Tamko la mbunge wa kigoma kusini

Don Alaba

Don Alaba

Senior Member
Joined
Nov 3, 2010
Messages
167
Likes
9
Points
35
Don Alaba

Don Alaba

Senior Member
Joined Nov 3, 2010
167 9 35
TAMKO LA MBUNGE WA KIGOMA KUSINI KUHUSU MGOGORO WA NISHATI YA UMEME NA KUSUDIO LA KUWASILISHA HOJA BINAFSI BUNGENI

JUMAPILI, DISEMBA05, 2010

Dar es Salaam.

UTANGULIZI
Karibuni wanahabari. Leo nimeamua kuwaomba kama wanahabari na watanzania wazalendo tujadili hatma ya Taifa letu ambalo utaratibu wa kuingizwa gizani na mgogoro wa nishati ya umeme unaelekea kukomaa na kuwa sehemu ya maisha ya watanzania.

Kwanza nipende kuwakumbusha tu kwamba tukiwa na nusu karne tangu tupate uhuru ni asilimia 14 tu ya watanzania ambao wanapata huduma ya umeme, kiwango ambacho ni sawa kabisa na takwimu za huduma hii kabla ya Uhuru takribani nusu karne iliyopita.Kwa vijijini kama jimboni kwangu na mkoa wa Kigoma kwa ujumla hali ni mbaya zaidi kwani kwa takwimu za sasa, ni asilimia 2 tu za watanzania vijijini wanaopata huduma ya umeme.
Lakini pia, tukumbuke kwamba bila nishati ya umeme ya uhakika hatuwezi kutekeleza MKUKUTA, hatuwezi kufikia MALENGO YA MILENIA, hatuwezi kufanikisha mpango wowote wa mapinduzi ama ya uchumi wala ya huduma. Takwimu mbalimbali na hata zile za Benki ya dunia zinaonyesha kuwa asilimia 40 ya uchumi duniani inategema nishati ya umeme.
Hapa Tanzania, kwa kasi ya ukuaji wa uchumi ya sasa ya takribani asilimia 7 kwa mwaka, uzalishaji wa Umeme unapaswa kukua kwa zaidi ya asilimia 15 kwa mwaka. Mahitaji ya Umeme nchini ni zaidi ya 1500 MW kwa mwaka, uwezo wetu ni kuzalisha 1034 MW lakini kiasi kinacho zalishwa ni 690MW tu kwa sasa kutokana na uchakavu wa mitambo na kupotea kwa umeme mwingi kwenye njia za kusafirisha. Hali hii ni mbaya sana kwa uchumi na inahitaji mikakati ya lazima kushughulikia.
Nikatika misingi hii watanzania tunawajibika kuwa wakali inapotokeo watu tuliowapa madaraka kutuongoza wanashindwa kutoa majibu ya msingi kuhusu masuala nyeti kama umeme.
Msingi mkubwa wa tatizo la umeme Tanzania ni serikali kufumbia macho miradi ya umeme ya uhakika ambayo ingetoa majibu ya kudumu ya tatizo hili na badala yake imebaki inasimamia sekta ya umeme kwa kudunduliza ikitumia mitambo ya kukodi ambayo kwa miaka sasa, tangu IPTL mwaka 1994 hadi Agreko, Songas, Richmond, Dowans imekuwa ikinyonya vibaya uchumi wa Taifa. Asilimia 86 ya mapato ya TANESCO yanatumika kulipia umeme unaozalishwa na mitambo ya kukodi ambayo inazalisha takribani asilimia 45 tu ya umeme wote. Hivi sasa mitambo ya kukodi inayotumika ni Songas na IPTL peke yake baada ya Agreko kumaliza mkataba wake na Dowans kufutwa mkataba wake. TANESCO wanailipa kampuni ya Songas takribani shilingi 266m kila siku kwa kununua 186MW za umeme. Mitambo ya IPTL ikiwa imewashwa TANESCO wanailipa kampuni hii shilingi 300m kila siku! Itakumbukwa kuwa TANESCO walikuwa wanapaswa kuilipa kampuni ya RICHMOND/DOWANS shilingi 152m kila siku kwa kununua 100MW za umeme.
Tangu mwaka 2006, serikali imeshindwa japo kupunguza tatizo hili la mgawo wa umeme. Viongozi wakuu wa serikali na hasa Waziri wa Nishati na Madini mara kadhaa wamekuwa akipotosha watanzania kuwa serikali inashughulikia kwamba mgawo wa umeme utakuwa historia lakini siku hadi siku sekta ya umeme imevuka upeo wa viongozi hawa kiasi cha kauli zao kupoteza imani kwa watanzania.
Leo tukiwa tunazungumza mgawo wa umeme, pembeni tunakabiliwa na deni la zaidi ya billioni 185 ambazo kwa uamuzi wa mahakama ya usuluhishi ya kimataifa (ICC) tunapaswa kuilipa kampuni ya Dowans, ambayo mpaka sasa serikali imekosa ujasiri kusema mmiliki wake ni nani lakini imekiri kushindwa kesi mahakama ya kimataifa.
Kwamba serikali isiyomjua wala kutambua uhalali wa mmiliki wa kampuni ya Dowans iko tayari kukiri kwa watanzania kuwa kampuni hiyo isiyojulikana mmiliki wake imeshinda kesi? Ni dhahiri kuwa Mahakama ya kimataifa yenye kuheshimika duniani kote haiwezi kukaa na kushiriki katika shauri ambalo Kampuni inayoshitaki haijulikani . Suala la umiliki wa Kampuni ya Dowans limekuwa likichezewa tu kwa maslahi ya makambi ya kisiasa ndani ya chama tawala.
Itakumbukwa pia kuwa mkataba ule ulikuwa ni wa miezi 24 na wenye thamani ya shs 172bn. Lakini kwa ukosefu wa uongozi na siasa duni ndani ya mfumo wa utawala wetu tunalipia shs 185bn tena bila kupata umeme. Billioni 185 zingetosha kuongeza 200MW za Umeme kwenye grid ya Taifa lakini sasa zinakwenda kulipwa kizembe. Huu ni unyama usio vumilika kwa watanzania maskini. Na ni unyama zaidii kwa watanzania masikini wa vijijini ambao asilimia 98 hawajui radha ya umeme lakini kodi zao sasa zinakwenda kutumika kijinga kabisa! Haiwezekani.
Mwanzoni mwa mwaka 2009 kulikuwa kuna mgogoro kuhusiana na ama TANESCO wanunue au wasinunue mitambo ya kampuni hii iliyotushinda kesi. Kundi moja la wabunge likisema isinunuliwe kwani itakuwa ni kukiuka sheria ya manunuzi (hakuna aliyethubutu kusema ni kifungu gani cha sheria ya manunuzi) na utata kuhusu mkataba wa Dowans(Hii ndio hoja ya msingi).
Kundi lingine lilikuwa likijenga hoja ya kununuliwa kwa mitambo ile ili kuepusha mgawo na vile vile iwe ni fursa ya kufuta kesi ambayo DOWANS waliifungulia TANESCO (mitambo ile ilikuwa inunuliwe kwa thamani ya shs 70bn). Kwa uamuzi tuliouchukua kama Taifa wa kutonunua mitambo ile, tunapaswa kulipa 185bn shs, mitambo wamebaki nayo na wataiuza watakapo baada ya uamuzi wa Mahakama Kuu kitengo cha Biashara kuamuru tarehe 22.10.2010 kuwa zuio la TANESCO dhidi ya Dowans kubeba mitambo ile lilikuwa batili. Mbaya zaidi Mgawo bado unaendelea na kuunyonya uchumi wa Taifa letu (bleeding the economy). Kinachosumbua hapa ni kwamba inawezekanaje serikali kushindwa kesi na kampuni ambayo tulielezwa mkataba wake ni batili( hapa ndio kuna siri nzito ndani ya serikali na chama tawala na ni siri hiyo nzito inayoendelea kukamua watanzania masikini mabilioni ya fedha ambayo yangepelekwa kwenye huduma za maji, Afya na Elimu).
MADHARA YA MGAWO

 • Uzalishaji viwandani : Shirikisho la wenye Viwanda nchini mara kwa mara limekuwa likieleza namna ambavyo wanachama wake wanaathirika na mgawo wa umeme. Mifano ya viwanda vya simenti imekuwa ikitolewa ambapo mgawo wa umeme unaongeza gharama za kuzalisha Simenti kwa kiwango cha dola za marekani 10 kwa kila mfuko wa kilo 50 wa Simenti na hivyo kuongeza gharama, kupata hasara na kushindwa kulipa kodi Serikalini.
 • Gharama za uzalishaji kuongezeka: Vijana wanaojishughulisha na kunyoa nywele jijini Dar es Salaam hupoteza zaidi ya asilimia 45 ya Mapato yao kutokana na kutumia majanereta ili kupata umeme wa kutoa huduma kwa wateja wao (REPOA report on electricity access for job creation 2010).
 • Bei za bidhaa kupanda kutokana na gharama za uzalishaji kuongezeka. Wafanyabiashara hujaribu kusukuma kuongezeka kwa gharama kwa walaji wa kawaida na hivyo kumdidimiza mwananchi wa kawaida. Maeneo ya vijijini ambapo hutegemea umeme kusaga nafaka zao kama Mahindi na Mpunga huathirika sana unapotokea mgawo kwa kutembea umbali mrefu kusaga nafaka na kwa gharama kubwa kutokana na gharama za mafuta ya kuendeshea majenereta kuwa kubwa.
 • Kusimama kwa shughuli nyingi za huduma kama benki, hospitali, vyuo na shule, na hata vyombo vya habari katika utendaji wake.

HATUA ZA KUCHUKULIWA.

  1. Serikali ione kwamba suala la mgawo wa umeme linaathiri maendeleo kuliko hata mtikisiko wa uchumi, hivyo ifanye maazimio magumu kwa kutenga fedha za kutosha kutekeleza mradi mkubwa wa umeme wa uhakika, kwa mfano Stigler’s gorge (2000MW), Mnazi Bay 300MW na kufufua KIWIRA 200MW. Miradi yote hii inaweza kuendeshwa na sekta Binafsi iwapo tutaweka mazingira mazuri ya uwezekezaji. Mifuko ya Hifadhi ya Jamii sasa iachane na kujenga majengo na ijielekeze kwenye uwekezaji wa uzalishaji umeme ili kutatua kabisa tatizo la umeme nchini kwetu.
  2. Kwa kuwa Serikali ndiyo iliyoielekeza TANESCO iingie mkataba na RICHMOND na baadae kuuhamisha mkataba kwa kampuni ya DOWANS. Vile vile kwa kuwa BUNGE ndio lililotoa azimio la kuvunjwa kwa mkataba na TANESCO kufanya hivy; Hivyo basi TANESCO wasibebeshwe chembe ya lawama katika suala hili. Mzigo huu ni mzigo wa Serikali unaotokana na ukosefu wa umakini, woga na kutowajibika kiuongozi kwa viongozi wa Serikali. Serikali haipaswi kujitenga na gharama zitokanazo na madhaifu ya TANESCO katika hatua zote kwani serikali ndio msingi wa matatizo yote ya TANESCO na hivyo inawajibika kubeba deni lote.
  3. Kwa kuwa Serikali itapaswa kulipa deni hili kutoka katika fedha za walipa kodi wa Tanzania na kwamba fedha hizi zitaondolewa katika bajeti ya Elimu, Afya na kadhalika, ni lazima Serikali itoe maelezo ya kina ya sakata zima mpaka kufika tulipofikia. Haiwezekani serikali itumie kodi ya wananchi kulipa deni la mabilioni ya fedha kwa kampuni ambayo serikali imeshindwa kuthibitisha uhalali wake na hata kutaja mmiliki wake.

  1. Kwakuwa Taifa linaingia hasara kubwa ya mabilioni haya ya fedha kutokana na udhaifu wa serikali kusimamia mikataba na mpango mzima wa nishati, nakusudia kupeleka hoja binafsi bungeni katika Bunge la Februari ya KWANINI SERIKALI ISIWAJIBIKE KWA KULINGIZA TAIFA HASARA KWENYE SEKTA YA UMEME.  1. Pamoja na mambo mengine na vile Bunge litaona inafaa, nitalitaka Bunge liazimie kupiga kura ya kutokuwa na imani na Waziri wa Nishati na Madini kwa kushindwa kusimamia utekelezaji wa Sera ya Nishati, na Mpango Kabambe wa usambazaji umeme (Power System Master Plan) na hivyo kusimamia migawo 3 ya umeme ndani ya miaka 2 ya uongozi wake.

