MSAGA SUMU
JF-Expert Member
- May 25, 2015
- 6,719
- 21,954
TANGAZO:
YAHUSU UPATIKANAJI WA FEDHA ZA MAFUNZO KWA VITENDO (FIELD)
Ndugu WanaUDSM, Serikali ya wanafunzi ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(DARUSO) kupitia Wizara ya Mikopo imefatilia kwa kufuata taratibu zote na kupitia ngazi zote zinazotakiwa kufuatwa kwa ajili ya kupata fedha za kujikimu wakati wa mafunzo kwa vitendo.
Kwa ufuatiliaji huo tulihakikishiwa na Bodi ya mikopo kuwa fedha ingeingia kwenye akaunti za wanafunzi wiki hii kitu ambacho hakijatekelezwa mpaka sasa.
Ndugu wanaUDSM, Serikali ya wanafunzi (Daruso) iliahidi kuwa hatutoenda nyumbani wala kwenye mafunzo kwa vitendo bila kupewa Fedha zetu.
Serikali ya wanafunzi inaendelea kuwahakikishia wanadaruso kuwa ahadi na kauli hiyo ipo HAI na ndio msimamo wa serikali.
UMOJA WETU NDIO NGUVU YETU, na NDIO USHINDI WETU.
Serikali inapenda kuwaasa na kuwakumbusha kuwa waliomaliza mitihani leo tarehe 26/06/2015 na watakaomaliza mitihani kabla ya tarehe 03/07/2015 TUSIONDOKE CHUO kabla ya kupata mustakabali wa pamoja kwenda kokote bila kupatiwa Fedha zetu zote tukiwa hapahapa chuoni.
MSISITIZO: Serikali inawahakikishia kuwa jitihada za dhati bado zinaendelea na tutazidi kupeana taarifa.
UNITY IS POWER
Ofisi ya Waziri Mkuu-DARUSO