CHUAKACHARA
JF-Expert Member
- Jun 3, 2011
- 12,358
- 6,422
TAMKO LA MAASKOFU NA WACHUNGAJI
KUTOKA MADHEHEBU MBALIMBALI JUU
YA TUKIO LA ASKOFU GWAJIMA.
Sisi maaskofu na wachungaji kutoka
makanisa mbalimbali tumeshtushwa na
kusikitishwa kwa taarifa ya ugonjwa wa
Askofu na mtumishi mwenzetu Josephat
Gwajima ambaye tarehe 27/03/2015
alifika kituo cha polisi cha kati kuitikia
wito wa polisi uliomtaka kwenda kujibu
shutuma za kutumia lugha ya matusi kwa
kardinali Pengo.
Tumepata fursa ya kutafakari na kujadili
kwa kina hali iliyompata Askofu
mwenzetu hasa baada ya kuzingatia kuea
Askofu Gwajima alifika polisi akiwa
mzima na mwenye afya njema lakini
wakati wa akihojiwa na polisi, hali yake
ilibadilika ghafla kiasi cha kupelekea yeye
kulazwa hospitali ya TMJ akiugua tena
kwenye wodi ya wagonjwa mahututi
yaani (ICU) katika chumba cha uangalizi
maalum.
Maswali yetu makuu ni kitu gani
kimempata mwenzetu? Tunajiuliza, je
vyombo vya usalama vimekua sio sehemu
salama kama zamani?
Tukiwa bado tunatafakari hill,
tumeshtushwa tena baada ya kupata
taarifa ya kuwa Wachungaji Wasaidizi wa
Askofu Gwajima pamoja na walinzi wake
waliokuwepo hospitalini hapo kwa ajili ya
kumuuguza nao pia wamekamatwa kwa
tuhuma za. kutaka kumtorosha Askofu
Gwajima.
Jambo hili linashangaza zaidi maana
wachungaji wale wale waliokuwa naye
akiwa mzima wa afya wakati anaelekea
polisi ndio wale wale wanatuhumiwa
kutaka kumtorosha akiwa mgonjwa.
Ni jambo la kushangaza na lisiloingia
akilini kuwa wasaidizi hao wa Gwajima
walitaka kumtorosha wakati Gwajima
kama angekua na nia hiyo angekwisha
fanya hivyo mana alikuwa na uwezo wa
kutoroka alipokua Arusha kwenye kikao
cha Maaskofu wakuu wa makanisa ya
Kipentekoste ambao alipata taarifa za
kuitwa Polisi.
Isitoshe Gwajima aliitija wito na kwenda
polisi mwenyewe kwa miguu yake bila
kushurutishwa, wala hakufikishwa polisi
kwa nguvu.
Swali: Kama alikua anaona ugumu wa
kutoroka wakati hakuna polisi
anayemlinda na huku akiwa mwenye afya
tele, itakuaje rahisi kutoroshwa leo akiwa
mahututi na akiwa kwenye ulinzi mkali
wa polisi?
Mbona hii inastaajabisha?
Jambo jingine linalotupa shida ni kuhusu
mlalamikaji wa kesi hii inayomkabili
Askofu Gwajima. Tumeelezwa na
wasaidizi wa Askofu Gwajima kuwa pale
polisi walielezwa kuwa aliyefungua kesi
hii sio Pengo ila mtu mmoja aitwaye
Aboubakar.
Kwa ufahamu wetu juu ya sheria
unatutuma kuamini kuwa Aboubakar sio
MTU sahihi wa kufungua kesi hiyo sababu
hawezi kutuonyesha ameumizwa kiasi
gani na matamshi ya Askofu Gwajima.
Isitoshe, Kardinali Pengo mwenyewe
ametamka katika Ibada yake ya Jumapili
hii ya tarehe 29/03/2015 kuwa
amemsamehe Gwajima, yupi tena mwenye
uchungu wa kumzidi Kardinali Pengo?
RAI YETU:
Rai yetu ni kwamba, ni vizuri serikali
pamoja na vyombo vyake vya usalama
vikatumia weledi katika kushughulikia
mambo ya kidini na viongozi wake kwani
yanaweza kusababisha chuki dhidi ya
serikali na pia kupelekea mpasuko
mkubwa wa kidini katika jamii yetu iliyo
na historia nzuri ya umoja na
mshikamano na ushirikiano katika
matukio yote ya kimaisha.
Tunaomba serikali isaidie kuondoa
mkanganyiko huu na busara kubwa
itumike ili kuepusha uvunjifu wa Amani
katika jamii.
MAAMUZI YETU:
Jambo hili linazungumzika, maana hata
hivyo tumeshaazimia kukutana na IGP ili
kupata suluhisho juu ya jambo hili.
Kwa niaba ya maaskofu na wachungaji:
Mwenyekiti: Askofu Dr. Mgullu Kilimba
Katibu: Askofu Dr. Dramas Mukassa
Askofu wa makanisa gani hao in red