Asanteni kwa kunisikiliza
Limetolewa na kusainiwa na;

David Zacharia Kafulila
Mbunge Jimbo la Kigoma Kusini :target:
0716 42 62 20
 
Buchanan

Buchanan

JF Diamond Member
Joined
May 19, 2009
Messages
13,211
Likes
385
Points
180
Buchanan

Buchanan

JF Diamond Member
Joined May 19, 2009
13,211 385 180
CCM huwa wanaangalia maslahi ya chama zaidi kuliko ya nchi, hivyo hiyo kura ya kutokuwa na imani ni unlikely! Pia Bunge lina uwezo Kikatiba na kikanuni kupiga kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu tu ambaye huwa anathibitishwa na Bunge akiteuliwa na Rais! Kwa upande wa mawaziri wengine hakuna sheria au kanuni inayotaka Bunge lipige kura ya kutokuwa na imani na Waziri (isipokuwa Waziri Mkuu).
 
M

mams

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2009
Messages
616
Likes
8
Points
35
M

mams

JF-Expert Member
Joined Jul 19, 2009
616 8 35
Hayo madai bila katiba mpya hayatashughulikiwa. Katiba mpya kwanza
 
E

Epifania

Senior Member
Joined
Oct 18, 2010
Messages
133
Likes
0
Points
0
E

Epifania

Senior Member
Joined Oct 18, 2010
133 0 0
Hilo la kutokuwa na imani na waziri mwenye dhamana nadhani linapaswa kwenda sambamba na kutokuwa na imani na mwanasheria mkuu wa serikali. Haiwezekani ashindwe kuishauri serikali wakati walipopawsa kufanya maamuzi. Sidhani kwamba hawakujua nini hatma ya maamuzi yao kisheria. It is such a shame.
Kuhusu 14% ya waTZ kuwa watumiaji wa umeme hatuhitaji kusubiri miujiza kuongeza hiyo idadi, hivi ni watanzania wangapi wenye uwezo wa kuvuta umeme ambao gharama kwa nguzo ni 1.2M? Fikiri mfanyakazi wa kawaida wa serikali ambaye amejipatia kiwanja pembeni ya mji kwa gharama nafuu na huduma ya umeme iko mbali, kupata umeme kwake ambako kunahitaji nguzo 2-3 itamlazimu kuchukua mkopo wenye riba. Swali linakuja, hivi iwapo mtu atakopa mkopo wa 3-4M ili avute umeme nyumbani, aendelee kulipa bili ambazo pia ni kubwa bila uzalishaji, huu si unyonyaji? Au tu-assume huyu mtu ananunua hiyo nguzo kama asset ambayo atajaiuza baadae?
Kuna habari kuwa kuna umeme unaozalishwa na makampuni ya ndani mf TPC, TANESCO inanunua kwao kwa bei gani na inamuzia mwanachi wa kawaida kwa bei gani? kweli Tanzania tunaangamia kwa kukosa maarifa.
 
N

ngoko

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2010
Messages
574
Likes
2
Points
0
N

ngoko

JF-Expert Member
Joined Oct 12, 2010
574 2 0
TAMKO LA MBUNGE WA KIGOMA KUSINI KUHUSU MGOGORO WA NISHATI YA UMEME NA KUSUDIO LA KUWASILISHA HOJA BINAFSI BUNGENI

JUMAPILI, DISEMBA05, 2010

Dar es Salaam.

UTANGULIZI
Karibuni wanahabari. Leo nimeamua kuwaomba kama wanahabari na watanzania wazalendo tujadili hatma ya Taifa letu ambalo utaratibu wa kuingizwa gizani na mgogoro wa nishati ya umeme unaelekea kukomaa na kuwa sehemu ya maisha ya watanzania.

