Tamko la serikali kuhusu migomo sehemu za kazi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tamko la serikali kuhusu migomo sehemu za kazi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Bajabiri, Jul 11, 2012.

 1. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #1
  Jul 11, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Wadau hili tangazo nimelikuta kwenye gazeti la mwananchi la leo,nimeona nilibandike hapa.

  Hivi karibuni kumekuwepo na wimbi la kuitishwa migomo isiyozingatia taratibu zilizowekwa kisheria.Kwa mujibu wa kifungu cha 80(1) cha sheria ya ajira na mahusiano kazini na.6/2004 ili mgomo uwe halali ni budi mambo yafuatayo yazingatiwe:
  1.Ni lazima kuwepo na mgogoro wa maslahi baina ya wafanyakazi na mwajiri.
  2.Mgogoro uwe umeishawasilishwa kwa kutumia fomu maalum katika tume ya usuluhishi na uamuzi.
  3.Mgogoro uwe haujapatiwa ufumbuzi baada ya siku thelathini(30) kupita tangu ulipopokelewa na Tume au katika muda wa siku thelathini za ziada zilizoongezwa na tume.
  4.Mgogoro uwe haujapokelewa na tume au katika muda wa siku 30 zilizoongezwa na tume.
  5.Mgomo uwe umeitishwa na chama cha wafanyakazi na kura imepigwa kwa mujibu wa katiba ya Chama cha Wafanyakazi husika na wengi wa wanachama wawe wanaunga mkono MGOMO
  6.taarifa ya masaa 48 itolewe kwa mwajiri ikielezea nia ya wafanyakazi kugoma.
  Hata hivyo kwa mujibu wa kifungu cha 76(1) cha sheria hiyohiyo wafanyakazi walio katika huduma muhimu hawaruhusiwi kugoma isipokuwa baada ya kukidhi vigezo kadhaa vinavyosimamiwa na kamati ya HUDUMA MUHIMU.

  Kupitia gazeti la MWANANCHI la tarehe 9.7.2012 Chama cha walimu tanzania wilaya ya Geita kimeazimia kufanya mgomo usio na kikomo kutokana na kile kinachodaiwa kuwa ni madai ya muda mrefu.
  Tayari chama cha Walimu Tanzania kimeishawasilisha mgogoro katika tume ya usuluhishi na uamuzi-Dar es salaam wenye namba za usajili CMA/DSM.ILALA/369/12 na tume inaendelea kushughulikia.
  Tunachukua fursa hii kuwataarifu wafanyakazi wote kuwa migomo ambayo si halali ina madhara yake ikiwa ni pamoja na kuchukuliwa hatua za kinidhamu dhidi ya wahusika.
  Mgomo uliozungumziwa kupitia gazeti la mwananchi ni BATILI.Hivyo serikali inawataka wahusika wote kujihusisha na vitendo vya uvunjaji wa sheria badala yake sheria na kanuni zinazotawala mahusiano sehemu za kazi ziheshimiwe na kuzingatiwa

  Imesainiwa na S.H kinemela
  Kamishna wa kazi
   
 2. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #2
  Jul 11, 2012
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,223
  Likes Received: 1,412
  Trophy Points: 280
  Ngoja nami niitishe mgomo usioisha maana watawala wetu wamezidi kutumia sheria, dora na mahakama kuwaziba watu midomo.
   
 3. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #3
  Jul 11, 2012
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Ina maana nchi ndiyo haitatawalika tena????? Maana kila siku ni mgogoro baina ya serikali na waajiri wake!!!!!
   
Loading...