Tamko la Maaskofu na Wachungaji wa Kipentekoste juu ya kuugua ghafla kwa Askofu Gwajima

Pamoja na Askofu Pengo kutamka kumsamehe Gwajma, na pia familia ya Gwajma pamoja na viongozi mbalimbali wa kidini kumsihi amwombe askofu Pengo msamaha, Gwajma anapaswa kuvuliwa uaskofu ili kulinda heshima ya ukristo duniani.
 
Gwajima alisema kweli, ila tu alizindisha kwa Hasira alokuwa nayo. Pengo ndiye avuliwe Uaskofu wa jimbo kuu la Dar kwa kuwadhalilisha Maaskofu wengine pamoja na Kanisa Katoliki kwa "kuufyata" mbele ya 'homeboy' wake Pinda. Ukabila ulimponza.Kuna msemo unaosema kuwa "Ukiwa mtupu huku umevaa Msuli usikwee kwenye mti"
 
Pamoja na Askofu Pengo kutamka kumsamehe Gwajma, na pia familia ya Gwajma pamoja na viongozi mbalimbali wa kidini kumsihi amwombe askofu Pengo msamaha, Gwajma anapaswa kuvuliwa uaskofu ili kulinda heshima ya ukristo duniani.

Ukristo sio dini ya kulazimishana kwa mapanga. Mungu ndie atakayejua kama kakosea na azabuyake kama kakosea.
 
Daaaah abourbakar kaanza lini kua pengo
hapana, Aboubakari anamapengo, sasa alivyosikia gwajima kamtukana pengo alifikiri ni mapengo yake, akakimbilia polisi, sasa kama unavyojua polisi wetu asilimia kubwa ni darasa la saba na wale wa form 4 walapata fail, kwa maana hiyo kichwa kiko wazi, wakachulia kesi kikichwa kichwa tu. Ata hao polisi ukiwauliza kesi inahusu nini hawajui, ndo maana walikuwa wanamuhoji maswali yasio husiana na kesi husika kabisa. Baada ya kuwa kituoni wakubwa kadhaa wenye chuki ya kisiasa na jamaa wakaona hapo ndo mahali pa kummaliza ndo unaona hayo mambo sijui kumtorosha, mara bastola, yote ni plan iliyopangwa kisiasa zaidi, hapa wala Pengo mwenyewe hausiki.
 
Pamoja na Askofu Pengo kutamka kumsamehe Gwajma, na pia familia ya Gwajma pamoja na viongozi mbalimbali wa kidini kumsihi amwombe askofu Pengo msamaha, Gwajma anapaswa kuvuliwa uaskofu ili kulinda heshima ya ukristo duniani.

Kwa taarifa kama ulikua huna pia, Msamaha alioutoa Pengo ni kutokana na shinikizo alilopewa na Baraza la Maaskofu wa Kikatoliki kwani kimaadili Pengo ndio mwenye kosa na chanzo cha haya yote kutokea.

Kwani Askofu Mkuu wa Kikatoliki ndio mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu Tanzania na alikuwepo kupitisha TAMKO la awali la maaskofu kwahiyo Pengo amemdharau hadi kiongozi wake which means Pengo ameyakana maamuzi yake mwenyewe.

Usiongee usichojua na tafuta wakatoliki wenye akili ndio watakufumbua macho achana na hawa wanaokurupuka humu.
 
hapana, Aboubakari anamapengo, sasa alivyosikia gwajima kamtukana pengo alifikiri ni mapengo yake, akakimbilia polisi, sasa kama unavyojua polisi wetu asilimia kubwa ni darasa la saba na wale wa form 4 walapata fail, kwa maana hiyo kichwa kiko wazi, wakachulia kesi kikichwa kichwa tu. Ata hao polisi ukiwauliza kesi inahusu nini hawajui, ndo maana walikuwa wanamuhoji maswali yasio husiana na kesi husika kabisa. Baada ya kuwa kituoni wakubwa kadhaa wenye chuki ya kisiasa na jamaa wakaona hapo ndo mahali pa kummaliza ndo unaona hayo mambo sijui kumtorosha, mara bastola, yote ni plan iliyopangwa kisiasa zaidi, hapa wala Pengo mwenyewe hausiki.