Kwanza nipende kuwakumbusha tu kwamba tukiwa na nusu karne tangu tupate uhuru ni asilimia 14 tu ya watanzania ambao wanapata huduma ya umeme, kiwango ambacho ni sawa kabisa na takwimu za huduma hii kabla ya Uhuru takribani nusu karne iliyopita.Kwa vijijini kama jimboni kwangu na mkoa wa Kigoma kwa ujumla hali ni mbaya zaidi kwani kwa takwimu za sasa, ni asilimia 2 tu za watanzania vijijini wanaopata huduma ya umeme.
Lakini pia, tukumbuke kwamba bila nishati ya umeme ya uhakika hatuwezi kutekeleza MKUKUTA, hatuwezi kufikia MALENGO YA MILENIA, hatuwezi kufanikisha mpango wowote wa mapinduzi ama ya uchumi wala ya huduma. Takwimu mbalimbali na hata zile za Benki ya dunia zinaonyesha kuwa asilimia 40 ya uchumi duniani inategema nishati ya umeme.
Hapa Tanzania, kwa kasi ya ukuaji wa uchumi ya sasa ya takribani asilimia 7 kwa mwaka, uzalishaji wa Umeme unapaswa kukua kwa zaidi ya asilimia 15 kwa mwaka. Mahitaji ya Umeme nchini ni zaidi ya 1500 MW kwa mwaka, uwezo wetu ni kuzalisha 1034 MW lakini kiasi kinacho zalishwa ni 690MW tu kwa sasa kutokana na uchakavu wa mitambo na kupotea kwa umeme mwingi kwenye njia za kusafirisha. Hali hii ni mbaya sana kwa uchumi na inahitaji mikakati ya lazima kushughulikia.
Nikatika misingi hii watanzania tunawajibika kuwa wakali inapotokeo watu tuliowapa madaraka kutuongoza wanashindwa kutoa majibu ya msingi kuhusu masuala nyeti kama umeme.
Msingi mkubwa wa tatizo la umeme Tanzania ni serikali kufumbia macho miradi ya umeme ya uhakika ambayo ingetoa majibu ya kudumu ya tatizo hili na badala yake imebaki inasimamia sekta ya umeme kwa kudunduliza ikitumia mitambo ya kukodi ambayo kwa miaka sasa, tangu IPTL mwaka 1994 hadi Agreko, Songas, Richmond, Dowans imekuwa ikinyonya vibaya uchumi wa Taifa. Asilimia 86 ya mapato ya TANESCO yanatumika kulipia umeme unaozalishwa na mitambo ya kukodi ambayo inazalisha takribani asilimia 45 tu ya umeme wote. Hivi sasa mitambo ya kukodi inayotumika ni Songas na IPTL peke yake baada ya Agreko kumaliza mkataba wake na Dowans kufutwa mkataba wake. TANESCO wanailipa kampuni ya Songas takribani shilingi 266m kila siku kwa kununua 186MW za umeme. Mitambo ya IPTL ikiwa imewashwa TANESCO wanailipa kampuni hii shilingi 300m kila siku! Itakumbukwa kuwa TANESCO walikuwa wanapaswa kuilipa kampuni ya RICHMOND/DOWANS shilingi 152m kila siku kwa kununua 100MW za umeme.
Tangu mwaka 2006, serikali imeshindwa japo kupunguza tatizo hili la mgawo wa umeme. Viongozi wakuu wa serikali na hasa Waziri wa Nishati na Madini mara kadhaa wamekuwa akipotosha watanzania kuwa serikali inashughulikia kwamba mgawo wa umeme utakuwa historia lakini siku hadi siku sekta ya umeme imevuka upeo wa viongozi hawa kiasi cha kauli zao kupoteza imani kwa watanzania.
Leo tukiwa tunazungumza mgawo wa umeme, pembeni tunakabiliwa na deni la zaidi ya billioni 185 ambazo kwa uamuzi wa mahakama ya usuluhishi ya kimataifa (ICC) tunapaswa kuilipa kampuni ya Dowans, ambayo mpaka sasa serikali imekosa ujasiri kusema mmiliki wake ni nani lakini imekiri kushindwa kesi mahakama ya kimataifa.
Kwamba serikali isiyomjua wala kutambua uhalali wa mmiliki wa kampuni ya Dowans iko tayari kukiri kwa watanzania kuwa kampuni hiyo isiyojulikana mmiliki wake imeshinda kesi? Ni dhahiri kuwa Mahakama ya kimataifa yenye kuheshimika duniani kote haiwezi kukaa na kushiriki katika shauri ambalo Kampuni inayoshitaki haijulikani . Suala la umiliki wa Kampuni ya Dowans limekuwa likichezewa tu kwa maslahi ya makambi ya kisiasa ndani ya chama tawala.
