaguliwa tena kuwa Viongozi katika mchakato wa uchaguzi unaendelea kwenye maeneo mbalimbali.

Tunapoelekea kufikia tamati ya taarifa yetu tungependa kuelezea Maadili ya Viongozi na Wanachama wa CHADEMA ambayo wanatakiwa kuishi katika kuyatekeleza kwa kiimani na kivitendo, hayo yanapatikana katika Ibara ya 10.1 na 10.3 ya Katiba ya CHADEMA. Sisi tunaamini kuwa hawa wanaojiita wajumbe wa Baraza Kuu na Mkutano Mkuu wa CHADEMA wameenda kinyume na Katiba hasa kama kweli wana uhalali wa kujiita viongozi katika ibara ya 10.1. (viii), (ix), (x), (xi) na (xii). Vile vile wamevunja Maadili ya Wanachama yaliyoainishwa katika ibara ya 10.3. (1) tunanukuu "Pamoja na sifa, haki na wajibu wa mwanachama kwa mujibu wa sura ya Tano ya Katiba ya Chama, kila mwanachama anatakiwa awe na tabia ambayo ni mfano wa kuigwa na jamii na ya kukiwezesha Chama kukubalika kwa jamii anamoishi huyo mwananchama. Kwa hiyo kila mwanachama anatakiwa kuzingatia yafuatayo:-
(1) Kuwa mkweli kuhusu uanachama wake kwa kutokuwa na uanachama wa chama kingine cha siasa".

MWISHO:

Tunawashukuru sana wanahabari na tunaomba mfikishe taarifa hii kwa umma wa Watanzania ili utambue kuwa kile kilichotolewa na kundi la mawakala wa CCM lengo lake kuu ni kudhoofisha harakati makini za CHADEMA ambazo zimeongezewa chachu na uwepo wa UKAWA. Lakini pia, umma wa Watanzania na wapenda mabadiliko kote nchini wanapaswa kujiuliza wajumbe hao kutoka mikoa ya Tabora, Singida na Kigoma wanafadhiriwa na nani kwa siku wanazoishi DSM? Wanasafirishwa na nani, na walala wapi kwa wingi wao kwenye jiji ambalo takwimu zinaonyesha kuwa ni miongoni mwa jiji ghali Afrika Mashariki lenye changamoto kubwa ya usafiri?

"KWA PAMOJA TUTASHINDA"

IMEANDALIWA NA:-


  1. Saidi Mtipula Ukwezi – Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Pwani
  2. Jamal Lwei - Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Mkuranga
  3. Saidi Kigomba - Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Mafia
  4. Ally Mtwindi - Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Rufiji
  5. Nasoro Kaparama - Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Kisarawe
  6. Bumija Moses Senkondo- Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Kibaha
  7. Richard Mbalase - Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Bagamoyo
  8. Kinabo E. Kinabo – Mjumbe Baraza Kuu (kupitia BAVICHA) - kutokea Mkoa wa Pwani

IMESOMWA LEO TAREHE 27/06/2014 NA:-
SAIDI MTIPULA UKWEZI
MWENYEKITI WA CHADEMA MKOA WA PWANI
 
Hili ndilo tamko la wazi lililoenda shule, siyo watu wanafinyanga finyanga mambo yasiyoeleweka.
 
IMEANDALIWA NA:-


  1. Saidi Mtipula Ukwezi – Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Pwani
  2. Jamal Lwei - Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Mkuranga
  3. Saidi Kigomba - Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Mafia
  4. Ally Mtwindi - Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Rufiji
  5. Nasoro Kaparama - Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Kisarawe
  6. Bumija Moses Senkondo- Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Kibaha
  7. Richard Mbalase - Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Bagamoyo
  8. Kinabo E. Kinabo – Mjumbe Baraza Kuu (kupitia BAVICHA) - kutokea Mkoa wa Pwani

IMESOMWA LEO TAREHE 27/06/2014 NA:-
SAIDI MTIPULA UKWEZI
MWENYEKITI WA CHADEMA MKOA WA PWANI

Nimeamini Chadema ni chama cha kidini
 
kwani chalinze iko mkoa gani?
chadema-saccos walipata % ngapi ya kura za uchaguzi mdogo mwezi jana?
nikisema hawa waleta hili tamko ni wanywa viroba nitakuwa nimekosea?
halafu nimeshangaa akina kinabo huko pwani.
hivi chadema hamuwaamini watu wengine zaidi ya wachaga wenzenu tu?
hebu wekeni utaifa mbele basi. hivi inaonekana kabisa mmezidi.
 
Hakuna mtu mwenye akili timamu chadema, wote mafyatu...si mtoto,mtu mzima na wanawake...full matusi
 
ccm/act mkajipange tena, hela yenu nodi imeliwa hivyo hata kabla kazi haijakamilika, ha ha ha
 
huyu kiongozi wa chama amepangua hoja za wasaka tonge vizuri mno, saafi sana
 
kuna wahuni wanahongwa na maccm kukichafua chama cha watu, watashindwa vibaya sana
 
Back
Top Bottom