Hahahahhahahahahahahahahaha
Kweli x7 ndo kinachotesa police wetu
 
Huyu muhuni gwajima si anajifanya anaombea watu wanapona sasa imekuwaje hajui kujiombea mwenyewe apone mpaka aende TMJ?
Lingine hata pengo kama kasamehe hilo ni la pengo sheria haisemi mkosaji akisha samehe basi na sheria nayo isamehe.
Jikumbusheni yule muhuni alie mzaba kibao mzee mwinyi.
Mzee mwinyi alimsamehe lakini sheria ilichukuwa nafasi yake.
Mm sio mkiristo lakini sikubaliani na matusi ya gwajima kwa mzee pengo hasa ukizingatia huyu gwajima anajiita sijui askofu sijui mtume sasa kama askofu unakuwa mpuuzi kiasi kile waiumini wako watakuwaje?
Acheni sheria ifuate mkondo wake musitake kutisha serikali kwa migongo ya dini.
Kumbukeni yanayo mkuta she Ponda na watu wa uwamsho.
 
unnamed%252520%2525281%252529.jpg

TAMKO LA MAASKOFU NA WACHUNGAJI KUTOKA MADHEHEBU MBALIMBALI JUU YA TUKIO LA ASKOFU GWAJIMA.

Sisi maaskofu na wachungaji kutoka makanisa mbalimbali tumeshtushwa na kusikitishwa kwa taarifa ya ugonjwa wa Askofu na mtumishi mwenzetu Josephat Gwajima ambaye tarehe 27/03/2015 alifika kituo cha polisi cha kati kuitikia wito wa polisi uliomtaka kwenda kujibu shutuma za kutumia lugha ya matusi kwa kardinali Pengo.

Tumepata fursa ya kutafakari na kujadili kwa kina hali iliyompata Askofu mwenzetu hasa baada ya kuzingatia kuea Askofu Gwajima alifika polisi akiwa mzima na mwenye afya njema lakini wakati wa akihojiwa na polisi, hali yake ilibadilika ghafla kiasi cha kupelekea yeye kulazwa hospitali ya TMJ akiugua tena kwenye wodi ya wagonjwa mahututi yaani (ICU) katika chumba cha uangalizi maalum.

Maswali yetu makuu ni kitu gani kimempata mwenzetu? Tunajiuliza, je vyombo vya usalama vimekua sio sehemu salama kama zamani?

Tukiwa bado tunatafakari hill, tumeshtushwa tena baada ya kupata taarifa ya kuwa Wachungaji Wasaidizi wa Askofu Gwajima pamoja na walinzi wake waliokuwepo hospitalini hapo kwa ajili ya kumuuguza nao pia wamekamatwa kwa tuhuma za. kutaka kumtorosha Askofu Gwajima.

Jambo hili linashangaza zaidi maana wachungaji wale wale waliokuwa naye akiwa mzima wa afya wakati anaelekea polisi ndio wale wale wanatuhumiwa kutaka kumtorosha akiwa mgonjwa.

Ni jambo la kushangaza na lisiloingia akilini kuwa wasaidizi hao wa Gwajima walitaka kumtorosha wakati Gwajima kama angekua na nia hiyo angekwisha fanya hivyo mana alikuwa na uwezo wa kutoroka alipokua Arusha kwenye kikao cha Maaskofu wakuu wa makanisa ya Kipentekoste ambao alipata taarifa za kuitwa Polisi.
Isitoshe Gwajima aliitija wito na kwenda polisi mwenyewe kwa miguu yake bila kushurutishwa, wala hakufikishwa polisi kwa nguvu.