Itakumbukwa pia kuwa mkataba ule ulikuwa ni wa miezi 24 na wenye thamani ya shs 172bn. Lakini kwa ukosefu wa uongozi na siasa duni ndani ya mfumo wa utawala wetu tunalipia shs 185bn tena bila kupata umeme. Billioni 185 zingetosha kuongeza 200MW za Umeme kwenye grid ya Taifa lakini sasa zinakwenda kulipwa kizembe. Huu ni unyama usio vumilika kwa watanzania maskini. Na ni unyama zaidii kwa watanzania masikini wa vijijini ambao asilimia 98 hawajui radha ya umeme lakini kodi zao sasa zinakwenda kutumika kijinga kabisa! Haiwezekani.
Mwanzoni mwa mwaka 2009 kulikuwa kuna mgogoro kuhusiana na ama TANESCO wanunue au wasinunue mitambo ya kampuni hii iliyotushinda kesi. Kundi moja la wabunge likisema isinunuliwe kwani itakuwa ni kukiuka sheria ya manunuzi (hakuna aliyethubutu kusema ni kifungu gani cha sheria ya manunuzi) na utata kuhusu mkataba wa Dowans(Hii ndio hoja ya msingi).
Kundi lingine lilikuwa likijenga hoja ya kununuliwa kwa mitambo ile ili kuepusha mgawo na vile vile iwe ni fursa ya kufuta kesi ambayo DOWANS waliifungulia TANESCO (mitambo ile ilikuwa inunuliwe kwa thamani ya shs 70bn). Kwa uamuzi tuliouchukua kama Taifa wa kutonunua mitambo ile, tunapaswa kulipa 185bn shs, mitambo wamebaki nayo na wataiuza watakapo baada ya uamuzi wa Mahakama Kuu kitengo cha Biashara kuamuru tarehe 22.10.2010 kuwa zuio la TANESCO dhidi ya Dowans kubeba mitambo ile lilikuwa batili. Mbaya zaidi Mgawo bado unaendelea na kuunyonya uchumi wa Taifa letu (bleeding the economy). Kinachosumbua hapa ni kwamba inawezekanaje serikali kushindwa kesi na kampuni ambayo tulielezwa mkataba wake ni batili( hapa ndio kuna siri nzito ndani ya serikali na chama tawala na ni siri hiyo nzito inayoendelea kukamua watanzania masikini mabilioni ya fedha ambayo yangepelekwa kwenye huduma za maji, Afya na Elimu).
MADHARA YA MGAWO • Uzalishaji viwandani : Shirikisho la wenye Viwanda nchini mara kwa mara limekuwa likieleza namna ambavyo wanachama wake wanaathirika na mgawo wa umeme. Mifano ya viwanda vya simenti imekuwa ikitolewa ambapo mgawo wa umeme unaongeza gharama za kuzalisha Simenti kwa kiwango cha dola za marekani 10 kwa kila mfuko wa kilo 50 wa Simenti na hivyo kuongeza gharama, kupata hasara na kushindwa kulipa kodi Serikalini.
 • Gharama za uzalishaji kuongezeka: Vijana wanaojishughulisha na kunyoa nywele jijini Dar es Salaam hupoteza zaidi ya asilimia 45 ya Mapato yao kutokana na kutumia majanereta ili kupata umeme wa kutoa huduma kwa wateja wao (REPOA report on electricity access for job creation 2010).
 • Bei za bidhaa kupanda kutokana na gharama za uzalishaji kuongezeka. Wafanyabiashara hujaribu kusukuma kuongezeka kwa gharama kwa walaji wa kawaida na hivyo kumdidimiza mwananchi wa kawaida. Maeneo ya vijijini ambapo hutegemea umeme kusaga nafaka zao kama Mahindi na Mpunga huathirika sana unapotokea mgawo kwa kutembea umbali mrefu kusaga nafaka na kwa gharama kubwa kutokana na gharama za mafuta ya kuendeshea majenereta kuwa kubwa.
 • Kusimama kwa shughuli nyingi za huduma kama benki, hospitali, vyuo na shule, na hata vyombo vya habari katika utendaji wake.

HATUA ZA KUCHUKULIWA.  1. Serikali ione kwamba suala la mgawo wa umeme linaathiri maendeleo kuliko hata mtikisiko wa uchumi, hivyo ifanye maazimio magumu kwa kutenga fedha za kutosha kutekeleza mradi mkubwa wa umeme wa uhakika, kwa mfano Stigler's gorge (2000MW), Mnazi Bay 300MW na kufufua KIWIRA 200MW. Miradi yote hii inaweza kuendeshwa na sekta Binafsi iwapo tutaweka mazingira mazuri ya uwezekezaji. Mifuko ya Hifadhi ya Jamii sasa iachane na kujenga majengo na ijielekeze kwenye uwekezaji wa uzalishaji umeme ili kutatua kabisa tatizo la umeme nchini kwetu.
  2. Kwa kuwa Serikali ndiyo iliyoielekeza TANESCO iingie mkataba na RICHMOND na baadae kuuhamisha mkataba kwa kampuni ya DOWANS. Vile vile kwa kuwa BUNGE ndio lililotoa azimio la kuvunjwa kwa mkataba na TANESCO kufanya hivy; Hivyo basi TANESCO wasibebeshwe chembe ya lawama katika suala hili. Mzigo huu ni mzigo wa Serikali unaotokana na ukosefu wa umakini, woga na kutowajibika kiuongozi kwa viongozi wa Serikali. Serikali haipaswi kujitenga na gharama zitokanazo na madhaifu ya TANESCO katika hatua zote kwani serikali ndio msingi wa matatizo yote ya TANESCO na hivyo inawajibika kubeba deni lote.
  3. Kwa kuwa Serikali itapaswa kulipa deni hili kutoka katika fedha za walipa kodi wa Tanzania na kwamba fedha hizi zitaondolewa katika bajeti ya Elimu, Afya na kadhalika, ni lazima Serikali itoe maelezo ya kina ya sakata zima mpaka kufika tulipofikia. Haiwezekani serikali itumie kodi ya wananchi kulipa deni la mabilioni ya fedha kwa kampuni ambayo serikali imeshindwa kuthibitisha uhalali wake na hata kutaja mmiliki wake.
  1. Kwakuwa Taifa linaingia hasara kubwa ya mabilioni haya ya fedha kutokana na udhaifu wa serikali kusimamia mikataba na mpango mzima wa nishati, nakusudia kupeleka hoja binafsi bungeni katika Bunge la Februari ya KWANINI SERIKALI ISIWAJIBIKE KWA KULINGIZA TAIFA HASARA KWENYE SEKTA YA UMEME.

