Tume Haki Binadamu(THBUB)
Member
- Sep 17, 2024
- 26
- 28
Katika kipindi cha takriban mwezi mmoja na nusu, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) imekuwa ikifuatilia kwa karibu matukio mbali mbali ambayo yamekuwa yakijitokeza nchini. THBUB baada ya kufanya tathmini kuhusu matukio hayo kwa mujibu wa Katiba na Sheria ya THBUB, imejiridhisha kuwa matukio hayo yanaashiria uvunjifu wa haki za binadamu, ukiukwaji wa misingi ya utawala bora na uvunjifu wa amani na utulivu nchini.
Aidha, katika kipindi hiki kuelekea uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani, kumekuwa na matukio mbali mbali yakiwemo matumizi ya lugha chafu zisizozingatia utu na heshima ya mtu na zinazoleta hamasa na kuchochea uvunjifu wa amani na utulivu, matukio yanayoashiria matumizi ya nguvu kupita kiasi wakati wa kushughulikia mikusanyiko ya kisiasa, kushambuliwa na kujeruhiwa kwa baadhi ya wananchi ikiwemo tukio lililotokea tarehe 30 Aprili, 2025 la kushambuliwa na kujeruhiwa Kiongozi wa Kidini Padre Dkt. Charles Kitima, Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Tanzania na tukio la kutekwa kwa Faluka Saidi Nyagali kwa jina maarufu Mdude na matukio mengine.
THBUB inatambua kuwa kwa mujibu wa Katiba ya nchi, sheria za nchi na mikataba mbalimbali ya kimataifa ya haki za binadamu ambayo Tanzania imeridhia, wananchi wote wa Tanzania wana haki ya kufurahia na kupata haki zao za binadamu. Aidha, kwa mujibu wa Katiba ya Nchi, kila mwananchi anayo haki ya kuishi, kuwa huru, kutoa maoni na kushiriki katika shughuli za umma moja kwa moja au kupitia wawakilishi kwa kuzingatia masharti yaliyowekwa katika Katiba na sheria za nchi.
Pamoja na haki hizo, Katiba inaweka sharti la wajibu kwa kila mwananchi kutotumia misingi ambayo itasababisha kuingiliwa au kukatizwa kwa uhuru na haki ya watu wengine na kwamba pale mtu anapoamini kwamba haki yake imevunjwa anaweza kuwasilisha suala hilo Mahakamani au katika vyombo vyengine vyenye mamlaka kwa mujibu wa sheria.
Vile vile THBUB inatambua kuwa kwa mujibu wa sheria, Jeshi la Polisi limepewa dhamana ya kulinda usalama wa raia na mali zao na hivyo kwa kuzingatia sheria na maadili, Jeshi hilo lina mamlaka ya kushughulikia viashiria vyote ambavyo vinaweza kuhatarisha amani na utulivu nchini.
THBUB inaona kuwa matendo yaliyojitokeza hayatoi taswira nzuri katika ustawi wa haki za binadamu, utawala bora na amani na utulivu nchini ambayo ni muhimu sana katika kipindi hichi kuelekea uchaguzi Mkuu. THBUB inalaani matukio hayo ambayo yamevunja haki za binadamu na kukiuka misingi ya utawala bora na yanayoashiria uvunjifu wa amani na utulivu.
Kutokana na matukio yaliyotokea THBUB inapendekeza yafuatayo:
a) Jeshi la Polisi ambalo ndiyo taasisi iliyopewa dhamana ya kulinda usalama wa raia na mali zao kutekeleza wajibu wake kwa kufuata Katiba, Sheria na Kanuni;
b) Jeshi la Polisi liendelee kuwasaka na kuwachukulia hatua za kisheria waliohusika na kujeruhiwa kwa Dkt Charles Kitima, waliomteka Faluka Saidi Nyagali (Mdude) na waliohusika katika matukio mengine ya uvunjwaji wa haki za binadamu;
c) Msajili wa Vyama vya Siasa kuwataka viongozi wa vyama vya siasa kuzingatia matakwa ya Katiba na Sheria katika shughuli zao;
d) Serikali iendelee kukaa na wadau wa Demokrasia katika kuzitafutia ufumbuzi changamoto mbali mbali zinazojitokeza;
e) Viongozi na wananchi waendelee kudumisha amani na utulivu ambao ndio msingi wa kufurahiya haki za binadamu; na
f) Wadau wote wa uchaguzi kuwa na ustahimilivu wakati wa mchakato wa uchaguzi kwa kuwa ushindani wa kisiasa nyakati za uchaguzi ndio chachu ya demokrasia.
Jukumu la Ulinzi na Utetezi wa Haki za Binadamu na uzingatiwaji wa misingi wa Utawala Bora ni letu sote.
Pia, Soma