Swali: Kama alikua anaona ugumu wa kutoroka wakati hakuna polisi anayemlinda na huku akiwa mwenye afya tele, itakuaje rahisi kutoroshwa leo akiwa mahututi na akiwa kwenye ulinzi mkali wa polisi?

Mbona hii inastaajabisha?
Jambo jingine linalotupa shida ni kuhusu mlalamikaji wa kesi hii inayomkabili Askofu Gwajima. Tumeelezwa na wasaidizi wa Askofu Gwajima kuwa pale polisi walielezwa kuwa aliyefungua kesi hii sio Pengo ila mtu mmoja aitwaye Aboubakar.
Kwa ufahamu wetu juu ya sheria unatutuma kuamini kuwa Aboubakar sio MTU sahihi wa kufungua kesi hiyo sababu hawezi kutuonyesha ameumizwa kiasi gani na matamshi ya Askofu Gwajima.

Isitoshe, Kardinali Pengo mwenyewe ametamka katika Ibada yake ya Jumapili hii ya tarehe 29/03/2015 kuwa amemsamehe Gwajima, yupi tena mwenye uchungu wa kumzidi Kardinali Pengo?

RAI YETU:
Rai yetu ni kwamba, ni vizuri serikali pamoja na vyombo vyake vya usalama vikatumia weledi katika kushughulikia mambo ya kidini na viongozi wake kwani yanaweza kusababisha chuki dhidi ya serikali na pia kupelekea mpasuko mkubwa wa kidini katika jamii yetu iliyo na historia nzuri ya umoja na mshikamano na ushirikiano katika matukio yote ya kimaisha.
Tunaomba serikali isaidie kuondoa mkanganyiko huu na busara kubwa itumike ili kuepusha uvunjifu wa Amani katika jamii.

MAAMUZI YETU:
Jambo hili linazungumzika, maana hata hivyo tumeshaazimia kukutana na IGP ili kupata suluhisho juu ya jambo hili.
Kwa niaba ya maaskofu na wachungaji:
Mwenyekiti: Askofu Dr. Mgullu Kilimba
Katibu: Askofu Dr. Dramas Mukassa
 
Pamoja na mambo mengine kuna sababu ya kupitia upya huu uhuru wa kuabudu uliopitiliza....Gwajima aje mbele ya jamii aombe radhi kwa kutoa matamshi yasiyokuwa ya kiungwana ilihali akijua yeye ni mtumishi na kwamba ana wafuasi wengi na kwamba aliyetolewa matamshi hayo ni kiongozi pia ambaye angeweza kuwasiliana naye kwa njia ya kistaarabu!
 
Kumbe siku hizi tunamaaskofu wajinga kiasi hiki siamini kama ndiyo viongozi wa dini kumbe ni makundi ya wahuni tu.
 
Pamoja na mambo mengine kuna sababu ya kupitia upya huu uhuru wa kuabudu uliopitiliza....Gwajima aje mbele ya jamii aombe radhi kwa kutoa matamshi yasiyokuwa ya kiungwana ilihali akijua yeye ni mtumishi na kwamba ana wafuasi wengi na kwamba aliyetolewa matamshi hayo ni kiongozi pia ambaye angeweza kuwasiliana naye kwa njia ya kistaarabu!
Huu uhuru wa kuabudu unakwenda mbali sasa Lazima sheria zikazwe zaidi kwa hawa wachungaji wahuni kama gwajima na wenzake.
 
Ndugu Simiyu Yetu nakubaliana na wewe kabisa. Ni upuuzi tu hawa wanataka kuujenga. Wameachiwa kuanzisha madhebu ya kipuuzi na sasa wanataka kutetea upuuzi. Acha polis na mahakama wafanye kazi yao. Sioni tatizo la polisi na serikali hapa
 
Back
Top Bottom