  1. Pamoja na mambo mengine na vile Bunge litaona inafaa, nitalitaka Bunge liazimie kupiga kura ya kutokuwa na imani na Waziri wa Nishati na Madini kwa kushindwa kusimamia utekelezaji wa Sera ya Nishati, na Mpango Kabambe wa usambazaji umeme (Power System Master Plan) na hivyo kusimamia migawo 3 ya umeme ndani ya miaka 2 ya uongozi wake.Asanteni kwa kunisikiliza
Limetolewa na kusainiwa na;

David Zacharia Kafulila
Mbunge Jimbo la Kigoma Kusini :target:
0716 42 62 20
Mhe. Wazo ni zuri na ujumbe utakuwa umeufikisha mahali pake, wasiwasi wangu ni kuwa matokeo ya hiyo kura ya kutokuwa na imani yako wazi mno kwani watalindana kama chama.
 
B

Byendangwero

JF-Expert Member
Joined
Oct 24, 2010
Messages
872
Likes
5
Points
0
B

Byendangwero

JF-Expert Member
Joined Oct 24, 2010
872 5 0
Wazo ni zuri, kwa muda mrefu sasa serikali imekuwa inapoteza hela nyingi katika ulipaji wa capacity charge, fedha ambazo zingelielekezwa katika kuendeleza vyanzo vya umeme vyenye uhakika sasa hivi uhaba wa nishati hiyo hapa nchini ingelikuwa historia. Hata hivyo kwa mfumo wa sasa wa bunge letu uwezekano wa bunge kuibana serikali kwa suala hilo ni mdogo sana.
 
Forum statistics

Threads 1,237,407
Members 475,533
Posts 29,287,333