Elections 2015 Tamko la Edward Lowassa Baada ya NEC Kumtangaza Dr Magufuli Kuwa Mshindi wa Kiti cha Urais

RobyMi

JF-Expert Member
Mar 4, 2012
848
862
attachment.php




Watanzania wenzangu!
Leo tarehe 29 October 2015, kwa kupitia Mgombea Mwenza wangu, Mh. Juma Duni Haji nimewasilisha rasmi malalamiko yetu kuhusu mwenendo mzima wa uchaguzi mkuu wa 2015 kwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi.

Tumeainisha kwenye malalamiko yetu, kutokuridhishwa kwetu na mwenendo na matukio mbalimbali, hususani, utangazaji wa matokeo batili, yasiyo akisi matokeo halisi yaliyopatikana kwenye vituo vya kupiga kura, kama ifuatavyo.

? Upunguzwaji wa kura zangu
? Kuongeza kura kwa mgombea wa CCM
?Tunaendelea kukataa dhuluma hii dhidi ya matakwa ya wananchi, na jaribio la kutaka kubakwa kwa Demokrasia kunakooneka wazi kutokana na mwenendo wa Tume kuendelea kutangaza matokeo ya kura yasiyo ya kweli kwa kupoka ushindi wetu.

Aidha, kumekuwepo pia na uporaji wa ushindi kwa wagombea wa vyama vya UKAWA kwenye ngazi ya Ubunge na Udiwani

Kama tulivyoeleza jana takwimu zetu sisi zilionesha kwamba nilikua naongoza kwa zaidi ya 67%,na sasa tumejiridhisha kwamba nimepata kura 10,268,795 sawa na asilimia 62% baada ya kukamilisha kazi ya kukusanya fomu za matokeo nchi nzima.

Kwa hali hii, ninaitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi initangaze mara moja mimi EDWARD NGOYAI LOWASSA kuwa mshindi wa nafasi ya Urais wa Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania.

Naendelea kuwashukuru wananchi kwa imani yenu kwangu na kunichagua, MImi, pamoja na viongozi wenzangu tunaamini kuwa kuchezea Demokrasia ni kuvunja Amani, lakini sote tunatambua ni nyie watanzania ndio mnaoporwa haki yenu ya kupata mabadiliko, na viongozi mnao wahitaji, hivyo nitaendelea kuwa pamoja na watanzania wote kudai haki yenu kwa nguvu zote.

Tanzania kwa miaka mingi imefahamika kama kisiwa cha amani katika Afrika, tunashangaa leo kuona vyombo vya ulinzi na usalama vikitanda kila mahali wakiwa na silaha za kivita mitaani kana kwamba uchagzui ni vita, hii ni kuwatisha wananchi ili wakubali kunyang?anywa haki yao ya msingi ya kuchagua viongozi wanao wataka, nina amini watanzania hatutakubali hali hiyo.

Lowassa, Edward Ngoyai.
29.10.2015


Tamko la Edward Lowassa Baada ya NEC Kumtangaza Dr Magufuli Kuwa Mshindi wa Kiti cha Urais - MPEKUZI
1.jpg
 
Last edited by a moderator:
Mzee Lowassa kwenye Kanisa lile ulilolipora Uwanja pale Mbezi , tulimwomba Mungu na ametusikia Juu ya Amani.
Tena tuliimba na wimbo wa Taifa kwa machozi.
Huna jinsi uende zako tu maana unavuna ulichopanda
 
Kwani bado haamini tu kama Rais wa Tanzania ni @dr john magufuli ..??

Tafadhari nyie vijana mlio mzunguka mzee white hair msimpotosheni
mwambie kitu tayari na mpira umekwiiiiishaaaa......
 
Last edited by a moderator:
jamaa ananipa raha sana mpaka wanavamia kituo chao cha kukusanya kura hata majimbo 5 yalikuwa bado hayajatangaza matokeo.

ni lini upinzani uliwahi kukubali kushindwa Tz kama vp akaushe tumesha mchoka.
 
Na pamoja na kuwa na wachunguzi wa uchaguzi kutoka nchi za Ulaya lakin bado haki inapokonywa na wao kuwa kimya tu...Wamegeuka waandishi wa habari wa vyombo vyao badala ya kusimamia haki...
 
RobyMi

Je, hukujua namna tume ya uchaguzi inavyopatikana kabla hujakubali kushiriki uchaguzi? Uchaguzi huu ni matunda ya katiba mbaya na ugomvi binafsi kati ya Lowassa na Kikwete.
 
Last edited by a moderator:
Haya ilibidi uyafanyie kazi kabla ya kuungua uchaguzi mkuu huu. Vinginevyo business as usual.
 
Kwa akili yake alikuwa anategemea kushinda urais wa tz, yy akapumzike monduli, kwani kibarua tumempatia Dr.Makufuli

Mafuriko yooote yalielekezwa baharini tangu tar24 ni mwendo wa kuchuana kwa kura tuu na sasa ni kusherehekea tuu ushindi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom